Mkondakaiye
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 838
- 174
Kwa siku za karibun, Nimekuwa nikifuatilia kwa umakin sana maneno yanayozungumzwa na viongozi wa Chadema kwenye mikutano na kugundua kuwa wamekuwa wakimtaja Mungu mara kwa mara.wanaonekana kutuaminisha kuwa kila wanachofanya wanatumia nguvu za mungu.Mungu hatumiwi kwa namna hiyo.MUNGU ANA MAHALI PAKE PA KUMTAJA TAJA.Itafika wakati mtu akiruhusu kuwa tegemiz sana kwa Mungu hukosa uwezo wa kujituma ktk kufanikisha jambo eti Mungu hajamjalia.Mungu husingiziwa kwa kila dosari au mafanikio.nashauri ktk majukwaa Mungu asitajwe kihivyo na chadema.tuige mfano wa MWALIMU NYERERE alikuwa mhudhuriaji sana ibada lakini ktk majukwaa ya kisiasa hakumtaja Mungu.
Wewe utakuwa umetumwa na askofu leizer aliyeshangilia lema kuvuliwa ubunge
Wanataka wananchi wawaonee huruma...hizi njaa ni mbaya sana!
Well,mkuu hutakiwi kuwa mlokole kumtaja mungu na hutakiwi kutokuwa mwanasiasa kumtaja mungu.Mkuu naomba unieleweshe nipate kujua.
Mungu ni kichaka cha wazembe na wanaotaka ku manipulate wenzao.
Hilo ndio tatizo letu kubwa humu jamvini badala ya kujibu hoja anakuambia umetumwa sasa sijui na wewe umetumwa na nani.
Well,mkuu hutakiwi kuwa mlokole kumtaja mungu na hutakiwi kutokuwa mwanasiasa kumtaja mungu.
Wewe tunakujua kuwa ni Atheist!
mungu gani unayemzunguzia? kwa mungu wa ukweli uzembe na uvivu ni dhambi kubwa...asiyefanya kazi na asile...nadhani unamzungumzia mungu wa tunguri za nigeria tunaomuona vijiweni kila uchao...!Mungu ni kichaka cha wazembe na wanaotaka ku manipulate wenzao.
Ni kweli kabisa mkuu unavosema, kwenye public mungu hana surname wala initial, so kama wanamtaja kiivo ilihali kuna watu wa dini mbalimbali basi laweza kuwa kosa.Mkuu nashukuru kwa kunifahamisha...mkuu kuna vitu vingine ni vya imani kwa upande wako unaweza kuona ni vya kawaida sababu akikuhusu.
Unaposema Mungu wa Yakobo na Mungu wa Yohana ndio Mungu Chadema.
Uoni kama unawagawa wapenzi wa Chadema ambao hawaamini hivyo?
Kwa nini usiseme Mungu wa wote?
Watu wanatumia Mungu kupumbaza wenzao tu
kuchangia thread na watu wenye akili hizi yataka uwe na moyo wa maiti.Sio yule mungu anayeishi mjini Makka?
kumbe hujajua kwanini cc chadema tunamwomba Mungu,this is becoz chama che2 ni cha kanisa, na ndiyo maana kwenye mikutano ye2 ha2kosi maaskofu wawili wa3.
Kabla hatujahoji Mungu atayetajwa na CDM, tujue Mungu:
-wanasali bungeni ni yupi
-tunayeimba kwenye national anthem
-anayetajwa kila mwisho wa hotuba ya rais n.k
Tunajadili jambo lisilotujenga na kutushikamanisha! Sioni tatizo la wafanyacho CDM, maana Mungu anahusika sana na taifa letu