Je kwa soka hili bongo tunaenda wapi?

Je kwa soka hili bongo tunaenda wapi?

Kateka Sanza

Member
Joined
Jun 8, 2013
Posts
44
Reaction score
8
Ndugu zangu Watanzania ni mda mrefu toka timu kubwa mbil Tanzania zimeanzishwa lakin mi naona hazina mipango endelevu zaidi ya kunga'anga'niana wachezaj na kuwasajir uwanja wa ndege! Hivi tutatoka lin hapa tulipo? Juz nimeckia kuna timu inaenda nje ya nchi kwa mapumuziko lakin sijasikia ujenz wa viwanja vya kisasa kwa timu hiz Yanga na Simba kama Azam kule Chamaz! Sasa najiuliza je kuna mpango wa kuendeleza soka Tanzania au ndo siasa imevamia! Wadau naomba kuwasilisha.
 
We unaiunga mkono timu ipi kati ya zote zilizoshiriki ligi kuu msimu uliopita,nitarudi baadaye.
 
Mkuu wangu NGANU, mdau wetu aliyeanzisha mada ni mshabiki wa SIMBA.
Maana kama kweli tunataka kuendeleza mpira na tunaona kwamba YANGA na SIMBA hazileti mabadiliko tufanyeje? Tuendeleze timu za mikoani ili zilete changamoto. Tayari AZAM wameleta changamoto nzuri. Mwaka jana walikuwa nambari 2 na YANGA ikawa nambari 3. Mwaka huu AZAM imekuwa nambari 2 na SIMBA imekuwa nambari 3.Nafikiri tunaelekea upande sahihi lakini huenda tukachelewa kufika. Maana hata Uingereza wanagombea kusajili wachezaji 'uwanja wa ndege' niambie mchezaji gani maarufu ambaye ametokana na akademi za michezo nchini Uingereza? SUAREZ, VAN PERSIE, CISSE, BA, CARZOLA, ARTETA, DZEKO, KUN AGUERO, DZEKO, wachezaji hao wote walisajiliwa 'uwanja wa ndege'. Ligi ya UJERUMANI: LEWANDOSKI, ROBEN, RIBERY, hao wote walisajiliwa 'uwanja wa ndege'. Ligi ya HISPANIA: CRISTIANO RONALDO, OZIL, BENZEMA, KHEDIRA, ALONZO, DI MARIA, NEYMAR, SANCHEZ, hao wote walisajiliwa 'uwanja wa ndege' Ingawa mpira ni mchezo, siku hizi mpira unalenga biashara zaidi. Ndo maana SAMATTA NA ULIMWENGU wako TP MAZEMBE, wakati MBUYU TWITE ametoka KONGO anacheza Tanzania! Naomba kuwasilisha.
 
Kwa Tz siasa na mpira ni chanda na kidole..........
 
Budget ya wizara ya michezo ni 600million nadhan bado tunapishana na mafanikio ya soka sio SIMBA NA YANGA wala Azam wanaotaka kubadilisha mpira wa Tanzania. Nawasilisha wadau...
 
We, Azam sio wakuwafananisha na hao wapumbavu wako. Azam ina kila kitu kinacho hitajika kwenye club.
 
kimsingi suala la kujenga kiwanja cha kisasa sio jambo la kawaida,garama kubwa sana inahitajika,istoshe zingatieni uchumi wa nchi hii,alafu timu hizi kubwa mbili kumbuka sio timu zinazomilikiwa watu binafsi km ulaya. hivyo vyanzo vya mapato ni vidogo na hata wakiingia mkataba na makampuni makubwa ni vigumu baadae kurudisha gharama hizo. TFF km shirikisho halina uwnja wake sembuse vilabu vyetu
 
kimsingi suala la kujenga kiwanja cha kisasa sio jambo la kawaida,garama kubwa sana inahitajika,istoshe zingatieni uchumi wa nchi hii,alafu timu hizi kubwa mbili kumbuka sio timu zinazomilikiwa watu binafsi km ulaya. hivyo vyanzo vya mapato ni vidogo na hata wakiingia mkataba na makampuni makubwa ni vigumu baadae kurudisha gharama hizo. TFF km shirikisho halina uwnja wake sembuse vilabu vyetu

Mkuu philosophy, nianze na heshima kwako. Nina hoja kadhaa ambazo zitapingana nawe.

1) Swala la uwanja wa kisasa ni gharama kubwa, Hata uwanja wa mazoezi mkuu, are you serious ?
2) Swala si kumilikiwa na watu binafsi au kampuni bali ni uongozi wenye mipango. Mimi si mtaalam wa uchumi ila wataalam wameshashauri sana. Simba na Yanga ni Migodi inayotembea, ni utajiri tosha kutokana na idadi kubwa ya wapenzi wake na Kuna njia kadhaa za kuingiza Pesa. Mkuu hivi unafikiri kwa nini wamiliki wa Facebook au google ni matajiri? Simply ni rasilimali watu wanaitumia mitandao na kampuni kujinufaisha kibiashara kwa kupitia matangazo.
3) Hivi Yanga na Simba walijenga vipi majengo yao? Hapo ndio utajua clab zinakopesheka. Ila ujanja ujanja na ubabaishaji wa viongozi wetu ni tatizo kubwa.

Kwa sasa niisihie hapo mkuu, unaweza kunirekebisha
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom