Je Kunapwaya??

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
49,282
19,616

(Picha kwa hisani ya Africabythebay)

Pubococcygeus muscle
[h=1](PC muscle)[/h]
Si kawaida katika maisha ya kila siku ikatokea mtu kuwa na funguo ambazo ukiwa nazo unaweza kufungua mlango wa kila tatizo na kuingia kutatua.
Hata hivyo kwenye suala la misuli PC, ikifanyiwa zoezi la Kegel imetoa majibu ya kushangaza kwa wanandoa wengi na kujisikia kama vile wamepata ufungua wa kufungua milango yote ya matatizo ya tendo la ndoa.
Wanawake wengi ambao kutokana na kufanya zoezi la kegel kuimarisha misuli ya PC kumewafanya kuridhika na tendo la ndoa kwa kufika kileleni kitu ambacho kwao lilikuwa giza nene na sasa hawana shaka na hili na wanaendelea kuenjoy mapenzi katika ndoa zao.

Mwaka 1940 Dr. Arnold H. Kegel mtaalamu wa magonjwa ya wanawake alitembelewa na mgonjwa aliyejulikana kwa jina la Doris Wilson.Huyu mama alikuwa na tatizo baada ya kuzaa mtoto wake wa tatu ilikuwa kwamba kila kibofu chake cha mkojo kikijaa tu basi akicheka tu, au akikohoa tu, au akiruka tu ghafla mikojo anaanza kuchuruzika yenyewe bila uwezo wa kuizuia. Hivyo alianza kuvaa pad ili kujizuia na mikojo tatizo ambalo lilimpeleka kwa Dr. Kegel.
Kutokana na uchunguzi wa Dr. Kegel aligundua kwamba tatizo lake linasababishwa na kulegea kwa misuli inayozuia mikojo isitoke bila matatizo na hivyo alihitaji upasuaji.
Lakini kabla ya kufanya upasuaji alimshauri afanye mazoezi ya kuimarisha hiyo misuli iliyokuwa dhaifu.

Doris Wilson alifanya mazoezi kwa muda wa miezi miwili na hiyo hali ilikoma pia Doris aligundua kitu kingine cha tofauti na cha kushangaza, kwani kwa miaka 15 katika ndoa yake hakuweza kufika kileleni (orgasm), pia kila aliyefanya hili zoezi alikuwa na the same story kwamba maisha ya sex yamekuwa ya ajabu, so sweet and satisfying.
[h=3]Misuli ya PC ipo wapi?[/h]
Hii misuli imeunganisha miguu na base ya kushika matundu matatu yaani kibofu, uke na rectum.
Wakati wa kuzaa hii misuli huweza kulegea kama ilivyotokea kwa Doris, hivyo kushika kuthibiti mkojo ukijaa kwenye kibofu kutoka, pia kuweza kushika uume ukiwa ndani ya uke kitendo ambacho husababisha uke kuonekana mkubwa na kushindwa kushika vizuri uume ukiwa ndani kiasi ambacho husababisha msuguano kuwa mdogo na tendo kutokuwa tamu.
Wanawake wengi hulalamika kwamba sehemu zao (uke ) ni kubwa sana kiasi kwamba mume wake akiingiza uume unapwaya na inakuwa ngumu sana kufurahia tendo la ndoa.
Dawa ni kufanya mazoezi ya Kegel ili kukusaidia misuli kukaza.
[h=3]Kazi za misuli ya PC kwa wanawake[/h]Kuwa na misuli imara ya PC husaidia sana mwanamke
Kufurahia utamu wa sex
Hii misuli huongeza pressure na msuguano unaotoa resistance nzuri wakati wa tendo la ndoa bila kujali size ya uume. (kuongeza mnato)
Kusisimka haraka kwa ajili ya tendo la ndoa.
Kuwa wet mapema wakati wa foreplay.
Huongeza enjoyment ya sex kwa wote mwanaume na mwanamke.
Huimarisha mwili wa mwanamke hasa:-


Wakati wa kuzaa kwa kutopata injuri zozote na usalama wa mtoto anayezaliwa pia kuelekeza vizuri kichwa cha mtoto wakati wa kuzaa.
Kuthitibi kibofu cha mkojo wakati wa kukojoa.
Hupunguza backaches
[h=2]Kazi ya misuli ya PC kwa wanaume[/h][h=2]Kusaidia jogoo kuwika kwa muda mrefu.
Kuchelewa kufika kileleni kwa kadri anavyotaka (premature ejaculations).
Uwezo wa kuthibiti mkojo.
Uwezo wa kusuma sperms umbali zaidi
[/h]
 
Wapo wanawake akishazaa watoto wawili au watatu uke wake hulegea na kupelekea kutofurahia tendo la ndoa.
Hasa kama hakuwa mtu wa mazoezi tatizo linaweza kuwa kubwa, hata hivyo kufanya mazoezi ya Kegel ndiyo jibu kamili ya kurudisha uke kwenye mstari na kuanza kufurahia tendo la ndoa.

Mara nyingi wanawake huwacheka sana wanaume ambao visamaki vyao ni vidogo sana kwa kuwatania kwamba hata ukikohoa tu wakati wapo sita kwa sita kanachomoka, wakati huohuo wanaume nao huwacheka wanawake ambao huko chini kwenye machimbo ya dhahabu kuna pwaya mno kiasi kwamba mwanaume akiingiza mpini hasikii kitu chochote yaani hakuna ule mgusano au msuguano unaoleta raha ya tendo la ndoa.
Wengine wanaita ana uke kopo la kimbo.
Pia kuna wanawake uke umejaa maji kwelikweli hata uume ukiwa ndani ni kuteleza tu bila msuguano wowote wala kubana kokote matokeo yake hakuna ladha na utamu wa tendo lenyewe.

Dawa ipo tena bure na ipo ndani ya uwezo wako, kitu cha msingi ni kukubali mabadiliko na kuwa na hamu ya kutaka kubadilika.
Kuwe na uke tight unaokupa raha wewe na mume wako na zaidi afya yako ya uzazi kuwa imara.
Hata kwa wanaume zoezi hili ni simple wala halina gharama.

Ni kawaida wanaume wengi kuogopa kwenda kwa daktari kuongea masuala ya afya ya uzazi, hapa huhitaji kwenda kwa daktari, ni wewe mwenyewe kuwa serious kwani ukifanya vizuri utakuwa na uwezo wa kusimamisha mti wako kwa muda mrefu na pia unaweza kuhimili kubana kutofika kileleni mapema kabla ya mwandani wako.

Wanawake wengi baada ya kuzaa zaidi ya mara moja na kama hawakuwa watu wa mazoezi misuli ya uke hulegea na kupelekea kupoteza mnato na u-tight wa uke na pia kutojiamini wakati wa kufanya mapenzi kutokana na kupwaya kwa uke.
Kitaalamu hili zoezi huweza kurudisha hiyo hali ya kuwa tight baada ya miezi miwili kwa kufanya kila siku mfululizo na kwa kujitoa na kuwa serious.

Je, hili zoezi ni gumu?
Si gumu
Ni rahisi sana
Ni salama
Siyo zito na halichoshi
Linaweza kukupa matokeo baada ya wiki nane

Je, unaanzaje au nitajuaje huu ndo msuli wenyewe?
Kwanza ili kufanya hili zoezi anza kwa kutambua misuli ya uke au uume inayohusika kwa kuzuia mkojo unapotoka, then kojoa kwa kukata huku ukikaza misuli kwa kutoa mkojo kwa kuhesabu sekunde 4 hadi 10 au namba 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10 the unakojoa tena ujazo wa kijiko cha chai then unaanza upya kwa kukata na kuhesabu 1 – 10 kila unapoenda kukojoa muda wowote.

Hii inasaidia kutambua msuli unaohusika na kukaza uke au uume.
Msuli uliotumia kuzuia mkojo ni rahisi kuuhisi ndo huo unahusika.
Hii misuli husaidia kukaza matundu matatu huko chini kwa mwanamke ambayo ni uke, tundu la mkojo na tundu la kutolea haja kubwa.
Ndiyo maana watu wanaofanya upuuzi ule wa sodoma na gomora kuna wakati huhitaji kuvalishwa nepi maana misuli imelegea hauwezi kuzuia tena haja kubwa.

Ukishapatia kujua msuli upi unamtumia kuzuia mkojo, basi unaweza kuendelea na zoezi hata kama hukojoi au kutoa haja kubwa kwa kuendelea kukaza kama vile unakojoa au unatoa haja kubwa ingawa siyo.
Unaweza kurudia zoezi muda wowote hata kama hukojoi mahali popote, kwenye kiti ofisini, kwenye daladala nk.
Wakati unafanya Hakikisha kuna tofauti ya sekunde tatu hadi kumi.
Pia unaweza kuongeza kukaza hiyo misuli kila ukikojoa fanya zaidi ya 20 kwa siku
Fanya kwa wiki nane mfululizo.

Kumbuka!
Kama wewe ni mwanamke ambaye chini kunapwaya au mume wake amekuwa analalamika kwamba hapati ladha na utamu halisi basi hili zoezi la kubana misuli litakuwezesha kubana uume au kuuvuta kwa ndani, au kwa kuukamua hatimaye anapata raha kwa msuguano unaokuwepo na wewe kufika kileleni haraka.
Ukitaka kujua uke wako unakubali zoezi jaribu kuingiza kidole wakati unafanya hili zoezi then utahisi kidole kubana zaidi kuliko kawaida.


 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom