Je, kuna uhusiano kati Plag na ulaji wa mafuta?

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,256
2,000
Ni upi uhusiano wa plug na ulaji wa mafuta katika gari? Pia Ni muda gani unapaswa kubadili plag.
Simple.
Mfano: Plugs zikiwa vizuri(zinachoma vizuri) ukikanyaga mafuta rpm 2000 unapata 100kph. Gari hio hio plugs zikiwa mbovu unajikuta unakanyaga mafuta hadi rpm 2500 kupata 100kph kwahio hapo unatumia mafuta mengi.

NB: rpm na speed hizo ni mifano tu.
 
JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
1,372
2,000
Ni upi uhusiano wa plug na ulaji wa mafuta katika gari?

Pia ni muda gani unapaswa kubadili plag.

Imbalance yoyote kwenye engine inaweza kupelekea gari kula mafuta.

Nikisema imbalance nazungumzia kitu chochote ambacho kitapelekea engine yako kuzalisha nguvu kidogo kuliko ile iliyokusudiwa.

Engine ina mechanism moja tu ya kucompesate nguvu iliyopungua. Ambapo ni kuongeza kiasi cha mafuta kinachotakiwa kuunguzwa kwa kuziacha nozzle wazi kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida.

Plug zikichoka zinapelekea mafuta yasiungue vizuri na hivyo gari kukosa nguvu. Compesation lazima mafuta zaidi yachomwe ili kufidia.

Nadhani nimeeleweka.
 
BONTABOY

Member
Nov 20, 2015
40
125

Naomba kujua ni plug aina gani sahihi kwa Toyota Rav4 old model cc1990 kwa kuwa kuna zinazotumia pin nyembamba na hizi tulizozizoea za kawaida
 
JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
1,372
2,000
Naomba kujua ni plug aina gani sahihi kwa Toyota Rav4 old model cc1990 kwa kuwa kuna zinazotumia pin nyembamba na hizi tulizozizoea za kawaida

Plug za sindano ni special kwa ajili ya performance engines. Una engine V6, V8 weka sindano pia engine zenye turbo.

Engine za kawaida zinafunga plug za kawaida. Huo ndio uhalisia.

3s fe inafunga Denso PK20TR11
 
LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,126
2,000
Plugs zinabadilishwa kwa km, zipo plugs zinaenda hadi km30,000. Pia unaweza kukagua physically ukaona zishaanza kurusha Moto pembeni(duh lugha za mafundi hizi), au unakuta ile tip imejaa uchafu etc
lkn tip kujaa uchafu au plug kujaa uchafu husababishwa na vitu vingi..plug zinaweza zikawa mpya au mda wakubadilishwa haujafika lkn ukaziona zimechoka kwa mfano air clener ikiwa chafu..valve seal zikiwa majanga kwa namna yoyote ile oil ikawa inaingia kwenye chember
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
41,755

Oil kuingia kwenye chamber zilipo plug ndio kunaua plug pre-maturely hili tatizo na deal nalo mara kwa mara! Sababu ya top cover gasket kufeli! Hivyo kila nikibadili plugs lazma nihakikishe top cover gasket iko sawa!
 
Lee

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
38,967
2,000
Oil kuingia kwenye chamber zilipo plug ndio kunaua plug pre-maturely hili tatizo na deal nalo mara kwa mara! Sababu ya top cover gasket kufeli! Hivyo kila nikibadili plugs lazma nihakikishe top cover gasket iko sawa!
mkuu kuuliza sio ujinga , hivi impreza dashboard yake eti haineshi temperature ... ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom