Je kuna maprofesa na madokta (PhD) jeshini??

barafuyamoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
32,405
Reaction score
29,811
Habari.
Nilitaka kujua maana sijawahi waona wala kusikia hawa 'wasomi' ktk nyanja ya jeshi eidha jwtz au polisi au jeshi lolote!
 
Wapo wakutosha Dr mkuu wa jeshi kipindi cha mgomo wa ma Dr Muhimbili alikuwa anaitwa Dr,Prof,Brigadier general? ???? Namuhifadhi kwa wasiojulikana taaluma zote zilizo uraiani pia ziko jeshini.Kudhibitisha hili wakati waongoza ndege waligoma hawa jamaa kitengo cha anga walikwenda kushika usukani.Vyeo vyao ambavo ndio maarufu vinafunika vyeo vyao vya kisomi hawa jamaa hawana majivuno.Jeshi la Marekani tafiti za mambo ya tiba na anga zinafanyikia kwao. Enzi za Nyerere marubani wa ATC japo walikuwa wanaonekana raia lakini walikuwa wanajeshi.Hivi unajua mkuu wa jeshi la magereza ni mwanamke na ana phD?
 
Wapo ila wachache kuwalipa inahitaji uwe nao wachache uweze kuafford mshahara yao
 
Habari.
Nilitaka kujua maana sijawahi waona wala kusikia hawa 'wasomi' ktk nyanja ya jeshi eidha jwtz au polisi au jeshi lolote!

Kuna mmoja tena ni best ' Neurologist ' akiwa amesomea nchini Urusi na amehudumu sana hapo Lugalo Hospital anaitwa Professor Yardon Kohi amestaafu akiwa na Cheo cha Major General anaishi Mbezi Beach barabara ya zamani ya kwenda Goba. Tena asikudanganye Mtu huko Jeshini ndiyo kuna ' Wasomi ' waliotukuka hadi balaa.
 
Rekebisha hapo kuhusu mkuu wa jeshi la magereza.
Sio mwanamke, ni mwanaume mwenye taaluma ya udaktari (MD).

Uhamiaji ndo kuna mwanamke.
 
Sio rasmi, utafiti wangu umekuwa ni wa kutumia masikio zaidi.
Jaribu kuwatafuta waliopo karibu na wakuu wa hizi idara, watakumegea ukweli. Naimani utapata jibu lililo sahihi, naimani pia hapa kuna wadau watafunguka kwa majibu ya kweli, japo kunawengine watayapamba majibu yao ya uongo.
 
Wako wapi mapoti? Wakuje na majibu hapa + mfano (nasubiria kusikia prof toka CCP). Mkiwataja naomba na mm mni quote
 
Hapana, sikujua wa magereza kama ni dr!! Mmenifumbua macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…