Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,803
- 71,229
Kwanini mambo mengi sasa hivi ni mabovu au magumu namna hii?
Umeme hakuna, maji sehemu nyingi ni mateso. Ukienda Bank no foreign currency, mtaani pesa hakuna, mahospitalini hali ni mbaya tofauti na mtangulizi wake na ajira kwa vijana ndio zinazidi kupotea.
Lakini ajabu ni kuwa HAKUNA anayeweza kumuambia #1 umeshindwa ungetupisha sasa inatosha bali limejaa kundi la viongozi na wananchi wanaosema "anaupiga mwingi" huku wakimpigia chapuo uchaguzi ujao!
Kazi hiyo ya kusema AMESHINDWA tumewaachia viongozi wachache wa upinzani tena huku tukiwabeza kuwa "wanapinga kila kitu" utadhani sisi hatuishi ndani ya taabu hizi?
Je, kumshauri au kumwambia mkuu umechoka na mambo yamekushinda ni kosa la jinai? Mbona hawamwambii bali wana mpaka mafuta kwa mgongo wa chupa?
Tumsaidie kumkumbusha kwa heshima kuu, kuwa hatukumchagua awe #1 bali msaidizi wa Magu na aliweza, sasa hiki anaita "kitabu" ndio kimempa nafasi hii ambayo imemzidi kimo.