Hivi kweli kumuona Nabii Mussa wa Kimara ni Tsh. 100,000/=?

Leo umeandika vyenye ukweli mtupu

Kila mtu akisimama kwenye nafasi yake kwenye jamii haya malalamiko yataisha

Na huko makanisani au misikitini wataenda watu kama familia sio baba huku, watoto kule, mke huku mume kule
Mama D sijawahi andika uongo au utumbo if not making revenge when I am abused! Cheki posts plus thread zangu. Leo umenibana kisawasawa
 
Huyu anajiita kuhani Musa na sio nabii musa kanisa lake ni la gharama sana, kahamia toka pale mwenge mpakani ndipo kanisa lake lilipokuwa mwanzo, ana waumini wengi mnooo na hilo eneo lake kalinunua mwaka jana kama sikosei kwa cash zaidi ya pesa za kitanzania milioni 700. Ila ndi hivyo kumuona gharama sana kwa mtu wa kipato cha chini ni mtihami..yupo katikati ya temboni na kwa msuguri
ukishamuona whats next?
 
Umemaliza kila kitu!

Wanaume mnaolalamika wake zenu kwenda makanisani msikoenda nyie jiongezeni, fanyeni wajibu wenu, wapendeni na kuwatunza wake zenu, simameni kwenye nafasi aliyowapa Mungu, nafasi yenu ya asili, nafasi yenu kwa desturi muone kama kutakua na shida.

Mnavyoacha kufanya majukumu yenu wamama wanawakosa kwasababu nafasi zenu zinapwaya kwenye maisha yao. Tena mshukuru hao wanaoenda kuwaombea kwa makanisa na misikiti;
Wengine wanaenda kutafuta msaada kwa wanaume wanaoweza kuwapa wanachokikosa kwenu, na wengine wanafika mbali zaidi kwenda kutafuta msaada kwa waganga ili mbadilike tuu na huko wanayokutana nayo ni mabaya zaidi

Mungu awasaidie na Mungu atusaidie
tatizo hampendeki
 
Tunaishi kwenye nyakati ngumu sana..... nyakati hizi ngumu zilizojaa mabalaa,vita na mateso ya kila aina imefanya mioyo ya wanadamu kuchoka na kukata tamaa kila iitwapo Leo.....

Mioyo ya wanadamu imesinyaa na inahitaji pumziko na faraja na hapo ndipo unapozaliwa mwanya wa watu wanaojiita mitume kupenyeza ajenda zao na kunufaika na mazingira hayo.........

Mahubiri yao yamejaa matumaini na kutiwa moyo na kuisubiria kesho njema isiyofika Hali ya kuwa wao wanaiishi leo kimatendo na kimaneno........

Hizi ndio nyakati ambazo mwanadamu anatakiwa matumizi yake ya akili yawe juu kuliko hisia.........kwani nyakati hizi zinapoishia fikra zako katika kutafakari ndio unapoanzia mtaji wa watu kutafakari kwa niaba yako kwa faida yao.......
Shida

Binadamu ni wavivu kusoma na kutafiti kuhusu Mungu na maandiko yake. Vile ambavyo mtu anasoma kemia mpaka kuwa mkemia na kutengeneza kilevi (mfano) ama mtu anavyosoma Biology mpaka anasoma masomo ya juu na kuwa Daktari, ndivyo maandiko yalivyo.

Kwamba ukiyasoma Kwa utulivu unapata maarifa makubwa ya kiroho ambayo Mungu amekusudia uyajue.

Shida yetu hatusomi, hatutafiti bali tunataka suluhisho toka Kwa Mungu.

Nionavyo, manabii wa Ukweli na manabii wa Uongo wote wanaishi hii Dunia. Tutie bidii binafsi kutafuta ukweli.
 
Wakuu habari,

Kuna rafiki yangu alikuwa ana shida, ananiambia ameenda kwa Kuhani Mussa huko Kimara ili aombewe.

Basi kufika hapo anaambiwa kumuona huyo mtume Ni Tsh. Laki moja (100,000/=)

Aisee Hawa manabii ni matapeli wakubwa
Wanatoa na risiti za kielectronic au ndo basi u aombewa tu
 
Kuna ndugu yangu alilipa laki moja tangu mwezi wa saba na hajaambulia kumuona, kila akienda wasaidizi wa huyo tapeli wananmwambia kwamba nabii yupo bize sana mpaka mwakani

Anaamini nabii ndio atatatua matatizo yake
 
Kulazisha kiaje?
kumlazimisha mtu kuingia kwenye Uislamu bali untkiwa umlinganie tu
20211116_102026.jpg
 
Tunaishi kwenye nyakati ngumu sana..... nyakati hizi ngumu zilizojaa mabalaa,vita na mateso ya kila aina imefanya mioyo ya wanadamu kuchoka na kukata tamaa kila iitwapo Leo.....

Mioyo ya wanadamu imesinyaa na inahitaji pumziko na faraja na hapo ndipo unapozaliwa mwanya wa watu wanaojiita mitume kupenyeza ajenda zao na kunufaika na mazingira hayo.........

Mahubiri yao yamejaa matumaini na kutiwa moyo na kuisubiria kesho njema isiyofika Hali ya kuwa wao wanaiishi leo kimatendo na kimaneno........

Hizi ndio nyakati ambazo mwanadamu anatakiwa matumizi yake ya akili yawe juu kuliko hisia.........kwani nyakati hizi zinapoishia fikra zako katika kutafakari ndio unapoanzia mtaji wa watu kutafakari kwa niaba yako kwa faida yao.......
Well said mkuu
 
Back
Top Bottom