EEX
JF-Expert Member
- Oct 19, 2014
- 4,404
- 14,268
Leo saa kumi za jioni nikiwa katika mazungumzo ya kawaida na babu yangu ambaye ni kama rafiki yangu ulizuka ubishani, yeye anaamini maisha ni bahati,mimi nikiamini kufanya kazi kwa bidii na kujituma ndio siri ya mafanikio.
Alikuwa akiongozwa na madai yafuatayo:
(1)Hakusomeshwa na wazee wake na hata ndugu waliokuwa na uwezo hawakutaka kabisa kumsomesha licha ya akili nyingi alizokuwa nazo wenzake sasa hivi ni maafisa katika wizara na mashirika hakuwa na bahati yakupata elimu.
(2)Akaamua kufanya biashara ya kuuza ndizi mbivu,anadai yeye ndio alikuwa kijana wa kwanza kwanza kuwa na meza sokoni.Biashara ilipochanganya akachukua mkopo,akanunua mikungu mingi zaidi,akavundika,siku ndizi tu zimeiva bwana Afya akatangaza marufuku ya kuuza matunda kwani kulikuwa na tishio la kipindupindu.
(3)Akaamua kwenda Dar es salaam kubangaiza anadai watu wengi walipita kwenye mikono yake na kufanikiwa,deal kubwa aliopata akiwa huko ilikuwa ni kutoa mzigo kutoka bandarini ambao haukuwa na mwenyewe 1994 vita ya wenyewe kwa wenyewe Rwanda na Burundi.Tajiri aliempa deal hiyo alimuahidi nyumba na pesa.Alifanikisha kutoa mzigo kwa kufoji,siku ya kukabidhiana pesa na nyumba akajikuta mikononi mwa polisi,tajiri alimzunguka,(anaiita bahati mbaya)
(3)Akaanza kusupply stationary katika wizara mbalimbali,hii deal alikuwa anaifanya chini ya jina la kampuni ya jamaa aliotoka nao mkoani,walikua wanafanya kwa mkopo,alipoingia madarakani uncle Ben,akastopisha biashara hiyo na mpaka leo hawajalipwa.
(4)Akaamua aende Ulaya,akiwa na wenzake watatu kama wakimbizi,wenzake wakafanikiwa na sasa wamesoma huko wana kazi za uhakika,wamebaki kumtumia nguo na viatu mtaji hawotoi.
(5)Akarudi nyumbani kulima,huku akizingatia ushauri wa wataalamu huku akihimiza maendeleo kijijini kwetu.Wanakijiji walienda kumshitaki kwa mkuu wa wilaya kuwa ni mpinzani na anataka kugombea udiwani.Wanakijiji wanahujumu mazao yake na anapokea vitisho vya kuchomewa kibanda anachoishi,kakimbia siku nyingi mnoo hii nayo anaiita bahati mbaya.
(6)Kila mpango wowote ambao yeye akihusishwa anadai lazima uvurugike,au watu wavurugane na haufanikiwi kama ulivyopangwa.
Ana mengi ya kuthibitisha madai yake ambayo nimeshindwa kuyaandika.Je ni kweli kufanikiwa katika maisha kunategemea bahati wanajamvi.