Je ku root simu Yako Kuna madhara yoyote?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Android ni mmoja wapo wa mfumo maarufu wa Uendeshaji wa simu unaotumika sana ambao umetengenezwa na Google.

Simu nyingi unazoziona Leo pamoja na kompyuta unazoziona sehemu mbalimbali zimetokana mfumo wa Uendeshaji wa android mbali na iphone ambao wao utumia mfumo wa Uendeshaji wa Apple wa iOS.

Android rooting ni nini?
Unajua kitu kizuri ukisikia kuhusu android ni kuwa Inamruhusu mtumiaji kuweza kuiboresha simu yake atakavyo lakini Kuna baadhi ya vipengele vimezuiwa kwenye Android kutokana na sababu za usalama na faragha.

Ila unaweza kuivunja hiyo Sheria kwa kutumia njia ya root simu Yako kwaiyo rooting maana yake ni mchakato unaofungua mfumo wa Android kukupa uwezo kamili na kumfanya mtumiaji Hawe na haki za juu za msimamizi ili uweze kuiweka simu Yako vile utakavyo.

Ngoja nikueleze kwa mfano unajua simu nyingi za android Huwa aziruhusu mtu kurekodi mawasiliano Yako wakati unaongea kwa sababu ya sheria na kanuni za faragha hivyo ukifanya rooting utakuwa na uwezo wa kufanya chochote.

Faida za kuroot simu yako?
• ukiweza kuroot simu Yako basi utakua na uwezo wa kufuta app zilizokuja na simu
• utaweza kuinstall app ambazo sio compatible na simu Yako
• unaweza ku custom ROM yako kwa kuweza kuiweka utakavyo Yani changing app icon , kuifanyia mambo mengi wanayokuzuia
• utaweza kuongezea Kasi zaidi ya mara kwanza Yani simu Yako inakua na Kasi

Hasara za kuroot simu Yako
• kuroot kunaweza kuua kabisa simu Yako Kuna baadhi ya Simu ukiroot tu ndo imekwisha.
• unaondoa warranty ya Simu Yako yani
• masuala ya ku update inakua ni ngumu kuipata
• security risk simu Yako inakua ni Rahisi kuingiliwa na virusi pamoja na malware.
• Kuna baadhi ya app azitafanya kazi kabisa kama vile app za masuala ya benki au kulipia kitu

Jinsi ya kuroot Sasa simu Yako
Ikiwa unataka ku root simu Yako unaweza kutumia kompyuta au app kupitia simu Yako
Download app ya king root Kisha Install kwenye simu Yako alafu root simu Yako .

Vipi una mpango wa kuroot simu yako tuachie maoni Yako Sasa ?

Teknolojia ni Yetu Sote
 
Habari ndugu zangu naomba mnipe faida na hasara za kuroot simu na nitumie nini ili niroote simu yangu na nitajuaje kama ipo rooted
 
Niliwahi root simu, sikuona hasara, faida niliweza futa apps za kujia na niliweza kutumia fonts zilizokuwa zimezuiliwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom