Je, kitakwimu Kagere alikuwa bora kuliko Mayele?

Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
5,885
13,263
Tuchukue misimu miwili ya Kagere alipojiunga Simba tuache misimu inayofuata ili tumlinganishe na Mayele.

Msimu wa Kwanza Kagere ana magoli 23
Msimu wa pili ana magoli 22.

Mayele msimu wa Kwanza ana magoli 16
Msimu wa pili ana magoli 17.

Hizo ni takwimu kwa ligi ya ndani.

Naomba wenye takwimu za assists zao kwa misimu hiyo atuwekee.

Halafu tuje kimataifa, magoli kwa misimu miwili na assists zao.

Halafu tuone nani bora kwanini mmoja anapambwa sana au style yake ya ushangiaji na siyo takwimu?
 
Sasa ukiitwa mbumbumbu ndiyo umtukane mtu matusi ya nguoni! Mbona Mwenyekiti wenu mstaafu alipowaita mbumbumbu kwenye ule mkutano wenu, hamkumtukana?
Hata wewe ukiweka uzi mtu akuite nyani kama Lucy alivyosema lazima utareact.

Turudi kwenye takwimu kujenga hoja
 
Kagere alifunga hayo magoli yote kipindi kile ligi ina timu 20. Kagere alifunga hayo magoli kipindi mshindi wa ligi anakula mil 80 sio sasa ambapo kila timu kwenye ligi inapata mgao wa haki za matangazo.

Yani kiufupi kipundi hiko kulikua na ukata sana
Tutapataje dk walizochoza, maana hata kama timu ni 20 mechi zinaweza kuwa chache kuliko Mayele ,Mayele kila mechi alikuwepo, nadhani hata haizidi mechi nne ambazo hakwepo kwa misimu miwili aliyocheza
 
Pyramid wametoa bil 3 kumchukua mayele. Kagere yupo singida united.
Hata Pogba alinunuliwa dau kubwa kutoka Juventus na Man U lakini alipofika Man U hakuwa na maajabu, kuna wachezaji wana mawakala wazuri na wananunuliwa kwa hela ndefu lakini kitakwimu wanazidiwa, Ronaldo kwenda Al Nasri siyo kwamba ni bora kuliko wengine
 
Hata wewe ukiweka uzi mtu akuite nyani kama Lucy alivyosema lazima utareact.

Turudi kwenye takwimu kujenga hoja
Kureact kupo. Ila tusitukanane bhana matusi ya nguoni. Maana matusi ya nguoni yanaondoa ile dhana ya utani wa jadi.
 
Tutapataje dk walizochoza , maana hata kama timu ni 20 mechi zinaweza kuwa chache kuliko Mayele ,Mayele kila mechi alikuwepo,nadhani hata haizidi mechi nne ambazo hakwepo kwa misimu miwili aliyocheza
Mzee unaongea kishabiki kumbe, unatak kusema katika mechi 72 za misimu 2 mayele hajacheza mech 4 tu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom