Je, Kila ulichokinunua ulikihitaji kweli au ni tamaa ya kumiliki kitu?

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
JE KILA ULICHOKINUNUA / KUNUNUA UNAKIHITAJI KWELI AU NI TAMAA TU YA KUMILIKI KITU?

Tunaishi kwenye dunia ambayo tunasukumwa sana kuwa wanunuaji, wateja.

Tunalazimika kununua vitu vingi ambavyo hata hatuna matumizi navyo, na kama tunayo basi sio muhimu sana. Tunalazimika kununua kwa sababu tu tunaogopa tusipitwe. Na hapa ndipo utumwa mkubwa wa dunia unapoanzia.

Sio vibaya kununua, ila kununua kwa msukumo ni utumwa mkubwa zaidi.
Na hapa ndipo matatizo mengi ya kifedha ya watu wengi yanapoanzia.
Pale wanaponunua vitu ambavyo hawana mahitaji navyo makubwa.

Matangazo mengi ya vitu yanakupa msukumo kwamba kinapita, na usiponunua sasa basi unapitwa, au utaonekana mshamba kwa sababu wajanja wote wanacho kitu hiko. Na wewe unalazimika kununua ili uwe sehemu ya wajanja hao.

Ni muhimu uelewe kwamba kufanikiwa kwenye dunia ya sasa unahitaji uweze kusimama mwenyewe, kufanya vile vitu ambavyo unavipenda wewe hata kama wengine hawafanyi na kuweza kusema hapana hata kama watu wengi wanasema ndio.

Kama utashindwa kusimama mwenyewe, basi utajikuta unapelekwa na kila kitu na kuishia kuwa mteja wa kila siku, kumbuka kama hutaweza kusimama kwa kitu fulani, basi utaanguka kwa kila kitu.

Kwenye dunia ya sasa ambayo inakusukuma uwe mteja wa kila kitu, kama hutakuwa na vipaumbele vyako ambavyo unavisimamia, utaanguka kwa kila kitu na hivyo kuwa mteja wa kila kitu.

Na mbaya zaidi ni kwamba mwanzo unasukumwa kununua vitu, ili uvimiliki, lakini mwishoni vitu hivi ndio vinakumiliki wewe. Na unakosa uhuru wa kuwa na maisha unayoyataka wewe.
 
Kununua kitu usichokitarajia ni Ulimbukeni tu, tangu nimejitegemea katika maisha yangu sijawahi nunua kitu bila kuwa na malengo nacho. Na mara zote nimekuwa wa mwisho kununua kila toleo linalopitwa na wakati na sishangai kufanya vile.
 
Ni kweli nipo na rafiki yangu, hapitwi na kitu anaviatu more than 12 peya za viatu, Sendo ananunua zile za kachina, yeye anakuwa happy kusikia Fulani amejenga nyumba AU Fulani amenunua shamba.
 
ukweli ni kwamba vitu vingi tunanunua kwa ushindani usiokuwa na msingi, mfano hai tafakari una pea ngapi za viatu, zinaweza kufika kumi, lakini unazozivaaa ni zile zile tatu tu, zilizobaki kutia wingi.
 
Kule kanda ya ziwa watu wanakuroga ununue bidhaa hata kama huitaji! ukifika home unajuta kwa nini umenunua....tusilaumu haya ni maujuzi tu.......
 
Back
Top Bottom