Je kampuni zilizimishwe kukua ?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je kampuni zilizimishwe kukua ??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Jan 20, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Wakati kampuni ya Tigo ilivyobadilishwa Jina toka mobilel Nilikuwa na shauku moja nayo ni kuja kuona kwamba sasa kampuni hiyo inakuwa zaidi kwa Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla kwa sababu ndio moja ya kampuni kongwe kabisa ya simu za mkono hapa Tanzania .

  Fikiria ina miaka zaidi ya 10 katika soko la Tanzania kwanini haijipanui kama Zain ambayo ilikuwa ni Celtel zamani au Vodacom ? kwanini kila siku tunaona matangazo tu katika magazeti radio tv zetu na barabarani bila kuona kampuni kama hii inajipanua zaidi katika sekta hii ya mawasiliano kuajiri watanzania wengi zaidi ?

  Mimi nafikiri hili ni kosa watu wanavyokuja kuwekeza nchi wapewe masharti ya kukuza biashara zao ili waajiri watanzania wengi zaidi katika biashara hizo bila hivyo kampuni hizi ziondolewe nchini kabisa hatuhitaji kampuni kama hizi zilizokuwa katika masoko zaidi ya miaka 10 na hatuoni watu wakiajiriwa kwa wingi wala kampuni hizi kujitanua nchi jirani .

  Afrika mashariki sasa inakuwa sana tunaona kampuni za nchi jirani zinavyokuja kuwekeza kwetu , kuchukuwa ajira zetu na kufanya wanachotaka kwanini zetu hazifiki huko nini kinachoendelea

  Sijui sera ya uwekezaji inasemaje kuhusu wawekezaji wanavyo kaa nchini kwa kipindi kirefu bila kupanua kampuni na biashara zao ili kuajiri watanzania wengi zaidi serikali ipate mapato mengi zaidi iweze kujiendesha

  Kama kampuni hizi zitakwepo mpaka 2015 uongozi ukibadilika itabidi zifungwe na kupewa watu wengine waweze kufanya kazi kujipanua na kuajiri watu wengi zaidi
   
Loading...