Siku za mapumziko za kitaifa (za dini na za kiserikali). Siku za mapumziko kwa kwawaida hutangazwa na serikali (kwa kawaida zipo siku za mapumziko 17 kwa mwaka). Siku za mapumziko zina ongozwa na sharia ya Siku za mapumziko ya mwaka 1966. Siku hizi ni Mwaka mpya (1 Januari), Mapinduzi ya Zanzibar (12 Januari), Maulidi, Ijumaa kuu (19 Machi), Jumapili ya Pasaka, Jumatatu ya Pasaka, Kumbu kumbu ya Sheikh Abeid Amani Karume ( Aprili 07), Muungano (Aprili 26), Siku ya wafanyakazi (Mei 01), Saba saba (Julai 07), Nane nane (Augusti 08), Eid-el-Fitri( siku 2 ), Siku ya kumbu kumbu ya Mwalimu Nyerere (Oktoba 14), Idd-El-Hajj , Uhuru wa Tanzania (Desemba 09), Krismasi (Desemba 25), Boxing Day (Desemba 26). Sikukuu za kiislamu zinategemea sana mwandamo wa mwezi.