Je, Joseph Mbilinyi (Sugu) anaweza kufungwa?

Je, Joseph Mbilinyi (Sugu) anaweza kufungwa?

Lema unakosea kusema hujui cha kufanya!
Tujaribu kuangalia watu wengine kwenye nchi nyingine walifanya nini katika wakati kama huu!
Hatuwezi kukosa model ya kutufaa kutumia.

Mimi najua kwenye roho yangu, Bila ujasiri wa kuwa tayari kuuza roho wakati wowote, hii hali haitabadilika.
Binafsi niko tayari wakati wote, na ninaamini siko peke yangu.

Uwezo wenu viongozi wa kuongoza na kupangilia matukio ndio unaohitajika zaidi!
Tukiendelea kulia tutafilisiwa, kuwekwa jela, kupigwa risasi mmoja mmoja mpaka tuishe au kupotezwa kama Ben!
Watakaobaki wataingiwa na hofu na watakimbilia CCM bila hata ya kupewa hela kwaajili ya usalama wao na familia zao.
 
walau siku hizi akili imekurudi baada ya kusota rumande, ngoja na mbunge mwenzako sugu asote kdg labda atapata akili. mdee tayari usawa wa kati.
mnafaidika nini mkishawaweka ndani, nini zaidi mnachopata, mngekuwa mnawaweka ndani kisha nyie mnaneemeka ningesema hapo ni kweli, lakini hakuna lolote, mnajidanganya tu wapinzani ni wananchi na sio hao uliowataja
 
Wananchi ndiyo waajiri wa Raisi na si vinginevyo. Busara lazima itumike, waliopigia kura upinzani ni watu zaidi ya milioni 6, hao watu wakiingia mabarabarani wakaanza fujo hiyo mipango ya Raisi itafanikiwa? Lazima busara itumike kuleta maelewano.
unajua hawa ndugu kinachowapa kichwa ni risasi tu, bila risasi hawa ni wepesi sana, manake kitu kidogo ishatangulizwa risasi
 
Tabia hii ya uoga isipo koma nafikiri hata ikatokea Chadema kuongoza Nchi hakutakuwa na tofauti kubwa sana kati yetu na ccm kwani mlinzi wa Nchi bora sio sera na rangi ya Chama cha Siasa bali ni tabia na fikra za wanaotawaliwa (Attitude ) dhidi ya Nchi yao .

Kuishinda hofu sio tu ni faida katika Nchi bali ni msingi mzuri wa kujenga kizazi cha ubunifu sehemu mbali mbali za maisha yao ya kila siku. Hofu haiwezi kujenga uwezo ubunifu (innovations) kwa sababu hofu ni ugonjwa mbaya sana wa akili.

Kabla ya kusema kwamba Bunge letu haliko huru ni muhimu kujiuliza kama hao Wabunge wenyewe wanajua thamani ya uhuru ? Na wako huru ?

Leo umenigusa! Ugonjwa wetu kila mahali ,eti watumishi hewa,eti mikataba hewa nk. Jamii nzima ndiyo ilioza. Hivyo bila kubadili jamii basi hata uwe na akina Nyerere 50 kupiga maendeleo ni kazi.

Ili mradi Mhe.Umeligundua hilo. Somo hili iwe sehemu ya Sera ya CDM kwa ila ofisi zake na hasa zile za mtaani. Tafuteni mpango Kazi wa kufanikisha hili.
(Elimu kwa Raia)
 
Kama kweli CDM ni waungwana ni vyema kwanza wangekemea viongozi wao kuporomosha matusi makali bila ya sababu za msingi, inafaa ile clip ya Sugu iwekwe pia humu ili tuone jinsi tulivyo na viongozi wa ajabu. Kama mbunge unaongea matusi, kejeli na uongo na unatetea huo ndio uhuru basi hamna faida yoyote kwa jamii. Uhuru usio na mipaka ni vurugu.

Hakuna hata Kiongozi mmoja wa CDM atakayekemea ujinga aliofanya Sugu, hii inachochea viongozi wengine wa mizuka wa CDM kuja kufanya makosa hayo hayo. Kama wakati ule Lijuakali anawafanyia fujo Polisi hadi kufungwa ingekemewa Sugu asingefikiria kufanya ujinga na yeye. Endeleeni kutetea ujinga ila hakuna mwananchi atakaye ingia barabarani ili kutetea uovu wa Sugu.
 
Majimbo yote yenye wabunge "Wasumbufu" na ambao maeneo yao yanaongozwa na vyama mbadala lazima yapite katika "Tanuri la Moto".

Ni lazima kuwaadabisha viongozi ili wafuasi wao warudi nyuma,ukiisikiliza "Audio" ya Sugu,haina tofauti kimantiki na kimaudhui na kauli za Rais alizozitoa wakati akisema "Watoto vilaza",hazina tofauti na kauli za kuwaita Mawaziri wake "Wapumbafu",wala hazina tofauti na zile kauli zilizotolewa wakati wa tetemeko kule Bukoba.

Kesi ya Sugu,ni kama ile ya Lijualikali na Suzan Kiwanga,ni tabia za ujasusi wa Kirusi enzi za USSR,mnaenda kuchoma moto ofis ya kijiji,wakati mnapokuwa mmedhurumu ushindi wa udiwani,ni dhahiri watakaoonekana wamechoma ni wale waliolia kupokwa ushindi.

Pale Iringa Mjini,Msigwa na vijana karibu 20(wako ndani mpaka sasa) wameuziwa kesi ya kuchoma nyumba ya kada wa zamani wa CHADEMA,na kiongozi wa CCM...Nyumba hizi zinachomwa wakati kukiwa na huzuni ndani ya Chadema kwa kuhamwa na viongozi wake Iringa Mjini,lengo ni kutengeneza picha kuwa CHADEMA ndio waliochoma.Haya mambo yooote anaratibu Kasesera na watu wake,ili kuuwa upinzani Iringa mjini.

Kosa la Sugu,ni kuibeba ile kata iliyokuwa na Uchaguzi mdogo,lazima alipe malipo ya ushindi ule.Hivi ni vitu ambavyo hata ukiwa ndani ya CCM na unapenda siasa nzuri tu ya ushindani huwezi kuviunga mkono,ni bahati mbaya wanaopanga haya yote ni watu tunaowaheshimu hadharani na faraghani.

Maendeleo sio majumba,barabara na madaraja,ni pamoja na UPENDO NA AMANI katika jamii ya watu unawongoza.Huwezi kujivunia maendeleo kama uhuru binafsi na wa vikundi unabakwa.Chuki inayojengwa katikati ya mioyo ya watu,inaweza isionekane leo,ni kama amani na mshikamano tunaojivunia,ulipandwa miaka hiyo ya 1960 na kina Nyerere,lakini mpaka leo tunaifaidi.

Hata Mungu alipata "upinzani",Mitume wa Mungu walipingwa,wewe binadamu mwenye nyama na siku zinazohesabika kwanini usipokee changamoto!??Ni ushamba wa kimadaraka tu....
 
Kitu tulicho kosa watanzania ni Uzalendo na nchi yetu kingine kukosa busara kwa viongonzi wetu wa Serikali pamoja na Upinzani. Siku moja mmoja wapo akijitambua basi mambo yataenda sawa hizi nyingine zilizokuwepo ni porojo tuu za kisiasa.
 
Bayyo,
kwa hiyo unataka kusema Lema ndio alikuwa anaratibu maandamano, wakitaka kuandamana si wanatumia njia zilizowekwa na serikali, wakikataliwa basi, wanaacha, unataka kusema yale mabomu siku ile kanisani ni lema ndio aliratibu, mbona nakumbuka vipande vya mabomu vilienda chekiwa na wakasema vimetengenezwa kutoka china, ni wajeda tu ndio wanayo, hakuna sehemu nyingine, sasa hao unaowaita watukufu kwako walileta mrejesho kuwa nani alilichomoa kwa wajeda na kulirusha kule, mlikuwa mnaruhusu wenyewe mwishowe mnaanza warushia mabomu kwa kumlenga mtu flani mnajikuta mnaangamiza wasio walengwa
 
mnafaidika nini mkishawaweka ndani, nini zaidi mnachopata, mngekuwa mnawaweka ndani kisha nyie mnaneemeka ningesema hapo ni kweli, lakini hakuna lolote, mnajidanganya tu wapinzani ni wananchi na sio hao uliowataja
Kitu kinacho fanyika huwa ni kuwatia adabu tu kwisha habari!
 
Mh. Lema hizi move zote za Hakimu ni kumfunga. There was no need ya kumnyima dhamana. These are calculated moves!

When assessing whether to grant bail, courts must – start with the presumption that an accused should be granted bail, unless there is a justified reason to refuse it.
The court will consider:

  • the nature and seriousness of the crime;
  • the character of the defendant, his/ her past criminal record, associations and ties with the community;
  • the defendant’s previous record of abiding by his/ her bail conditions;
  • the strength of the evidence against the defendant.
Time will tell!

the character of the defendant, his/ her past criminal record, associations and ties with the community;
 
Acheni kulialia kasikilize ile audio ya dakika 39 ikiyowekwa mahakamani live Jana halafu utwambie nani anamuonea nani?,tatizo mlizoea kuchukulia mambo kirahisirahisi awamu zilizopita, zamu hii mambo yamebadilika na msipobadilika mvua zitewanyeshea kweli. Hakuna demokrasia ya kuongea bila break duniani.Demokrasia Ina mipaka yake, JPM alipoingia madarakani alisema "Nimeamua nchi isonge na itasonga tu", na kweli inasonga tu mtakaoamua kuwa walalamishi endeleeni Kama itawasaidia, wengine tunaendelea na Maisha Kama kawaida, wananchi wanataka maendeleo sio porojo za demokrasia, sijui mikutano ya siasa na malalamishi kila siku.
Labda kama maana ya 'reverse' imebadirika na sasa ndiyo inaitwa 'kusonga mbele'.
 
Kuwa na wanasiasa wanaojikita kwenye ajenda uchwara ya demokrasia ni wa kuogopa sana!Sijawahi kusikia Lema akizungumzia kujenga visima, kuhamasisha wananchi wake kujitolea kwa ajili ya maendeleo yao..Muda wote ni kulalamika tu..Hii inaonyesha mtaji wake wa kisiasa au kiki ni mafujo na kutukana serikali kuu.
 
Back
Top Bottom