Je, ifikapo 2020 upinzani utakuwa?

Je, ifikapo 2020 upinzani utakuwa?

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Posts
240
Reaction score
769
IMG-20180216-WA0014.jpg

Hili ni swali linalozunguka miongoni mwa watanzania wengi kutokana na hali ilivyo sasa na wengi wameingia wasiwasi baada ya viashiria vya ukandamizaji juu yao sio kwamba huko nyuma hakukuwai kutokea ukandamizaji la hasha! Ulikuwepo lakini haukuzuia shughuli za siasa kufanyika ila kwasasa kuna zuio la kutofanya siasa mpaka 2020 hiii ni mbaya kwa upinzani lakini tujipe TAFAKURI TUNDUIZI nafasi ya upinzani 2020.
Kwanza vyama mbadala (upinzani )havikuanza 1992 vilikuwepo hata kabla ya uhuru sema tulipopata uhuru mwalimu nyerere alivifuta kwa hiyo 1994 ulikuwa ni urejeshwaji japo ccm haikupenda kwa sababu kilijiunganisha na dola ndo maana kulikuwa na mikoa ya kijeshi ktk majeshi yetu kwa hiyo toka mfumo wa vyama vingi urejee ccm haijawai kuukubali watu wengi waliojiunga na upinzani 1992 walifilisika waliumia wamekuwa vilema na kulikuwa na hujuma ndani vyama upinzani toka kurejea kwake

Ktk hawamu hiii ya tano wamekuja na style ya kuumaliza upinzani kupitia taasisi za kiserikali rejea chaguzi wa kata 43 na majimbo mawili ya siha na KINONDONI wakuu wa mikoa na wilaya
wamekuwa ndo wafanya maamuzi rejea uchaguzi wa KINONDONI mkuu wa mkoa wa DSM na mkuu wa wilaya KINONDONI walikuwa kwenye majumuisho ya kura achana na amri zao kwa vyombo vya usalama.

UPINZANI UFANYE NN?
Ni lazima urudi kwenye uanaharakati kuforce vyombo vya serikali kuwapa hadhi sawa na chama tawala.
Uunganishe nguvu na makundi mengine ktk jamii hasa asasi kiraia
Utumie mfumo wa mahakama kutafuta haki kwa watendaji wanaowavunja sheria ya vyama ya mwaka 1992 na wanaokiuka haki za kibinaadamu



Mwisho 2020 ndo mwaka upinzani kuwa na wabunge wengi wanaweza kuwa nusu na ccm
 
Upinzani hauwezi kufa kamwe, dunia huwa hairudi reverse

Labda wanaweza kuua upinzani ndani ya bunge kwa maana kutumia vyombo vya dola kupora ushindi wa wabunge wa upinzani

Wakiua upinzani ndani ya bunge haina maana huku mtaani haupo, upinzani huku nje uko imara sana kuliko wakati wowote ule

Fikra kinzani ndio tafsiri sahihi ya neno upinzani, hivyo kuua upinzani ni kitu kisichowezekana
 
Ikifika 2020 zaidi ya asilimia 80 ya watanzania watakua wapinzani ila hakutakua na jukwaa la kiuwakilisha wapinzani. Jukwaa kama vile vyama vyenye muonekano wa kipinzani. Ila hapata pita mda mrefu kitazaliwa Chama cha watu, kitakachokua na nguvu kuliko chama chochote kilichowahi kutokea Tanzania. Chama hiki kitaongozwa na watu Si kwaajili ya kushika dora Bali kutetea haki zao. Mda utaongea
 
Back
Top Bottom