Ashampoo burning
JF-Expert Member
- May 12, 2023
- 1,296
- 3,929
Unajua Idi Amin? Watu wake walimuita Big Daddy, lakini maadui wake walimuita mzee wa buchani – “The Butcher”. Yaani huyu jamaa alitokea kule West Nile uganda kaskazini, Uganda, kijiji chenyewe hakijulikani jina, alikulia kwenye familia maskini chokaa balaa. Baba na mama wakatengana, akabaki kulelewaa na mama yake watoto wa mjini wanasema single maza, akiwa mdogo anahangaika kama watoto wengi wa mtaa kula kwa shida saana yaani.
Sasa elimu hakuwa nayo sana, yaani mpaka kijana wa miaka 21 bado hana direction. Ndo akamua kuingia jeshini, King’s African Rifles , jeshi la kikoloni la Waingereza. Wanasema alianza kama mpishi wa makande na supu ,yaani mpishi wa jeshi 😂, lakini jamaaa akapanda cheo fasta hadi kuwa mwanajeshi kamili.private
Akatumwa Somalia 1949 kupiga waasi, akaja Kenya kudhibiti Mau Mau. Lakini issue ikawa moja – Amin hakuwa tu askari, alikuwa na ukali kupita kiasi katili haswa. Watu walikuwa wanamwogopa interrogation zake. Waingereza walitaka kumshitaki, lakini badala yake wakampa cheo kingine! 1959 akawa “Afande” – cheo cha juu kabisa kwa askari mweusi wakati ule.
piai alikuwa bonge la bodybuilder mwili nyumba kipande cha mtu na bondia pia? Akawa bingwa wa ngumi Uganda kwa miaka mingi. Kwa hiyo alikuwa na nguvu, ukali, na sasa cheo kinapanda.
Uganda ikakaribia uhuru. Apo ndipo alipokutana na Apollo Milton Obote – kiongozi wa siasa. Wakaunganisha nguvu. Obote akawa Waziri Mkuu 1962 baada ya uhuru, Amin akapewa nafasi kubwa jeshini. Lakini, Amin alikuwa mtu wa maneno machache na vitendo vibaya. Alipopewa kazi ya kukomesha wizi wa ng’ombe Kaskazini, aliua watu hovyo mpaka Waingereza wakakasirika. Obote hakumfukuza, bali akamtuma Uingereza kwenda kusomea zaidi jeshi. Jamaa akarudi akiwa amekomaa zaidi.
1964 jeshi la Uganda likawa na mgomo, nani akaletwa kutuliza? Amin! Akawekwa Deputy Commander. Lakini bado alikuwa na michezo yake ya magendo – dhahabu, kahawa, na pembe za ndovu kutoka Congo za magendo kauza sana mzee baba iddy. Na Obote mwenyewe alikuwa ndani ya mchezo huu wa kuuza magendo kutoka congo.
1966 Obote akafumua serikali, akajiweka Rais. Akawa anamtegemea Amin kwa ulinzi. Amin sasa akawa Chief of Army and Airforce ***** yaani mkuu wa majeshi. Cheo kikubwa kuliko vyote. Lakini miaka ikasogea, Obote akawa anamshuku. Hasa baada ya jaribio la kumuua 1969. Alipojaribu kumshusha cheo Amin, hakufaulu. Obote kaenda safari Singapore 1971, huku nyuma mzee Amin akapiga coup d’état kiswahili akapindua serikali fasta. Akaweka serikali yake, akajipa majina marefu kama mzaha jina refu na ukikosea kulitamka kesi:
"Rais wa milele, Field Marshal Al-Hajji Dr. Idi Amin VC, DSO, MC, Bwana wa wanyama wa nchi na samaki wa bahari, mshindi wa Waingereza barani Afrika kwa ujumla na Uganda kwa ujumla."
Mara baada ya kuingia madarakani, akawa mkali mbaya. Viongozi wote waliokuwa tishio – Askofu Mkuu, Majaji, Chansela wa Makerere, wote akawamaliza. Jeshi likajaa wapiganaji wa kabila lake na wapiganaji wa zamani wa vita. Ndani ya miezi michache, damu ilikuwa ikimwagika kila upande.