Je, huu ushauri ni sahihi?

Je, huu ushauri ni sahihi?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,637
Dear Aunt,
Naomba msaada wako nifanye nini? Mimi ni mke wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume wangu ana angalia TV. Sikufika mbali gari ghafla likazima, nikalazimika kutembea kwa miguu kurudi nyumbani nikamwambie mume wangu anisaidie. Nilipofika nyumbani sikuamini macho yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa jirani yetu. Nilimkabiri mume wangu na kwa bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao una mwaka sasa, lakini cha ajabu amesema atalazimika kumuacha huyo binti pole pole ili asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado mdogo. Je hii ni sawa? Nifanye nini? Naomba
ushauri Mzee wangu
Fransiska wa Mwenge


JIBU
Binti yangu Fransiska,
Nimesoma kwa makini ujumbe wako, kitu ambacho nimekiona mara moja ni hili tatizo la gari kuzimika ghafla. Kwanini uendeshe gari na baada ya muda mfupi lizime? Hapa kuna matatizo kadha wa kadha ambayo yanaweza kuwa chanzo. Inawezekana plug mbovu au uchafu umeingia kwenye mrija unaopeleka mafuta kwenye engine. Au pengine ni tatizo la umeme, au fuel pump, ulicheki kama petroli ipo? Ikiwezekana waone mafundi warekebishe hivyo nilivyovitaja.
Nategemea ushauri huo utakusaidia mwanangu
 
Safi sana.... kiuhalisia hakuna kosa kwa mwanaume kuchepuka ila kwa heshima tuu inatakiwa mwanamke asijue..
 
japo ya zamani ila inaendelea kuvutia.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom