Je, huu sio uvunjaji wa haki za msingi za binadamu unaofanywa na serikali ya Magufuli?

Ben Saanane,

Heshima yako. Sioni shida kutekeleza sheria zilizopo. Katiba ni mchakato. Hata kama Katiba itakuja na iwe nzuri kama Malaika wa Mbinguni ikikosa Sheria na Kanuni haina maana kabisa.

Aidha, lazima tujue bila kupata mtu wa kusimamia hiyo Katiba na sheria zake, hakuna tutakapofika. Tuamini hata Katiba ikija ataisimamia kama anavyofanya. Tunajua vipengele vingi sana vya katiba iliyopo vinavyokanyagwa tangu enzi za Mwinyi, Mkapa hata JK. Shida ilikuwa nini? Katiba, sheria au viongozi!!!

Hivyo, hatuwezi kusitisha kusimamia sheria zilizopo kwa kigezo cha Katiba. Inakuja, kama haiji tutaidai.
Angekuwa seriou kuwa anataka kubadili nchi angerudisha Rasimu ya Wananchi.Huko kuna maadili na Tunu zote.Maigizo hayajawahi kuwa ya msaada katika kuongoza nchi
 
Wanabodi,

Tanzania ni nchi inayofuata katika na utawala wa sheria!.

Ndani ya katiba ya JMT kuna vifungu rasmi vya haki za msingi za binaadamu!. Moja ya haki hizo ni kipengele hiki

Kama jambo hili ni kweli limefanyika,
Kigogo wa BoT azuiwa Airport kutokana na kukosa vibali vya kusafiri nje ya nchi

then
Haiwezekani mtu ambaye yuko huru, tena yuko likizo, ameamua kwenda kujipumzikia zake nchi za wenzetu, azuiliwe!.

Nafahamu kuna wafanyakazi wa serikali, na baadhi ya idara nyeti, au hata madakitari, jeshi, polisi na zimamoto, hata wakiwa likizo, wanawajibika kumtaarifu mwajiri wao, likizo yake atakuwa wapi, ili in case of anything, aweze kuwa reached out!, lakini kitendo cha maofisa uhamiaji, kumzuia mtu mwingine yoyote wa serikali, asisafiri nje ya nchi, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu!.

Pamoja na nia nzuri, na nia njema ya Rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kudhibiti safari za nje ya nchi zisizo na tija kwa taifa, utekelezaji wa kauli hiyo, lazima uzingatie taratibu, sheria na kanuni, na sio kutekelezwa tuu kama zimamoto, na kukiuka haki za msingi za binadamu!.

Ila pia niliwahi kushauri humu, kama baadhi ya sheria, zinaweza kuwa ni kikwazo kwa rais wetu, kututengeneza Tanzania tunayoitaka, rais anayo mamlaka ya kisheria, kuandika waraka, 'decree' kuiweka kando katiba , hivyo kuitawala Tanzania kwa kutumia decree hivyo kuwa huru kufanya jambo lolote atakavyoona inafaa!.

Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria Ongoza Kwa Kutumia Decree tuu!

Viongozi wote wanakula kiapo cha utii wa katiba!, kama katiba inatoa uhuru fulani!, haiwezekana, akaibuka mtu mwingine, kwa mamlaka aliyopewa na katiba hiyo, akauondoa uhuru fulani na haku tunamtazama tuu, au tunamshangilia!. Hili haliwezekani!.

Japo wengi wetu, tunaishi katika lindi la umasikini, uliotopea, na sio tuu hatuna hata hiyo likizo, lakini umasikini wetu, usutufanye tuwachukie, wenzetu waliobahatika kuwa wenye heri, wenye uwezo wa kwenda kujipumzikia zao ulaya wakati wa likizo zao!.

Nashauri serikali itoe waraka wa ufafanuzi wa hili katazo la safari za nje, unless itamkwe wazi, watumizi wote wa umma, hata safari zao binafsi kujipumzikia, au kuwatembelea wapendwa wao, wapenzi wao au hata vimada wao, sasa lazima waombe kibali kwa KMK!, na jee kama hivi ndivyo katiba ilivyotamka?!, kama sio kwa mujibu wa katiba, then rais atoe waraka, Tanzania tujijue tuko kama China au Urusi, enzi zile, kuingia Beijing au Moscow, mtu hujiingilii hivi hivi!.

Jee kumkumbusha rais wetu kuhakikisha watendaji wake wanazingatia katiba aliyoapa kuilinda, ni kumuingilia katika utendaji wake?!.

Pasco
Mkuu Pasco kwanza unajulikana kama a true believer wa Lowassa, hivyo hutegemewi kuona positivity ya issues unazoziona katika maamuzi ya mzee wa Push Up.

Kwanza jiulize mwenyewe, mtu na familia yake wanaamua kwenda Switzerland au kwingineko ili "kupumzika" sikukuu ya Xms.
Its not a bad idea lakini kwanza piga mahesabu ya income yake inayoweza kuwabeba hao watu, ticketing, hotel costs(pengine wana nyumba abroad, hatujui) na incidentals-and mind you ni familia nzima!!

Pili, kwa agizo la rais, pengine huyo mkuu wa BOT hakuelewa, kwa nini asiombe vibali?
Na viikuwepo zamani, kama ni mfanyakazi wa serikali, hata Tax Clearance certifcates zilitolewa.

Tatu, huyo bosi kweli ana uwezo, lakini nina wasiwasi na wisdom na thinking yake na pengine ndio wakati wa kuondolewa hapo alipo ili akafanye kazi kwenye benki za kawaida. Wengi tunafahamu perks and benefits ambazo zimelalamikiwa sana za wafanyakazi wa benk kuu
Just do not blow it!!
 
Last edited by a moderator:
Kaka Pasco hivi mbona naona wanajamvi wengi hapa wanakuchukulia kama mtu mweledi na makini! Kwanini sasa unaonyesha hali ya kuwa single track minded?!
Nakushauri utafakari falsafa hizi mbili kwa kina kidogo!
1: Desperate situations demand desperate interventions (read solutions); hizi ni hatua za muda tu kutibu kansa ya JK aliyoliambukiza taifa hili.
2: If the state can not serve the many who are poor; for sure it can not protect the few who are rich. Ili kulinda maslahi ya wananchi walio wengi lazima serikali ichukue hatua nzito na ngumu kumeza
3: Uhuru usio na mipaka ni ghasia na karaha! Ukiendekeza uhuru wakati hao wakwasi; wezi, wala rushwa na mafisadi kama tulivyoshuhudia siku za karibuni ambao wao hawakuzitilia maanani haki za kikatiba za wananchi wakati wanakwiba; serikali itakuwa imepoteza uhalali wa kutawala kama hiyo ya JK iliyofuga uozo wa kutisha.

Kweli katika hali tuliyofikia chini ya utawala wa JK kama inavyoendelea kufunuliwa pazia Pasco unadiriki kutetea inconvinience ndogo kama hiyo ambayo bado kigogo husika kashindwa kuwaridhisha maofisa husika kama anakidhi masharti yaliyowekwa!

Hebu declare interest Pasco; are you with us or you are with the enemy; Wezi na mafisadi?!

Pasco stand up and be counted; uko upande gani?!

Wanabodi,

Tanzania ni nchi inayofuata katika na utawala wa sheria!.

Ndani ya katiba ya JMT kuna vifungu rasmi vya haki za msingi za binaadamu!. Moja ya haki hizo ni kipengele hiki

Kama jambo hili ni kweli limefanyika,
[h=1]Kigogo wa BoT azuiwa Airport kutokana na kukosa vibali vya kusafiri nje ya nchi[/h] then
Haiwezekani mtu ambaye yuko huru, tena yuko likizo, ameamua kwenda kujipumzikia zake nchi za wenzetu, azuiliwe!.

Nafahamu kuna wafanyakazi wa serikali, na baadhi ya idara nyeti, au hata madakitari, jeshi, polisi na zimamoto, hata wakiwa likizo, wanawajibika kumtaarifu mwajiri wao, likizo yake atakuwa wapi, ili in case of anything, aweze kuwa reached out!, lakini kitendo cha maofisa uhamiaji, kumzuia mtu mwingine yoyote wa serikali, asisafiri nje ya nchi, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu!.

Pamoja na nia nzuri, na nia njema ya Rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kudhibiti safari za nje ya nchi zisizo na tija kwa taifa, utekelezaji wa kauli hiyo, lazima uzingatie taratibu, sheria na kanuni, na sio kutekelezwa tuu kama zimamoto, na kukiuka haki za msingi za binadamu!.

Ila pia niliwahi kushauri humu, kama baadhi ya sheria, zinaweza kuwa ni kikwazo kwa rais wetu, kututengeneza Tanzania tunayoitaka, rais anayo mamlaka ya kisheria, kuandika waraka, 'decree' kuiweka kando katiba , hivyo kuitawala Tanzania kwa kutumia decree hivyo kuwa huru kufanya jambo lolote atakavyoona inafaa!.

[h=3]Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria Ongoza Kwa Kutumia Decree tuu! [/h]
Viongozi wote wanakula kiapo cha utii wa katiba!, kama katiba inatoa uhuru fulani!, haiwezekana, akaibuka mtu mwingine, kwa mamlaka aliyopewa na katiba hiyo, akauondoa uhuru fulani na haku tunamtazama tuu, au tunamshangilia!. Hili haliwezekani!.

Japo wengi wetu, tunaishi katika lindi la umasikini, uliotopea, na sio tuu hatuna hata hiyo likizo, lakini umasikini wetu, usutufanye tuwachukie, wenzetu waliobahatika kuwa wenye heri, wenye uwezo wa kwenda kujipumzikia zao ulaya wakati wa likizo zao!.

Nashauri serikali itoe waraka wa ufafanuzi wa hili katazo la safari za nje, unless itamkwe wazi, watumizi wote wa umma, hata safari zao binafsi kujipumzikia, au kuwatembelea wapendwa wao, wapenzi wao au hata vimada wao, sasa lazima waombe kibali kwa KMK!, na jee kama hivi ndivyo katiba ilivyotamka?!, kama sio kwa mujibu wa katiba, then rais atoe waraka, Tanzania tujijue tuko kama China au Urusi, enzi zile, kuingia Beijing au Moscow, mtu hujiingilii hivi hivi!.

Jee kumkumbusha rais wetu kuhakikisha watendaji wake wanazingatia katiba aliyoapa kuilinda, ni kumuingilia katika utendaji wake?!.

Pasco
 
Kuna tatizo, kama mnakumbuka EU walitoa maoni yao juu ya kukamatwa kwa vijana wa cdm pamoja na wale wa tume ya haki za binadamu lakini hati zao za mashitaka zilionyesha 'human trafficking'.
Huenda yakawa makosa ya aina hii ambayo unakuta huyu mtu alikuwa anasafiri kwa nia njema tu ambayo kwa upande mwingine ingeliweza kuvutia uwekezaji kwa faida yetu sote (bila kujali ni kwa kiwango gani). Nilivyosoma kwenye gazeti la citizen maelezo ya huyu ofisa endapo akiamua kwenda mbele kudai damage inaweza kuwa fundisho kwa wengine.
 
Ben Saanane,
Heshima yako. Sioni shida kutekeleza sheria zilizopo. Katiba ni mchakato. Hata kama Katiba itakuja na iwe nzuri kama Malaika wa Mbinguni ikikosa Sheria na Kanuni haina maana kabisa.

Aidha, lazima tujue bila kupata mtu wa kusimamia hiyo Katiba na sheria zake, hakuna tutakapofika. Tuamini hata Katiba ikija ataisimamia kama anavyofanya. Tunajua vipengele vingi sana vya katiba iliyopo vinavyokanyagwa tangu enzi za Mwinyi, Mkapa hata JK. Shida ilikuwa nini? Katiba, sheria au viongozi!!!

Hivyo, hatuwezi kusitisha kusimamia sheria zilizopo kwa kigezo cha Katiba. Inakuja, kama haiji tutaidai.
Gaza and Israel,

Asante kwa mrejesho.

Katiba ni mkataba kati ya wananchi na watawala. Katiba ndiyo sheria mama.Hata sheria zilizopo tayari Rais na Watendaji walioko chini yake wanazivunja. Rasimu ya Warioba imeweka misingi mzuri ya kustawisha taifa letu kisiasa,kiuchumi na kijamii. Tunu za Taifa zimefafanunuliwa. Katiba inapaswa ijisimamie yenyewe ila iheshimiwe na wote yaani watawala na watawaliwa.

Sasa mtu aliyeapa kuilinda katiba anakuwa mstari wa mbele kuivunja.Au anakaa kimya kushuhudia ukiukwaji wa haki za binadamu.Hiyo ni silent consent !
 
Last edited by a moderator:
Kuna tatizo, kama mnakumbuka EU walitoa maoni yao juu ya kukamatwa kwa vijana wa cdm pamoja na wale wa tume ya haki za binadamu lakini hati zao za mashitaka zilionyesha 'human trafficking'.
Huenda yakawa makosa ya aina hii ambayo unakuta huyu mtu alikuwa anasafiri kwa nia njema tu ambayo kwa upande mwingine ingeliweza kuvutia uwekezaji kwa faida yetu sote (bila kujali ni kwa kiwango gani). Nilivyosoma kwenye gazeti la citizen maelezo ya huyu ofisa endapo akiamua kwenda mbele kudai damage inaweza kuwa fundisho kwa wengine.
Unaonekana kuwa unaelewa in deep unachoandika sasa
 
Ndugu si kweli Magufuli ni dictator ila anasimamia zaidi sheria kuliko ilivyokuwa mwanzo tatizo ni sisi bush lawyers tunakurupuka sana maana kabla hatujajua undani wa jambo tunakuja huku kusema/kulalamika. Hata hivyo maendeleo yanakuja kwa chembechembe za dictatorshihip angalia USA-Roosevelt, Germany-Hitler, China-Mao, Italy- Musolin na France-Napoleon. Democracy ni baada ya kuendelea kama zilivyofanya nchi hapo juu ingawa naelewa mchango wa factors zingine katika uchumi wao.
 
Francis kama umesoma andiko vizuri..huyo Bwana alikuwa likizo anatumia fedha zake mwenyewe kwenda likizo kupunzika hajatumia hata senti tano ya serikali. Nadhani interpretation ya zuio za safari za nje halijaeleweka na waendaji. Naanza kukumbuka Azimio la Arusha miaka 10 baadae..watekelezaji wa AZIMIO ndio walimwangusha JK Nyerere.
 
Jamani ninavyoelewa mimi ni kwamba mtumishi atasafiri nje kwa kibali kutoka IKULU, kwani ukiwa LIKIZO inakuzuia nini kuomba KIBALI na sababu inaeleweka??

OMBA KIBALI, NENDA ZAKO kula raha. Labda kama unatumia na influence ya title ya umma.
 
Nchi iliyokubali kufuata misingi ya demokrasia,Utawala bora wa Sheria ndio alama na katika hilo Uwazi na Uwajibikaji(transparency and Accountability) ndio nguzu kuu.

Hapo kwenye red Bold ni fikra za kijima(Primitiveness).

Utawala bora ni dhana pana sana inajumiusha kuzuia na kupambana na rushwa, utawala wa sheria, uwazi, uwajibikaji, na mengine mengi, Rais ameikuta nchi ipo pabaya hata wewe unafahamu kwaani umekuwa mstari wa mbele kukosoa serikali iliyopita, Utawala wa nchi siyo kama kutawala chama, inahusisha mambo mengi yanayo onekana na yasiyo onekana, kwa kazi za TISS huwezi kuziona physically km siyo mtu wa usalama. Rais anapoingia madarakani kuna vitu vingi anapewa, kwa hali ya kawaida kama apewa taarifa wa ufisadi mkubwa km huu wa bandarini na mengine mengi yanayokuja muda si mrefu utaona, kwanza lazima uzuie watu kutoka nje wasitoroshe pesa na mali au wenyewe kukimbia nchi, lkn mkuu wa nchi hawezi kutangaza kuwa kwa sababu ya kupambana na wezi hivyo amefuta safari za nje, yeye anatumia njia nyingine km hii. naamini kama utakubaliana na me kuwa bila kuzuia safari za nje baadhi ya wafanyakazi wa TRA na BANDARI wangekuwa wameshakimbia, BOT napo ndiyo store yetu ya pesa na hazina zetu, hivyo basi ni lazima kujiridhisha kama hawa watu wanasafiri kihalali.

Pili: Rais alitoa ahadi lukuki km elimu bure na nk, bila kupambana na matumizi mabaya lazima hatu kama hizi zichukuliwe, katika mazingira kama haya kuna makosa madogo yanaweza kutokea, kumbuka makosa hurekebishwa kila yanapotokea ndiyo maana sheria hutungwa na kurekebishwa kila siku, hata katiba ya nchi iliyitufaa kipindi kila sasa tunaiona ina mapungufu.

Labda nikuulize swala dogo, wewe ni mtawala katika kazi zake, km ni yes ina watu wangapi? kama ni taasisi kubwa utazijua changamoto za kiutawala.

Well come tujadili.
 
Huo utaratibu upo na ulikuwepo isipokua watu walizoea kufanya kazi kwa mazoea. Mtumishi anapoenda likizo hua anajaza form na kunyesha kua likizo atakua wapi. mtumishi hata ukiwa likizo ni lazima utoe taarifa kua utakua wapi ili ikitokea emegernce kazini basi wajue namna ya kukupata then compasation ya leave yako itafanyika
 
Sikilizeni wakuu, kwa sasa kuna uchunguzi mkubwa unaendelea kwa watu wanaohujumu uchumi ndio maana kusafiri nje lazima upate kibali maalum.

Serikali haitaki mtu atoke nje ya nchi kwani ni rahisi kutokomea na wakashindwa kuwapeleka mahakamani.

Muacheni Magufuli afanye kazi, mlipewa miaka kumi ya kuchapa usingizi sasa ni mda wa taifa kusonga mbele.

Safari zenu zinaweza kusubiri mpaka uchunguzi ukamilike.
 
Msitetee vitu nusu nusu uyo wa BOT hakuwa na vigezo mbona mwenzie wa TBC alipita na kusafiri.
Jaribuni kukidhi vigezo na masharti wapo wengi tuu wanasafiri why yeye arudishwe kuweni wakweli kwenye hili don't be too general on issues that are specific
 
mi sipo huko kwenye uvunjifu wa haki za binadamu ila nipo kwenye zuio Zima kwa ujumla...kumekuwa na watu wakishangilia 'kila' anachofanya mheshimiwa...sijui kama watu wanapata muda wa kuyatafakari hayo maagizo au mazuio...yapo mengi pia nadhani wanaotakiwa kuya-define wanapotosha...'niko likizo natumia hela yangu sina tuhuma yoyote kwanini nizuiwe kusafiri?' ni wrong interpretation...ila utasikia watu tumbua tumbua tumbua huku wakinyanyua hadi miguu!!siyo haki...nadhani kun sababu ya wahusika kutoa mipika ya hilo zuio!

Mnaondoka likizo munaenda nje kuficha mabilioni muloiba katika wizara zenu? Naomba magufuli atie kufuli airport hakuna kiongozi yoyote wa serikali kuondoka bila ya.kuomba kibali kutoka kwake mpaka pale serikali itakapo ridhishwa na wizara zote kwa upotevu wa fedha za Umma.

Utaratibu huu ningependa uwe mwaka mzima kwa.kuanzia, mana huko tuliko toka mumefanya ufisadi wa kutosha, sasa munakimbia eti holiday.
 
Ndugu si kweli Magufuli ni dictator ila anasimamia zaidi sheria kuliko ilivyokuwa mwanzo tatizo ni sisi bush lawyers tunakurupuka sana maana kabla hatujajua undani wa jambo tunakuja huku kusema/kulalamika. Hata hivyo maendeleo yanakuja kwa chembechembe za dictatorshihip angalia USA-Roosevelt, Germany-Hitler, China-Mao, Italy- Musolin na France-Napoleon. Democracy ni baada ya kuendelea kama zilivyofanya nchi hapo juu ingawa naelewa mchango wa factors zingine katika uchumi wao.

Mkuu tafadhali sana.Muheshimu sana Roosevelt usimuweke kundi moja Fashisti Musolini na wengine wanaotoa Amri holela. By the way zile taka zilizokusanywa bado zimetelekezwa barabarani
 
Back
Top Bottom