Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Haki ni moja ya tunu kubwa na muhimu kwa taifa lolote, nchi ukiwa na haki, inabarikiwa, nchi ikikosa haki inalaaniwa.
Vivyo hivyo kwa Watawala, tumeshuhudia watawala wakitawala kwa haki, utawala wao ukibarikiwa, na watawala wakitawala kwa hila, utawala wao ukifitinishwa. Wamekuwepo watawala wenye nguvu sana wakiwemo Mafarao, Wafalme kama kina Nabukadreza, Belshaza, Suleiman, na wengine wengi, hivi sasa hawapo kutokana na kukosena haki kwenye utawala wao.
Kuna msanii wa muziki wa kizazi kipya wa enzi hizo akijiita Balozi Dola Soul, kwenye moja ya nyimbo zake aliweka kibwagizo "wengi walikuwepo na sasa hivi wako wapi?".
Huu ni mfululizo wa makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zinaandikwa kwa mfumo wa swali au maswali ambayo yatafanya viongozi wetu kujitafakari, kwa maswali fikirishi, na wewe msomaji utapata majibu yako kwa kila mtu atakuwa na jibu lake.
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, inayofuata katiba na utawala wa sheria!.
Ndani ya katiba ya JMT kuna vifungu rasmi vya haki za msingi za binaadamu!. Moja ya haki hizo ni kipengele hiki
Haiwezekani mtu ambaye yuko huru, tena yuko likizo, ameamua kwenda kujipumzikia zake nchi za wenzetu, azuiliwe!. Huu ni ukiukwaji wa haki msingi za binaadamu.
Nafahamu kuna wafanyakazi wa serikali, na baadhi ya idara nyeti, au hata madakitari, jeshi, polisi na zimamoto, hata wakiwa likizo, wanawajibika kumtaarifu mwajiri wao, likizo yake atakuwa wapi, ili in case of anything, aweze kuwa reached out!, lakini kitendo cha maofisa uhamiaji, kumzuia mtu mwingine yoyote wa serikali, asisafiri nje ya nchi kwa safari binafsi, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu zilizo ainishwa kwenye katiba yetu.
Pamoja na nia nzuri, na nia njema ya Rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kudhibiti safari za nje ya nchi zisizo za lazima na ambazo hazina tija kwa taifa, utekelezaji wa amri hiyo, ni lazima uzingatie haki za msingi za binaadamu zilizotolewa na katiba yetu na kufuatwa kwa taratibu, sheria na kanuni, na sio kutekelezwa tuu kama zimamoto, na kukiuka haki za msingi za binadamu!.
Ila pia niliwahi kushauri humu, kama baadhi ya sheria, zinaweza kuwa ni kikwazo kwa rais wetu, kututengeneza Tanzania tunayoitaka, rais anayo mamlaka ya kisheria, kuandika waraka, 'decree' kuiweka kando katiba , hivyo kuitawala Tanzania kwa kutumia decree hivyo kuwa huru kufanya jambo lolote atakavyoona inafaa!
Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria Ongoza Kwa Kutumia Decree tu!
Katiba ya nchi ndio sheria Mama, Viongozi wote wakuu wa umma, baada ya kuwachagua, tunawaapisha, wanakula kiapo cha utii wa katiba!, kwa kuapa watailinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumuomba Mungu awasaidie.
Kama katiba inatoa haki fulani na uhuru fulani! haiwezekani, mtu aliyeapa kuilinda katiba, akaibuka kwa mamlaka aliyopewa na katiba hiyo, akauondoa uhuru fulan au haki fulani na huku Watanzania wengine wote tukimwangalia tuu, au tunamshangilia tuu!. Huku ni kwenda kinyume cha katiba, wote tukiendelea kunyamaza tuu, kunaweza kusababisha mtenda haki Mkuu, kuingilia kati kama kwenye zile tawala za nyuma, hivyo the best thing we can do, ni kwa sisi baadhi yenu kusema tuu, maana huo ndio mwisho wa uwezo wetu, kusema, au kuandika tuu na kuwaachia wenye uwezo wa kutenda watende!, na maadam wenye uwezo huo nao wameamua kunyamaza, matokeo ni Mtengaji Mkuu wa yote, ataingilia kati na atatenda!.
Japo wengi wetu, tunaishi katika lindi la umasikini, uliotopea, na sio tuu hatuna hata hiyo likizo, lakini umasikini wetu, usitufanye tuwachukie, wenzetu waliobahatika kuwa wenye heri, wenye uwezo wa kwenda kujipumzikia zao ulaya wakati wa likizo zao!.
Nashauri serikali itoe waraka wa ufafanuzi wa hili katazo la safari za nje, unless itamkwe wazi, watumishi wote wa umma, hata safari zao binafsi kujipumzikia, au kuwatembelea wapendwa wao, wapenzi wao au hata vimada wao, sasa lazima waombe kibali kwa KMK!, na jee kama hivi ndivyo katiba ilivyotamka?!, kama sio kwa mujibu wa katiba, then rais atoe waraka, Tanzania tujijue tuko kama China au Urusi, enzi zile, kuingia Beijing au Moscow, mtu hujiingilii hivi hivi!. Lazima uombe kibali.
Jee kumkumbusha rais wetu kuhakikisha watendaji wake wanazingatia katiba aliyoapa kuilinda, watimize wajibu wao kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni ni kumuingilia katika utendaji wake?!
Pasco

Kama jambo hili ni kweli limefanyika,Kigogo wa BoT azuiwa Airport kutokana na kukosa vibali vya kusafiri nje ya nchi thenUhuru wa mtu
kwenda atakako
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
17
(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya
kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.
(2) Kitendochochote cha halali au sheria yoyote yenye madhumuni ya
(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako na kumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au
(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu kwenda anakotaka ili kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;
au
(ii) kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibu wowote anaotakiwa na sheria nyingine kuutimiza; au
(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumla au
kuhifadhi maslahi fulani mahususi au
maslahi ya sehemu fulani ya umma,
kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyo
haitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibara hii