Je Huu si ni Ubaguzi Katika Bima ya Afya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Huu si ni Ubaguzi Katika Bima ya Afya?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichankuli, Mar 24, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Mfuko wa Bima ya Afya kwa Watumishi wa Serikali umeanzishwa kisheria ambapo kila Mtumishi hulazimika kusajiliwa na kukatwa asilimia 3 ya mshahara wake kila mwezi kuchangia bima hiyo. Leo asubuhi Mkuu wa Mfuko huo alikuwa akihojiwa na ITV, na moja wapo ya mambo aliyoyaongea ni upanuzi wa huduma zinazolipiwa na Mfuko huo kujumuisha kipimo cha CT Scanner. Katika maelezo yake alieleza kwamba pamoja na kipimoo hicho kuwa covered na Bima ya Afya, ni kweli kwamba wanachama wake wengi wanaweza kutonufaika na kipimo hicho kutokana na hospitali nyingi kutokowa na vifaa vya kuwezesha kufanya kipimo hicho.

  Kwa maoni yangu naona kwamba Menejimenti ya Mfuko wa Bima ya Afya haututendei haki wanachama wake na badala yake inatubagua kutokana na maeneo ambayo tunaishi na kufanyia kazi. Naamini kwamba kwa kutumia fedha tunazokatwa Menejimenti ya Bima ya Afya wageweza kufungua maabara kwa kila mkoa na baadaye kuteremka zaidi hadi kwenye kata. Au la, wanachama tuwe tunagharamiwa fedha za nauli na kujikimu pale inapoonekana kwamba mwanachama mgonjwa anatakiwa kupimwa kipimo hicho.

  Ubaguzi mwingine ambao ninauona katika Bima ya Afya ni ule wa kuwa na makundi mawili ya wanachama. Kuna wanachama ambao wanapewa vitambulisho vyenye sehemu yenye rangi ya kijani ambao hawa huruhusiwa kutibiwa hospitali yeyote. Wanachama wengine ni wale wnye vitambulisho vya rangi nyeupe ambao hawawezi kutibiwa kwenye hospitali kama Mikocheni au Aghakani (siyo zahanati za Aghakani). Nionavyo mimi hii siyo haki kwa sababu Mfuko huu ni wa lazima kisheria, vinginevyo ungefanywa wa hiari kama ule wa Mfuko wa Afya ta Jamii (CHF) na kwamba Mtumishi aambiwe kuna aina mbili za uanachama ili aweze kuchagua wapi anapopenda kuchangia kama ni VIP au Kima cha Chini. Msingi wa hoja yangu ni kwamba kwa vile hakuna utaratibu wa kukokotoa kila mwanachama ametumia gharama kiasi gani kwa mwezi au mwaka katika matibabu na kwamba kuna uwezekano wa Mtumishi Mwanachama wa ngazi ya chini kutotumia huduma ya Bima ya Afya kwa mwaka mzima au zaidi na yule wa ngazi ya juu kutumia zaidi; ni wazi kwamba kila mmoja wa wanachama anao uwezekano wa kutumia fedha za mwanachama mwenzake katika kukidhi gharama. Na hii ndiyo mantiki ya kuunda Mfuko wa Bima ya Afya ili wanachama wakusanye nguvu zao za kifedha kuweza kumkabili adui maradhi. Hakuna haja ya kuwatenga wanachama kwa makundi.

  Wana JF mna maoni gani?
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Hapa ndugu yangu kuna ufisadi wa mkubwa unaendelea chini kwa chini, karibu wanachama wote wa mfuko huu hawaridhiki na huduma zake na pia utaratibu wa makato umekaa kibabe mno. Kwanza wagonjwa wanao tumia kadi hizi hawapewi huduma inavyo stahili hasa huko vijijini kwa sababu hawachangii vituo vya afya moja kwa moja. Hata dawa hutolewa kwa shida na pengine huambiwa wafuate katika maduka yaliyoingia mkataba na mfuko huu kuhudumia wateja wake. Huko nako ni balaa tu wenye maduka haya huwa hawatoi ushirikiano kwa wagonjwa na mara nyingi huwa hawatoi dawa. Ukiwauliza kwa undani utagundua wanafanya hivyo kwa kuwa mfuko huchelewa sana kuwalipa pesa zao hivyo. Hata mikataba na maduka haya inatia shaka kwani hutolewa bila kujali hadhi au ukubwa wa duka lenyewe hivyo kuwanyima wateja wao huduma wanayo stahili.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Je kila mwanachama hutoa mchango sawa?

  Kama mwal. wa primary anatoa mchango wa 6,000 na Daktari 30,000 je wapate matibabu yaliyo sawa? Ndo maana kuna wanaopewa kadi zenye rangi tofauti!

  Does government provide support kwa wanatoa kidogo ili kupata vipimo kama CT Scan?

  Ikumbukwe pia Tz hatuna Universal Health Insurance Covarage: na kama ukiwa mlala hoi ukiungua basi ni shida sana ndugu yangu!

  Ikimbukwe watz wote ni binadamu na wanahitaji kuhudumiwa kama watu wengine: uwe maskini au tajiri, au uwe na kazi au mlala hoi!
   
 4. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkuu je katika kuugua je ugonjwa unachagua kipato chako au mchango wako katika huu mfuko??

  Je kama wewe umechangia kiasi kidogo inapotokea unahitaji kipimo kikubwa kama cha CT scan husipimwe kwakuwa wewe mchango wako ni mdogo??

  Je katika uanzishaji wa huu mfuku je wadau wake walitaarifiwa kwamba kutakuwa na makundi ya wafaidika na huu mpango??

  Swala la pili ni kwa watoa huduma husika mahospitali,zahanati na maduka ya dawa, wao wameingia mkataba na Bima ya afya na sio wanachama wa bima ya afya, kwa hiyo basi ucheleweshaji wa malipo wanayodai sio sababu ya kuwanyanyapaa wanachama wa mfumo huu. Kwani katika mikataba yao wamekubaliana kwamba, watalipwa baada ya muda fulani na baada ya mfuko wa bima kuhakiki madai yao kama yapo sahihi au la kulingana na vigezo walivyowekeana.

  Nina experience na mifumo hii ya bima ya afya nchi Tanzania kwa muda mrefu tu (manake mimi ni miongoni mwa waanzilishi wake kwenye sekta binafsi) Kinachotokea mara nyingi ni kwamba watoa huduma wengi wa Tanzania sio waaminifu. Kila wanapotoa huduma(matibabu na madawa) wa wanazidisha bei au wanakuchaji huduma ambayo hakupewa. Kwani wateja/wadau wengi huwa hawaelewi uhandishi wa kidaktari( lugha wanayoandika kwenye cheti cha mdau)


  Upungufu mwingine ni mfumo wa uhakiki wa malipo ya huduma zilizotolewa kwa wadau.
   
 5. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
   
Loading...