Je, huo nao ni ushujaa?

Je, huo nao ni ushujaa?

Mp

Mpendazoe kalime hata bustani na mbogamboga inalipa pia,usilazimishe biashara ambazo hazilipi,ukiona ya kulima Bustani haikulipi nenda hata Nigeria au Congo ukatafute hata uchungaji wa ndumba inalipa pia,huko uanakokulazimisha uzeeni utakuja tembea peku,kuongea peke yako barabarani na kuvaa suruali zilizotoboka matakoni.
Qr
1479376027165.jpg
1479376027165.jpg
 
Duh! Kama wanasiasa wenyewe kama hivi basi Maendeleo ni ndoto sana kwa TZ. Mie na subiri vijana wa Kata pengine watatutoa.
 
Katika mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti yanaandika Sana kuhusu baadhi ya wanachama wa chama kimoja cha siasa hapa nchini kukamatwa na polisi na kuwekwa mahabusu na baadae kuhojiwa na kupelekwa mahakamani.

Wanachama hawa wamekamatwa kwa tuhuma mbalimbal zikiwemo kufanya uchochezi au kukaidi maelekezo waliyopewa na vyombo vya usalama. Wengine wamekamatwa kwa kutumia lugha chafu kwa viongozi hasa wa chama kinachotawala ambao wamepata ridhaa ya watanzania wengi kuongoza nchi..

Serikali ya JPM ndiyo iliyochaguliwa na watanzania wengi na iko kikatiba, hivyo ni halali. Hivyo serikali ya JPM siyo ya dikteta.

Kumekuwepo madai kwamba JPM anawanyanyasa watanzania na hashauriki. Siyo kweli, JPM analo baraza la mawaziri linalomshauri na anacho chama chake kinachomshauri. Pia anao watalaam wanaomshauri katika masuala mbalimabali. Hivyo hoja hizi hazina mashiko.

Kibaya zaidi Upinzani leo, hasa Chadema hauishauri serikali bali unaitukana na kuikejeli.

Hata hivyo, kwa muda mfupi, serikali ya JPM imeonesha mwelekeo wenye kuleta matumaini kwa watanzania.

• JPM ameonesha dhamira ya kweli ya kupiga vita ufisadi ukilinganisha na baadhi ya vyama vinavyompigia kelele kwamba ni dikteta.

• JPM anapiga vita rushwa, uzembe kwenye serikali, ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka.

• JPM anachukua hatua kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watanzania wengi
• JPM anasimamia kwa karibu watendaji na kufuatilia kwa karibu kero za wanachi, hakuna ombwe la uongozi.

• JPM ameweza kuchukua maamuzi magumu, mfano elimu bure; mchanga wa madini usipelekwe nje ya nchi.

• Hatua alizochukua JPM dhidi ya wizi bandarini na sehemu nyingine zinaonyesha uzalendo wake.

• JPM anatekeleza vizuri ilani ya uchaguzi ya chama chake kilichopewa ridhaa kuongoza na watanzania.

Kwa hatua hizo alizochukua JPM ni mtanzania yupi mzalendo ambaye amenyanyaswa au kuonewa ?

Kwa ujumla, JPM ameleta heshima kwa nchi yetu hadi nchi za nje zinaanza kuchukua hatua ambazo JPM amezichukua hapa Tanzania.

Mtanzania yeyote anayenung’unika kwa hatua hizo zilizochukuliwa na serikali ya JPM ni dhahiri uzalendo wake una walakini na ni dhahiri pia anapigania maslahi yake binafsi au maslahi ya kikundi cha watu fulani wachache wala si maslahi mapana ya nchi yetu.

Lakini pamoja na hayo yote baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani tena wenye elimu nzuri wanamkejeli na kumwita JPM eti dikteta uchwara, KWELI INASIKITISHA. Lakini, ni kwa lipi hasa wamwite dikteta uchwara?

Wapo wanachama wa chama kimoja wanawasifu hawa viongozi waliokamatwa na kuachiwa kwa dhamana eti ni mashujaa. Je, ni kipi cha maana na heshima kwa nchi yetu wanachokipigania hadi waitwe mashujaa?

Wapo wanachama wa Chama kimoja wanaodhani kuwekwa rumande mara Kwa mara ni ushujaa.

Ushujaa wao uko wapi? Je kukamatwa na kuwekwa rumande kwa kuitukana serikali ni ushujaa ?

Je, kuwekwa rumande na baadae kupata dhamana kwa kuandamana bila kibali cha polisi ni ushujaa?

Je, kukamatwa na vyombo vya dola kwa kukaidi maelekezo ya vyombo hivyo ni ushujaa? Hapana.

Wanachokifanya wanachama hawa ni uchochezi wenye lengo la kuvuruga amani. Watanzania tukatae upotoshaji huu na tuwapuuze. Nawasihi watanzania tuinge mkono serikali ya JPM.

Juzi kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Democrati huko Marekani Mama Obama amewatahadharisha na kuwataka wamarekani kuwapuuza viongozi wanaotukana ovyo hadharani kwani wanajenga fikra mbaya kwa vijana wamarekani. Mama Obama alikuwa anamzungumzia mgombea wa chama cha rebublican ambaye ni msema ovyo, ambaye ana lugha ya matusi kwa viongozi na amekuwa akimtukana rais Obama kwenye mikutano.

Mama Obama ameuliza, Je vijana wa marekani wanajifunza nini kwa viongozi hawa wanaotumia lugha chafu hadharani? Ni dhahiri maadili ya vijana wa marekani yatakuwa hatarini. Kwa mtazamo huo wa Mama Obama, vijana wetu hapa Tanzania wanajifunza nini wanaposikia lugha za matusi kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa ?.Vita ni siasa inayomwaga damu kwani haina majadiliano wala ushawishi. Ni ugomvi.Vyama vya siasa viepukane na ugomvi.Vijenge hoja na viwashiwishi watanzania kuhusu sera zake.

Je, ikitokea kijana akamwambia baba yake kwamba ni baba uchwara atajisikiaje?Au akakuambia wewe mama ni mama uchwara. Je utafurahi jirani yako akimpongeza huyo kijana na kumwita shujaa ?

Je haiwezekani kudai haki nademokrasia bila kutumia matusi na kejeli kwa serikali iliyoko madarakani?.Upinzani ujifunze kwamba, siasa za kiuanaharakati kwa Tanzania hazikubaliki

Tukumbuke Nyerere alidai uhuru kwa kutumia hoja za msingi hadi wakoloni wakatoa uhuru. Siasa ni vita isiyo mwaga damu. Ni majadiliano na ushawishi.
Hata sasa inawezekana kudai haki, kuikosoa serikali bila kutumia lugha ya matusi.

Na mtu yeyote asiyetaka kuongozwa hawezi kupata fursa ya kuogoza.

Tafakari hii....."Itakuwa ni kosa na haina umuhimu kudhani kuwa ni lazima tusubiri hadi viongozi wafariki kabla ya kuanza kuwakosoa"JKN.

Mchochezi wa kwanza wa Taifa hili ni JKN kupitia quotes na vitabu vyake.Ishauri serikali kuchoma moto taarifa,mikutano,hotuba,vitabu vyote vilivyoandikwa na JKN.

Pole,haki ya Lema ni kuhoji na kuikosoa serikali,kukutana na wapiga kura wake.
 
uteuzi kwa kuangalia vitu maalum umekwisha..lakini jitahid stakuangusha!
 
Ni demokrasia gani unayoizungumzia Mh Mpendazoe?
Katika mazingira tuliyonayo sasa ambapo hata kuota ndoto na kusimulia wengine ni kosa la kijinai. Unataka watu wafunge midomo?
Mh Mpendazoe ni Kwa vipi nchi hii itapiga hatua katikati ya wanafiki?
 
Back
Top Bottom