Je, huo nao ni ushujaa?


Masikini Mpendazoe! Sasa sijui haya maneno yako utayaweka wapi? au ndiyo utakula tena matapishi yako kama ulivyozoea?!

Mtu uliyembeza Donald Trump tayari Wamarekani wamemchagua kuwa Rais wao? Au unataka kutuaminisha kwamba wewe una akili sana kuliko hao Wamarekani waliomchagua Donald Trump.
 
CHADEMA wanatapatapa kama mfa maji
Ndugu Mpendazoe ni msakatonge tu na mtu asiye na msimamo. Makala zake za kuitukana serikali ya ccm akiwa chadema leo anakula matapishi yake?Mpendazoe wekeza kwenye kilimo siasa imekushinda
 
Kaka Fred,
Ni haki yako kabisa kikatiba kutoa maoni yako na si busara mtu kukutukana uapokuwa umetoa maoni yako ambayo kikatiba uko sawa.
Binafsi napenda tu kujibu andiko lako japo kwa ufupi,
Kwanza yale unayoyaona kwa mtizamo hasi kwa sasa ni muda mfupi sana uliandika na kusimama majukwaani ukiyaongea kwa mtizamo chanya kiasi kwamba nakuwa na wasiwasi kama ni kweli yanatoka moyoni au ni kwa sababu tu kuna matumaini unayafikiria kwa kuwa na mtizamo huo.
Hizo credit unazozitoa kwa mh raisi pia mimi sipingani na wewe japo ningependa pia nami niayasemee kwa jicho jingine,

Kupinga ufisadi sikatai,binafsi ningefikiria kuwa, hiyo speed ya upingaji wa ufisadi haiendani na majeraha ambayo nchi hii imeyapata,kama dhamira ndo kulifanyia kazi hilo, ingekuwa vizuri mh raisi aanzie kwenye mapendekezo ya bunge. Hayo mapendekezo ya bunge kuhusu mstakabari wa nchi juu ya ufisadi tukianzia na RICHMOND mpaka EPA.
Rushwa pia anaenda vizuri tatizo ni kwamba huu mziki anacheza peke yake,sioni kama watendaji wake kulisimamia ipasavyo suala hili,juzi kumeibuka mgao wa milioni kumi japo limetolewa ufafanuzi kuwa walikuwa wakigawana pesa zao. Kama mwenyekiti nilifikiria hata asingemaliza siku mbili bila kulitolea maelezo, kama ilivyokuwa kwa aliekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga. Harufu ya rushwa kwa anaeipinga waziwazi haitakiwi wananchi tubaki na maswali bila majibu.Ukimya waweza kutafsiriwa kama YES au NO.

Kwenye maamuzi magumu umetolea elimu bure,hiyo elimu kweli na iwe bure...tujiulize kwanza hiyo elimu ya bure ni mpaka level gani? Je hiyo level inawasaidia watanzania kwa kuitwa wamepata elimu? Katika suala la elimu kiukweli hali yetu si nzuri na mimi binafsi naona kama asipoangalia na kuliweka sawa hayo maamzi magumu yataturudisha nyuma kidogo. Nasema hivyo sababu,mpaka leo hii kuna wanafunzi walitakiwa kujiunga na vyuo vikuu bado wako majumbani au wako vyuoni lakini hawaingii madarasani kwa ajiri ya kutofanya usajiri kwa kutokulipa ada. Hiyo elimu bure imewasaidia nini hawa? Nilifikiri mh angetimiza ilie ahadi yake aloitoa Tabora wakati wa kuomba ridhaa ya uongozi wa nchi ya kuwa wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu watapata mikopo bila kubaguliwa.....sasa leo wanabaguliwa kwa vigezo lukuki. Bila kufikiria ya kuwa elimu yenyewe wanayoitaka hawaihitaji bure bali wanaomba wakopeshwe!!! Pesa ni za serikali na elimu ni haki yao. Ndugu yangu Fred umesema tu elimu bure ukaishia hapo mi nakuambia sio kweli ELIMU sio bure! Na hili lingeenda pamoja na pale uliposema anasimamia rasilimali za nchi ziwanufaishe watanzania waliowengi! Nilifikiri lasilimali za nchi watoto wapewe elimu bila kubaguliwa hata kama iwe kwa kukopeshwa na sio bure lakini bila ubaguzi,wafaidike wote kuliko ilivyo sasa imekuwa ovyo hata zaidi ya awamu iliyopita.
 
NAJIONA KABISAAA "NAKULA BAN YA MAISHA"....EEE MWENYEJI MUNGU NINUSURU MJA WAKO NA HAYA MAJARIBU ANAYOTULETEA SHETANI KUPITIA MZEE FREDDY MPENDAZOE.....AMEEN.
 
Crap!


We Mzee wenzio wanatafuta kick kwa kutumia Nyota ya Lowassa na sio Lema... Duh umesahaulika sana... Omba nafasi ya Mrema maana hafiti kabisa...
 
NAJIONA KABISAAA "NAKULA BAN YA MAISHA"....EEE MWENYEJI MUNGU NINUSURU MJA WAKO NA HAYA MAJARIBU ANAYOTULETEA SHETANI KUPITIA KIBARAKA WAKE MZEE FREDDY MPENDAZOE.....AMEEN.
Mkuu umetisha... kwani ulitaka kumusi au kumcrash?
 
Nafasi za Uteuzi zimeisha Mkuu. Jaribu kiki nyingine.
Halafu sijui ameshapona pale alipokatika mkia maana alirudi zizini akiwa na kidonda cha kukatika mkia.

Hata akijikomba vipii haaminiki tena ndani ya chama ndio maana hajapewa hata usemaji wa chama. Kwa sababu ya kuwa kigeugeu na kuangalia masilahi binafsi. Hata hapo CCM atavumilia kwa muda akiona bado hawajampa cheo atasepa tena kwenda ACT au hata kwa Dovutwa.
 

Huyu sio Mpendazoe jamani atakuwa Shilole, Mpendazoe hawezi kuandika hii pumba hata kama njaa imemlemea kiasi gani!

Huyu sio Mpendazoe jamani atakuwa Shilole, Mpendazoe hawezi kuandika hii pumba hata kama njaa imemlemea kiasi gani!
 
Huyu pandikizi kumbe yumo humu pia? Nani anaweza kumsikiliza tena? unless you are a moron.
 
Dah! Mi watu kama hawa kila wanachokiandika naona ni unafiki tu.
 
mpenda Zoe umejidhalilisha sana lakini nimejikuta nikisita kuendelea kukoment baada ya kujua kuwa na wewe ni ccm ..unasubiri mmoja atumbuliwe ukae hapo maana ndio pekee mnachokitafuta...

kila kheri!!
JPM hachangamani na ng'ombe waliokatika mikia, atasubiri sana!
 
Umeongea jambo zuri.....ila viongozi wengi wa kiserekali na wanasiasa hata Rais mwenyewe ndio wanao ongoza kutoa lugha za kubeza
Huyo huyo anaemtetea ndie aliemwita ng'ombe asomkia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…