Je, huo nao ni ushujaa?

Naona unajitahidi mkia uote ila haiwezi kuwa rahisi kiivyoo!
 
Unatia huruma sana mzee. Siku ile unatoka CCM ulidiriki hata kumtaja mama yako kwa jina na kusema CCM haijakuzaa na kusema dhamira yako ilikuwa inakusuta kipindi chote ukiwa kwenye hilo lichama chakavu, leo njaa imebana unakula matapishi yako???Duuu, unampa shida sana mwanao aisee.
 
Nchi hii kuna watu wanajifanya wanajua kuliko wengine. Wanajifanya wazalendo kuliko wengine. Wanajifanya kile walichonacho kwenye ubongo wao ndio bora kuliko cha wengine.

Rais aliyepita alikuwa na uungwana wa hali ya juu mno, aliweza kukubali kujishusha ili hao wanaopenda kujikweza waweze kujikweza kadri wanavyojisikia. Bahati mbaya tabia ya JK haifanani na ya JPM, kwa JK kuweza kuvumilia na kujifanya mdogo ili wengine waweze kujipa ukubwa hewa, hakumaanishi kwamba JPM nae ni lazima afuate tabia hiyo hiyo.

Ukimkejeli JPM na ushahidi dhahiri ukapatikana, ukileta sarcasm kwenye stage huku watu wakikurekodi kwa simu zao, then my friend you will be in for a hard time of your life.
 
Well said. SIDHANI KAMA TUTAMPATA RAIS SHUJAA KAMA MAGUFULI.
 
Ushapewa mgao wako wa milion 10?
Km bado muone LIZABONI AU WAKUDADAVUA akupe pesa yako milion 10
 
ccm hii ndio imejaa rushwa na raisi kabariki rushwa kwa wabunge wake, rushwa gani atapambana nayo? sidhani mkuu!
 


Mzee kwa umri wako inakupasa uww mkweli na si kuleta hoja zenye kulenga kuwafurahisha kundi Fulani bila kujali maslai mapana ya watu wanyonge.

Serikali hii inakosolewa kwa haki na si kwamba wapinzani wanakataa kila kitu kinachofanywa na serikali hii.Kwa mfano unawezaje kuipongeza serikali hii kwa haya yafuatayo:-

1.kubana matumizi halafu dawa hakuna mahospitalini.
2.kununua ndege za usafiri Wa ndani ambapo watanzania wenye kupanda hizo ndege hata 5% hawafiki na bado kuna mashirika binafsi ya ndege yanayooparate na hawajazi abiria alafu watoto Wa masikini wanakosa mikopo vyuoni.
3.Kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020 wakati nchi hii ni ya vyama vingi.
4.Biashara zinapolomoka tunaambiwa tunaficha Pesa kwenye magodoro.
5.makaburi ya mafisadi dagaa yanafukuliwa wakati makaburi ya mafisadi papa yanaachwa.

N.k
Muone aibu wazee, Taifa bila wazee ni tatizo lakini kuwa na wazee wasioweza kulisaidia Taifa ni tatizo zaidi.
 
Wahanga wa tetemeko walishapewa pesa yao waliyochangiwa na watanzania wenzao?
Kwani zile 10mil walizogawana zilitoka wapi?? Tuanzie kwanza hapo
 
Njaaa inakupelekesha tafuta shuguli nyingine ufanye..

OVA
 
[QUOTE "kirerenya, post: 18394615, member: 166436"]Kwa nini usijikite kujadili mada?[/QUOTE]
Mada ipi ya kujadili hapa kwa mfano?
 
Anajitahidi kuotesha mkia wake tena.


Jaribu kupenda chache, ukipenda zote utazikosa jamaa yangu
 
Baada ya siku zile kufululiza na post naona umeibuka tena leo
 
Acha tabia za kujikomba komba mkuu ili uonekane nawe upo.... Ni bora nipige Story na vibonzo vya masoud kipanya na sio akili hz za vijana wa rumumba

Mpendazoe siyo kijana tafadhali, ni mzee ambaye njaa imempiga sana hata akasahau kuwa wazee wa umri wake kazi yao kubwa katika jamii ni kutoa ushauri wa busara na si unafiki
 

Ulivyosema Mkapa ni mwizi kule bungeni sasa ameacha?CCK imefia wapi halafu CCM hawakwamini kwa sababu mkia wako umekatika.@Mkulu
 


Duh uko mzee, nadhani nimiongoni mwa wale waliopokelewa wakafananishwa na Ng'ombe wasio na mikia, any way komaa bado kuna nafasi za uteuzi, jitahidi kuwa mvumilivu tu utatoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…