Je, huku ndio kupendwa?

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
378
Habari zenu?

Jamani mimi simuelewi mpenzi wangu kabisa. Tuligombana ugomvi mkubwa tu sababu ya jamaa mwingine kuingilia mapenzi yetu kwa wivu. Ugomvi huo ulipelekea mpenzi wangu kunitamkia kuwa mimi na yeye imebaki kuwa historia. Alinipenda mpaka kunitambulisha kwao kama rafiki na kujitoa kwa kila kitu lakini baraka zinaanzia kwa watu hivyo mimi na yeye tumekosa baraka hizo hivo hawezi kunioa.

Nililia na kuomba msamaha kwa kila namna. Njia zote ziliposhindikana nikamwambia yeye ameniacha ila mimi sijamuacha. Nilisema hivyo kwa kujipa moyo huku nikiona kweli mwanaume kaamua. Cha ajabu ninachoshangaa hasa, baada ya kuonyesha msimamo huo, mwenzangu amekubali kurudi chini.

Akaahidi kuwa hatoniacha tena mpaka aondoke hapa duniani. Ingawa hatuonani mara kwa mara sababu za kikazi lakini kila ninachoomba atalalamika kidogo na nikimkazia anafanya nitakavyo. Sasa sielewi haya ndo mapenzi au ni nini jamani?
 
Mmh hujaeleweka vizuri ila kama vipi mwambie aje ajitambulishe kwenu akuoe ili uthibitishe kama kweli hayo ndo mapenzi ama laa
 
inategemea aisee,, anaweza asikuache ila ukateseka maisha yako yote kila la kheri
 
Kama ambavyo kwenye huu uzi hueleweki vizuri vivyo hivyo hata kwenye mahusiano.
 
Mhh!! Mkazie aje apajue kwenu atoe mahari na akuoe.. Kufanya hivyo itakuwa lweli kuwa hatokaa akuache
 
Jipime uone kama hapo ulipo una furaha au la. Ni upumbavu kung'ang'ania sehemu ambayo huna furaha. Maisha siyo mapenzi tu, vipo vingi vya kufanya ukiwa umesimamisha mapenzi kwa muda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom