Je, historia/malezi inaweza kuathiri ndoto zako?

Lamkyeku

JF-Expert Member
Apr 18, 2014
494
661
Noamba tushare experience!


Mimi nilihamia kuishi kwa shangazi yangu nikiwa darasa la pili, alikuwa mlevi sana yeye na mume wake, mtoto wake wa mwisho alinipita miaka mitano wengine walikuwa tayari watu wazima na hawakuwa pale, nikiwa darasa la tatu yeye alimaliza darasa la saba, alikuwa anadekezwa huyo mtoto wa kiume mpaka nguo nilikuwa namfulia, mimi ndio nilikuwa hausegirl naamka saa kumi naamza na kupika chai, vyombo, kufagia uwanja, kudeki na kumwekea maji ya kuoga, maana alikuwa ni mwalimu, saa mbili na nusu ndio nafika shuleni na nikifika ananichapa mbele ya walimu wenzie akijinasibu kwamba nalala mpaka saa moja au ameniacha sijaamka ili walimu wake wajua kwamba hanitesi, saa nane nimesharudi nyumbani ili niende sokoni na pia kukata majani ya ng'ombe, kufua na kuanza kupika cha jioni mana saa nne ndio huwa wanarudi tena wamelewa na matusi juu. Sikuwahi kushika nafasi ya pili darasani toka nianze darasa la kwanza kwenye ile shule kila term nilikuwa nashika nafasi ya kwanza bila kujali magumu niliyokuwa napitia, alikuwa hapendi maana hata daftari na kalamu alikuwa hanunui natafuta ya watoto wake ambayo hayakuisha nachana kulikotumika natumia. Nilipomaliza darasa la saba nilifaulu mwenyewe kwenye ile shule nikapangiwa shule ya day kama kilomita 3 kutoka kwake hivyo niliendelea kukaa pale, (yule mwanae nae alifaulu hii shule ila alipekewa private). Maisha ya secondary yakanza hali ilikuwa mbaya zaidi kazi ngumu, hakuna huduma yyte hata daftari hanunui nakumbuka nilisoma miaka miwili bila sweta ya shule na ni mikoa yenye baridi mpaka baba yangu akajikusanya akaninunulia. Hakutaka nisome kabisa maana hata akikuta nimewasha taa alikuwa anazima akidai namaliza umeme, hivyo nilikuwa na taa yangu wakishalala naamka taratibu naenda barazani naiwasha naanza kusoma kipindi cha mitihani, sikuwa nikifanya vizuri nilikuwa nashika nafasi ya 9-15 kati ya wanafunzi 150, ila i was better that that. Nilikuwa napenda sana kuwa mwanasheria, wakati wote niliwaza kama ningekuwa mwanasheria ningeshulikia watoto wanaopitia mazingira magumu kama yangu, Nilimaliza kidato cha nne nikapata division three bahati nzuri nikapangiwa shule ya A-level govt nikaondoka kwake,
Kipindi hicho dada alikuwa kidogo ameshajitegemea na ada ilikuwa elfu 70 hivyo alinisaidia na vitu vingine vidogo na baba yangu alinisaidia, (nikiwa darasa la saba mama na baba walitengana). Baada ya kwenda A-level yani nilirelax imagine nilinenepa mpaka nikafikisha kg 80:p, yani nilikuwa sisomi, wastani mimi ilikuwa ni 98, nikifika 90 hapo nimefeli, wenzangu walinishangaa, nilikuwa naongoza kuanzia kata mpaka mkoa, kozi zote mimi ndio nilikuwa naongoza kwa wastani, kila term nilipewa zawadi, Nilimaliza ile shule na kuzawadiwa kuwa mwanafunzi bora.(nilijua kumbe kule nilikuwa ninafeli kwa sababu ya hali ya maisha) Nilifaulu kwenda chuo kikuu ingawa sikusoma kozi ile niliyokuwa naipenda ila maisha yalisonga. Nilimaliza niko mtaani sasa nimeajiriwa ila i know Im more than this naona wananichelewesha.. Nina imani nina akili sana kiasi kwamba sijawahi kutumia hata 1% ya akili niliyonayo. Shangazi sasa ndio amekuwa anajifanya ananipenda kuliko wanae wote, Yule mwanae aliyekuwa anadekezwa mpaka leo ana reseat!!


NB 1. Kuna watoto wanafeli sio kwa sababu hawana akili ila wanakosa malezi bora/huduma na motivation

2. Kuna watu wanafanya kazi fulani sio kwa sababu wanaipenda ni kwa sababu nature ili waforce wawe hivyo.

3. Kuna watu wapo kwenye nafasi fulani sio sababu ya uwezo wao ila nature ya maisha/exposure nk.

4.Tusiwaamini ndugu zetu katika malezi ya watoto hata kama ni ndugu wa damu.
 
Pole kwa mateso ya Shangazi lakini hongera kwa kusoma na kutimiza ndoto yako. Kuna mahali niliwahi kusoma " You CAN turn Challenges into opportunities in life"
 
Pole kwa mateso ya Shangazi lakini hongera kwa kusoma na kutimiza ndoto yako. Kuna mahali niliwahi kusoma " You CAN turn Challenges into opportunities in life"

Asante!
Malengo nimetimiza ila sio kwa kiwago cha kuridhisha but i can still do better.
 
Ni kweli baadhi ya ndugu hwapendi kuona ndugu akifanikiwa, hongera kwa kutokata tamaa maana hilo tu ndio limeweza kukufanya uwe ulivyo hata kama una amini ulivyo sivyo ulivyotaka ila amini pengine ungekuwa ulivyokuwa unatamani kuwa usingekuwa na amani, mshukuru Mungu kwa jinsi ulivyo sasa.
 
Ni kweli baadhi ya ndugu hwapendi kuona ndugu akifanikiwa, hongera kwa kutokata tamaa maana hilo tu ndio limeweza kukufanya uwe ulivyo hata kama una amini ulivyo sivyo ulivyotaka ila amini pengine ungekuwa ulivyokuwa unatamani kuwa usingekuwa na amani, mshukuru Mungu kwa jinsi ulivyo sasa.

Asante mkuu.
 
Back
Top Bottom