Je, Hili ni gazeti la Taifa au Chama ?

Ndesaika

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
219
92
1458619292085.jpg
Mimi nashindwa kuelewa uandishi huu katika Gazeti la Taifa. !
1458619292085.jpg
 
Nadhani taarifa kama hii ingevutia zaidi kama ingeandikwa na gazeti la mzalendo au uhuru! hapo tusingeshangaa. Kwa habari leo! wamekengeuka bila shaka.

Kwanza hakuna mtu wa kuizika CUF zanzibar.Huo ndio ukweli ulio wazi hasa kule Pemba na hakuna jambo ambalo wazanzibari wamefanikiwa kama suala hili la kuwa na vyama viwili vikubwa vya kisiasa huku vilivyobakia vikisindikiza tu.

Changamoto kubwa ni chama tawala kutokua tayari kuruhusu na wapinzani kuongoza nchi. Natamani na huku Tanzania bara siku moja tuwe na vyama viwili vikubwa kama ilivyo marekani. Mkichoka itikadi za chama hiki mnachagua chama mbadala huku demokarasia ikiheshimiwa na utaifa ukitangulizwa mbele badala ya masilahi ya chama fulani na watu wachache tu kwenye jamii wanaojiona wao ndio pekee wenye haki ya kuwatawala wengine.
 
Itachukua muda mrefu kufika huko ni mpaka apatikane raisi ambaye ni mzalendo kweli kweli ndo tutaweza kufika huki
 
THAT IS PARTY SUPREMACY, usualy it plant the seed of its decline, let us wait the their destiny
 
Nadhani taarifa kama hii ingevutia zaidi kama ingeandikwa na gazeti la mzalendo au uhuru! hapo tusingeshangaa. Kwa habari leo! wamekengeuka bila shaka.

Kwanza hakuna mtu wa kuizika CUF zanzibar.Huo ndio ukweli ulio wazi hasa kule Pemba na hakuna jambo ambalo wazanzibari wamefanikiwa kama suala hili la kuwa na vyama viwili vikubwa vya kisiasa huku vilivyobakia vikisindikiza tu.

Changamoto kubwa ni chama tawala kutokua tayari kuruhusu na wapinzani kuongoza nchi. Natamani na huku Tanzania bara siku moja tuwe na vyama viwili vikubwa kama ilivyo marekani. Mkichoka itikadi za chama hiki mnachagua chama mbadala huku demokarasia ikiheshimiwa na utaifa ukitangulizwa mbele badala ya masilahi ya chama fulani na watu wachache tu kwenye jamii wanaojiona wao ndio pekee wenye haki ya kuwatawala wengine.
Kwani kuna tofauti gani kati ya Taifa Leo na Mzalendo. Waandishi wanatafuta U-DC wewe!
 
Sioni cha kushangaza hapo,vyote vya UMMA vimekuwa vya CCM na hata viwanja vya michezo wamejimilikisha.
 
Kwa namna akili za waafrika zilivyo nashawishika kusema sisi waafrika ndo tulimsulubisha yesu kristo msalabani huu sio uroho wa madaraka ni laana juu ya madaraka.
 
eti hilo ni gazeti linalotakiwa lijiendeshe kibiashara! huyo mhariri inaelekea hajui kuwa pesa za kodi za watanzania wote bila kujali itikadi za vyama ndizo zinazogharamia gazeti hilo. ndio yale yale ya tbc kuonyesha 'live' harusi.
 
Ndio maana waandishi kama hawa wanapotumbuliwa majipu wanahangaika sana kupata kazi
 
Hawa watakuwa kama gazeti la uhuru, mtaani kwetu huletwa nakala tatu na siku nyingine nakala mbili au moja hubaki haijauzwa
 
Back
Top Bottom