PostGE2025 Je hili kundi linaloondoka sasa kutoka Dar kwenda mikoa mingine, ni hofu ya maandamano au? Je, vipi kuhusu huko waendako?

PostGE2025 Je hili kundi linaloondoka sasa kutoka Dar kwenda mikoa mingine, ni hofu ya maandamano au? Je, vipi kuhusu huko waendako?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Wakuu

Nimeona taarifa juwa hali ya usafiri Dar kwenda mikoani imekuwa changamoto, wasafiri ni wengi kuliko mabasi.

Je kuna tetesi zozote za magari kutokusafiri ikikaribia Disemba 9? Ama wananchi tu wamekuwa na hofu?

===

Hali ya usafiri katika eneo la Shekilango jijini Dar es Salaam imekuwa changamoto huku idadi ya abiria wanaosaka safari za kwenda mikoani ikiongezeka mapema kuliko ilivyozoeleka miaka ya nyuma.

Kwa kawaida, misururu ya abiria huanzia Desemba 20 kuelekea Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Hata hivyo, safari hii msongamano huo umejitokeza mapema, jambo lililowashangaza hata wasafirishaji wa magari ya mikoani.

Katika eneo hilo maarufu kwa vituo vidogo vya mabasi na ofisi za makampuni ya usafirishaji, hali ya hekaheka imetawala, kuanzia asubuhi ya leo Jumatano, Desemba 3, 2025 huku foleni za abiria na magari zikisababisha usumbufu na kukwamisha huduma za usafiri.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwananchi wamekiri awali walipanga kusafiri baadaye, lakini wameamua kuondoka mapema kufuatia tetesi za mitandaoni kuhusu yanayohofiwa yanaweza kutokea Desemba 9.

Hivyo wamesema hawataki kuhatarisha safari zao au kuhofia kukosa usafiri endapo hali ya usalama itabadilika. Wengine wamedai taarifa zinazosambaa mtandaoni zimeongeza presha na kuwalazimu kutafuta usafiri mapema.

Hadi saa 5 asubuhi, uwingi wa abiria Shekilango umeongeza shinikizo kwa watoa huduma za usafirishaji, huku wamiliki wa magari wakilazimika kuongeza safari ili kukidhi mahitaji jambo wanalofurahia kwa kuwa wanaongeza kipato
1764757538958.png

Source Mwananchi Digital
 
😂hueshimu mamlaka?
Hapana unajua currently huu msemo wa Guys guys guys una trend sanaa.

Of course na safari ya kwenda mkoani near/ soon ila napata mashaka maana ni kilometer 1000 iviii..
Sasa sijajua kwa usafiri wa ardhini which transport itakua more economical..
Hofu pia usije kukutana na Chao's ama riot's za 9D
Safari yangu ni muhimu sana sanaa sanaa
 
Hapana unajua currently huu msemo wa Guys guys guys una trend sanaa.

Of course na safari ya kwenda mkoani near/ soon ila napata mashaka maana ni kilometer 1000 iviii..
Sasa sijajua kwa usafiri wa ardhini which transport itakua more economical..
Hofu pia usije kukutana na Chao's ama riot's za 9D
Safari yangu ni muhimu sana sanaa sanaa
Ni vema uka move mapema, mkuu
 
Kuna dogo yupo arusha ana familia anasema hana hamu ya kubak arusha yaan kwa vyovyote vile lazima asafir kabla ya 9d maana maisha ya 29mo yalikuwa hatar
 
Atakwenda wapi sasa mkuu? Au yale maeneo ambayo yalikuwa down kama vile Moro?
Mwanza vijijin,kawaambia kwao wauze hata mifugo ili arudi au yeye huko arusha atafanya namna yoyote aondoke kabla ya 9d,inavyoonekana 29mo ile curfew ilimfanya vibaya dogo hana hamu nayo tena
 
Back
Top Bottom