- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Madai
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa na kipande cha video chenye Sauti inayodaiwa kuwa no ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokradia na Maendeleo yet(CHADEMA) na mwanaharakati Maria Sarungi wakijadili namna ya kumficha aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa Video hiyo inayosambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ni ya kughushi ambayo imetengezwa na wapotoshaji.
Sehemu ya sauti ya Maria Sarungi inayosikika katika video hiyo ni kutoka katika Space aliyoifanya Oktoba 9, 2025 kupitia mtandao wa X wakiongolea kuhus mada hiyo ya Polepole ambayo imechukuliwa na kuunganishwa sauti ya kughushi inayodaiwa kuwa ni Ya John Heche.
Aidha ufutailiaji kupitia maneno muhimu umebaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishwa na Clouds Tv na badala yake wapotoshaji walitumi grafiki ya chanzo hicho kwa ajili ya kupotosha