Je hii ni haki kutokea kwenye mitihani ya taifa?

atenedius

New Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
3
Reaction score
1
Hii imetokea jana tar.11/11/2019 wakati wa mtihani wa taifa wa kidato cha nne ktk shule moja ya sekondari Wilayani Karagwe Kagera.
Wadau saidia na naomba maoni katika hili:
Wanafunzi wa kidato cha nne jana walibainika kuwa nje ya eneo la shule takribani nusu kilomita kutoka shuleni wakiwa wametoka chumba cha mtihani kwa ajiri ya kufanya usafi wa miili yao na kurefresh kwasababu ya uchovu wa kukesha usiku wakisoma. Walikaa takribani dakika 30 tu na kurejea shuleni hapo. Baada ya kufika shuleni uongozi wa shule uliwapa adhabu km ifuatavy
o:

1. Kutokula siku hiyo.
2. Kufanya mitihani inayofuata wakiwa nje ya mazingira ya shule.

3.Wamezuiliwa kujaza "Self forms" kwasababu hawajajenga uzio.
4. Kujenga uzio kwa gharama ya Tshs 120,000 kila mmoja hali ikijulikana shule haina uzio.

Jambo la kusikitisha ni kuwa shule haijawai kujenga hata hatua moja ya uzio na eneo la shule ni km ekari ishirini hivi.
Ninajiuliza Je, ni haki watoto kupewa adhabu ya ujenzi wa uzio hali haupo?
Je, haitasababisha wanafunzi wengine kuonewa kisa eti shule ipate pesa ya kujengauzio? na Je hii si kujipatia pesa kwa udanganyifu?
Je, wazazi watapata wapi pesa za haraka zilipwe ili wanafunzi waweze kujaza "self forms" hizo?,
Je, haitakatisha tamaa wazazi wengine tamaa kupeleka watoto shule hiyo? , Je mkuu wa shule kwa kufanya hivyo anadhani atazungushia uzio eneo lote la shule? Je, hii haiwezi kuathiri watoto kupata stress hata kutofaulu vema mtihani wao?
Tafadhali wadau naomba maoni yenu ili nipate majibu halisi ya sera na sheria ya elimu Tanzania na NECTA.
 
hao vijana ni wapumbavu kama alivyo mleta hoja.

walienda nje dk 30 kuganya nini?

waache ujinga
 
Kila shule inataratibu zake za namna ya kutoka eneo la shule. Naomba kwanza kujua endapo walifuata taratibu na sheria za shule walipokua "wanaenda kufanya usafi na kurefresh"

Sijajua unalalamikia ukubwa wa adhabu au unaona wameonewa bila sababu?
 
Ungetaja na jina la shule ili jambo lako lipate kushughulikiwa na wahusika.
 
Hii imetokea jana tar.11/11/2019 wakati wa mtihani wa taifa wa kidato cha nne ktk shule moja ya sekondari Wilayani Karagwe Kagera.
Wadau saidia na naomba maoni katika hili:
Wanafunzi wa kidato cha nne jana walibainika kuwa nje ya eneo la shule takribani nusu kilomita kutoka shuleni wakiwa wametoka chumba cha mtihani kwa ajiri ya kufanya usafi wa miili yao na kurefresh kwasababu ya uchovu wa kukesha usiku wakisoma. Walikaa takribani dakika 30 tu na kurejea shuleni hapo. Baada ya kufika shuleni uongozi wa shule uliwapa adhabu km ifuatavy
o:

1. Kutokula siku hiyo.
2. Kufanya mitihani inayofuata wakiwa nje ya mazingira ya shule.

3.Wamezuiliwa kujaza "Self forms" kwasababu hawajajenga uzio.
4. Kujenga uzio kwa gharama ya Tshs 120,000 kila mmoja hali ikijulikana shule haina uzio.

Jambo la kusikitisha ni kuwa shule haijawai kujenga hata hatua moja ya uzio na eneo la shule ni km ekari ishirini hivi.
Ninajiuliza Je, ni haki watoto kupewa adhabu ya ujenzi wa uzio hali haupo?
Je, haitasababisha wanafunzi wengine kuonewa kisa eti shule ipate pesa ya kujengauzio? na Je hii si kujipatia pesa kwa udanganyifu?
Je, wazazi watapata wapi pesa za haraka zilipwe ili wanafunzi waweze kujaza "self forms" hizo?,
Je, haitakatisha tamaa wazazi wengine tamaa kupeleka watoto shule hiyo? , Je mkuu wa shule kwa kufanya hivyo anadhani atazungushia uzio eneo lote la shule? Je, hii haiwezi kuathiri watoto kupata stress hata kutofaulu vema mtihani wao?
Tafadhali wadau naomba maoni yenu ili nipate majibu halisi ya sera na sheria ya elimu Tanzania na NECTA.
Ndugu,
Kama wewe ni mzazi basi una tatizo na wewe ndiye chanzo cha mwanao kutoroka shule. Anapata wapi ujasiri wa kurefresh badala ya kuwazia mitihani.

Badilika ili upate uwezo wa kumsaidia mwanao. Otherwise utampoteza mazima.
Byeeeeeee
 
Ungetaja na jina la shule ili jambo lako lipate kushughulikiwa na wahusika.
JINA LA SHULE: KAJUNGUTI SECONDARY SCHOOL IPO WILAYA YA KARAGWE MKOANI KAGERA.
Naomba kueleweka nazungumzia ukubwa wa adhabu na kutosikiliza maoni wazazi baada ya kuitwa.
 
Naomba kueleweka wadau sijakataa adhabu kutolewa lakini hapa suala ni ukubwa wa adhabu na jinsi ilivyotolewa kwa watahiniwa. Kwanza zingatia shule haina uzio halafu kuambiwa uujenge je, si uonevu huo?
pili walioitwa wazazi hawakupewa nafasi kusikilizwa maoni yao isipokuwa kuambiwa fuata maelekezo ya uongozi wa shule,
tatu muda wao wa kukaa shule ulikuwa unamalizika maana ilikuwa imebaki one day wote kuhitimu
 
Madogo washatiwa kiwewe wanaweza kuwa na matokeo mabovu.

Ushauri wangu, nenda kachape mkono kuanzia mkuu wa shule hadi PS ukimaliza panda basi nenda Kankonko Kigoma au Kisiwani sanasana vilivyoko Sengerema huko utakaa zako majini upendavyo hakuna atakaye kupata baada ya miezi miwili rudi.

Zingatia sana kutembeza mkono wa maana
 
Safi sana mkuu, hapa umenena, akili kama hizi ndio zinatakiwa Tanzania hii
 
Back
Top Bottom