Je hii kesi ntaishinda?, Ushauri wenu

Je hii kesi ntaishinda?, Ushauri wenu

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
460
Reaction score
360
Kuna jirani angu tarehe 22.03.katika maelezo yake alidai mnamo mda wa saa saba usiku alikuwa ameweka simu 2 na computer juu ya meza karibu na dirisha.
Kipindi amelala aliskia watu wanagusa kitasa cha mlango wake.
Mara akaskia kama upepo unapuliza na dirisha kufunguka (dirisha ni la nyavu na nondo linafungiwa ndani) basi ndipo alipoona watu wakichukua simu na baadae wakibeba na computer mezani.

Katika maelezo yake hayo anadai alivyokuja kuchungulia kwenye tundu la dirisha akanitambua mimi kwa mbali tukiwa tunakimbia na mali yake. Akarudi kulala na kuamka saa 1:30 asubuhi huku akidai amemuona aliyemuibia na kwenda kuripoti chuo na baadae polisi
Juzi kanipeleka polisi na kuniweka maabusu.

Kwa upande wangu sikufanya tukio hilo na wala sina tabia ya wizi ila nilichokigundua ni kuwa kwa kuwa mimi najiweza kifedha angalau kidogo ninaweza kumlipa kirahisi.
Kesho tunapanda mahakamani kujibu mashitaka nami kama ushindi nauona njenje.

Ushauri wenu juu ya maswali ntakayomuuliza ashindwe kuyajibu maana yeye mwenyewe hajiamini na ukweli anajua sio mimi ila tu anataka alipwe.
 
Tafuta mwanasheria akusaidia na baada ya kushinda kesi mshitaki akulipe faini kwa kukupotezea muda na kukudhalilisha.
Mpige km milion 50 hivi ili siku nyingine ajue nn anapaswa kufanya na siyo kumshitaki kila mtu.
Ukimlipa atajua ww ni mwizi na mtaani vitu vikiibiwa utakuwa muhanga ni ww. Hiyo hela ya kumlipa mpe mwanasheria.
Watu mnachezea nafasi sana. Hizo nafasi ndizo za kupiga hela. Make money hata km upo mahabusu.
Show him no mercy
 
Muulize kwa niaba ya maelezo yake alipokuwa analala alikuwa anasikia watu wanagusa kitasa cha mlango wake kuingia na kuiba hivyo vitu.

Kwa nini muda wote huo hadi vitu vinaibwa asingeamka na kumkamata mwizi wake bali alisubiria mpaka waondoke ?

Pili alifanya jitihada zozote za kupiga kelele ata za wizi ili majirani walio karibu waamke na kumsaidia ina maana kwa hali yoyote ile wewe kama jirani yake wa karibu lazima ungekuwa miongoni mwa watakaoamka na kutoa msaada na kama haukuwepo wakati huo ndio hakuhisi na kuuliza ulikuwa wapi wakati anaibiwa.?.


Kuna maswali mengi tu mengine watakuja nayo wengine.
 
Ukikubali kumlipa hata kama una uwezo ina maana uko guilty, kesi itakugeukia. Je una shahidi wa kueleza ulikuwa naye wakati wa tukio (mke? mtu mnayeishi naye?)
 
Kesi rahisi sana hiyo.
Huyo jirani yako baada ya kukugundua wewe usiku huo alienda kutoa taarifa kwa viongoz wa mtaa ili kuja kukufuata kwako mda huo huo? Kama hakufanya hivyo kesi imeshaisha na umeshinda.
 
Huyo mpe sumu baada ya kesi atakusumbua baadaye.... [emoji4]
 
Kesi zinapoteza Mda lakin kwa kuwa kapenda kukuzalilisha we nenda mahakamani ...umshinde..maana hakuna kizibiti ulichokamatwa nacho...chochote.

baada ya hapo umlipishe Fidia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom