Je, hii kauli ina ukweli kwa Tanzania?

Je, hii kauli ina ukweli kwa Tanzania?

Joined
Nov 5, 2025
Posts
81
Reaction score
130
"This battle is going on everywhere on the continent, if not the whole earth. Tanzanians have just realised they were behind. It's the Tanzanians who maintained a rotten system and are responsible for this mess, not CCM. Tanzanians, in general, were not significantly affected by the fall of the Berlin Wall.

Nyerere saw the impact and quickly allowed the changes, but the population in general didn't see the need for the change and did not demand accountability from CCM. Observe the changes that have occurred in the regions of Kenya, Malawi, Botswana, and others.

In most African countries, the general population changed in the early 90s. We had these riots in *** in the late 80s. We watched the Tinamen Square demos in China live on CNN. Tanzanians in general were not affected by this until recently. Welcome to the club.

In Africa, military coups were the order of the day, but are rare now. Why? Because Africa has grown. They hold their leaders accountable. Tanzania should do the same henceforth, not allow the constitutions that we have now in this age!"

swahili
"Mapambano haya yanaendelea kila mahali barani, kama siyo duniani kote. Watanzania ndiyo wamegundua tu kwamba walikuwa wameachwa nyuma. Ni Watanzania ndio waliodumisha mfumo uliooza na wanawajibika kwa hali hii yote, siyo CCM. Kwa ujumla, Watanzania hawakuathiriwa na kuanguka kwa Ukuta wa Berlin.

Nyerere aliona athari zake na kuruhusu mabadiliko haraka, lakini wananchi kwa ujumla hawakuona umuhimu wa mabadiliko wala hawakudai uwajibikaji kutoka kwa CCM. Angalia mabadiliko yaliyotokea katika eneo hili—Kenya, Malawi, Botswana, n.k".

Katika nchi nyingi za Afrika, wananchi kwa ujumla walibadilika mapema miaka ya 90. Tuliwahi kuwa na maandamano haya huku *** mwishoni mwa miaka ya 80. Tuliangalia moja kwa moja maandamano ya Uwanja wa Tiananmen nchini China kupitia CNN. Watanzania kwa ujumla hawakuathiriwa na mambo haya hadi hivi karibuni. Karibuni kwenye klabu.

Afrika, mapinduzi ya kijeshi yalikuwa jambo la kawaida, lakini sasa ni nadra. Kwa nini? Kwa sababu Afrika imekua. Wanachi wanawawajibisha viongozi wao. Tanzania inapaswa kufanya vivyo hivyo kuanzia sasa, na isikubali kuwa na katiba hii tulionayo sasa katika zama hizi!”
 
Back
Top Bottom