Je, hii dhana ya “Usawa wa Kijinsia” tumeielewa kweli?

Guus

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
1,130
823
Binafsi huwa natatizika sana kila ninapoitafari dhana ya Usawa wa Kijinsia. Sijawahi kuipinga na wala sitokuja kuipinga kama inamlengo wa kufikisha usawa katika upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kwa makundi haya mawili (Ke na Me). Na kwa vile taswira kubwa (kama sio yote) iliyo ndani ya dhana hii kwa makundi haya mawili hujionesha kupitia maisha ya ndoa, nami nitaitumia ndoa kwa kiasi kikubwa katika tafakuri yangu. Kwa hiyo sipati shida kuielewa dhana hii katika upatikanaji wa huduma za jamii na uchumi kama nilivyosema awali, lakini pia katika kuondoa unyanyasaji wa mmoja wa wanandoa kutoka kwa mwingine kwa kigezo cha jinsia.

Kinachonitatiza ni namna tunavyojaribu kuiishi hii dhana hii. Kwa mtazamo wangu, wengi (kama sio wote) tunachukia unyanyasaji wa kijinsia. Lakini Je, ni namna gani tunatasfiri ukosefu wa Usawa wa Kijinsia katika majukumu yetu ya kifamilia? (1) Labda tuifikirie jamii ambayo mila zinaelekeza kuwa baba ndiye mwenye jukumu la kuigharamia familia (ambapo kama familia inakaa katika makazi duni, mtoto akiwa na utapiamlo, asipopelekwa shule, akiwa na mavazi chakavu, nk fedheha humuangukia baba). Katika jamii ya namna hii, wazazi wanapokuwa pamoja na mama akamueleza baba kuhusu ada ya shule, nk, Je hapa nako kuna upungufu wa usawa wa kijinsia? Na vipi kama jamii hiyo mama anajulikana kuwa ni mlezi wa nyumba yake (yaani jamii humbebesha lawama kwa hali ya usafi wa watu wake, nk), halafu baba akamtaka mama akasafishe vyombo, Je hapa napo pana upungufu wa usawa wa kijinsia? (2) Hebu tuifikirie jamii inayokinzana na ya awali. Jamii ambayo familia inapokuwa katika lishe na makazi duni, fedheya anayoipata mama ni sawa na vile baba anavyotafsiriwa. Na pia, watu wa familia na nyumba kwa ujumla inapokuwa katika mazingira ya kutovutia, vilevile fedheha anayoipata baba ni sawa na ile anayokumbana nayo mkewe. Katika jamii hii baba akikaa kumuachia mama asafishe vyombo, Je kuna upungufu wa usawa wa kijinsia? Na vipi mama akidai ada ya shule ya mtoto kwa baba? Nimeweka hizo sehemu mbili (1 na 2) ili kujaribu kukielezea kile kinachoonekana sana kwa sasa. Kinachodhaniwa ni upundufu wa usawa wa kijinsia katika ndoa kwa sasa umejikita katika kuzilazimisha jamii, pasi kuzingatia mila, kuondokana na taratibu zilizoweka majukumu ya kijinsia. Leo hii tunalazimishana kuamini kuwa katika ile jamii ya kwanza (1) kuwa mama naye ni lazima alipe ada ya shule ya mtoto/kodi ya nyumba/alishe familia/nk ili ionekane ni usawa wa kijinsia. Vilevile baba naye ni lazima aoshe vyombo/afue nguo/apike/nk. Ya kwamba mmoja asipofanya hivyo inatafsiriwa ni ukosefu wa usawa wa kijinsia. Sisemi kuwa tusifanye hayo majukumu kabisa, la hasha, tuweze kufanya lakini upande wa pili ni wazi una wajibu wa kuelewa kuwa ni msaada kutoka kwa mwenza wake. Mimi naamini kuna umuhimu wa kufuata majukumu ya “kijinsia” yaliyotokana na mila, na pale yanapofuatwa ndipo tuite “usawa wa kijinsia”, badala ya kulazimisha mila ya jamii nyingine na mgawanyo wao wa majukumu utueleze nini maana ya “usawa wa kijinsia”. Mfano kwa jamii ile ya kwanza usawa wa kijinsia ni pale baba asipoleta mushkeri katika kuigharamia familia na mama asipomgomea mumewe kufua nguo/nk. Hata Christine de Pizan (mmoja wa waanzilishi wa kwanza wa dhana ya usawa wa kijinsia) hakutaka tuibebe dhana yake nje ya mila za jamii husika. Kiuhalisia kupingana na mgawanyo wa majukumu uliowekwa na mila ndiyo kutoka nje ya usawa wa kijinsia. Bahati nzuri hakuna mahala wale jamaa wa “Magharibi” wametueleza kuwa mgawanyo wa majukumu uliowekwa na mila fulani si usawa wa kijinsia. Hivyo binafsi naamini pamoja na kuwa usawa wa kijinsia ni hitaji la wengi (kama sio wote), mapokeo yake hayajawa sawa na hatimaye kuleta shida. Na hili linaweza kuwa ni sababu kubwa inayofanya ndoa nyingi za zama hizi ziwe na migogoro endelevu, huku sehemu kubwa ya malalamiko ikiwa “ukosefu wa heshima” kwa upande fulani wa ndoa. Laiti tungetasfiri usawa wa kijinsia katika kutekeleza majukumu ya kifamilia kwa kufuata mgawanyo wa majukumu chini ya mila zetu, nyufa nyingi za ndoa zisingekuwapo. Kwa kutotaka kutasfiri usawa wa kijinsia katika kutekeleza majukumu ya familia kwa kufuata mgawanyo wa kazi uliowekwa na mila zetu, ni wazi tunapoteza urahisi wa kuyatumia yale maneno mawili muhimu (samahani na ahsante) ya kwenye ndoa yana. Na bahati mbaya sio hili tu, ni mengi mazuri tunayoyapokea, lakini tunayapokea na mitizamo yao ya ki-Magharibi na kushindwa kuyapa uhalisia wa maisha yetu, hatimaye tunajikuta tukibomoa kuliko kujenga. Tchaoo!!
 
Guus. Wamama wa Kiafrika wameubeba Ufeminist pasi na kujua lengo lao kwa nchi zetu. Ndoa nyingi ziko vitani japo wanaume wana akili sana juu ya hili.
 
Mada nzuri kama hizi zinazohitaji kufikiri kwa kina, hekima na busara hazinaga wachangiaji. Na wakiwepo wachangiaji ghafla yanaanza matusi, kebehi na kashfa.

Back to topic.
Usawa wa kijinsia unatafsiriwa tofauti sana. Mila, desturi, mapokeo na maandiko matakatifu yanasiginwa kwa kitu kinaitwa usawa wa kijinsia. Tukiachana na mila na desturi ambazo zinatoa mgawanyo wa kazi pamoja na majukumu mengine ya familia kwa mwanamke na mwanamme vizuri kabisa na mgawanyo ukaendana na mazingira husika ya sehemu hiyo jamii ilipo na tukarudi kwenye maandiko, kuna migogoro mingi ingefutika kwenye familia.

Nitanukuu waefeso 5:21-30
"21 Kila mmoja wenu ajinyenyekeze kwa mwenzake kwa sababu ya upendo mlio nao kwa Kristo. 22 Wake, watiini waume zenu kama mnavyomtii Bwana.23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo ni mwili wake, naye mwe nyewe ni Mwokozi wa kanisa.24 Basi, kama vile Kanisa linavyom tii Kristo, vivyo hivyo na wake pia wanapaswa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili 26 alitakase. Alifanya hivyo kwa kuliosha kwa maji na kwa neno lake 27 ili ajipatie kanisa linalong’aa, lisilo na doa wala kunjamano wala kitu kingine cho chote kama hicho; liwe takatifu na bila kasoro. 28 Vivyo hivyo waume wawapende wake zao kama miili yao. Anayempenda mkewe anajipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza kanisa lake. 30 Sisi tu viungo vya mwili wake."

Hapo juu maandiko yapo wazi wazi kabisa, wanawake wawatii waume zao kwa kila jambo. Siku hizi utii wa mke kwa mume umegeuzwa jina na kuwa utumwa. Na hapo ndipo msingi wa migogoro inapoanza na tafsiri ya usawa wa kijinsia inakuzwa na kufubaza msingi mkuu wa familia ambao ni utii na upendo. Kama jamii ingeendelea kusimamia usawa wa kijinsia at the same time ikawa haiachi misingi hii mikuu kusingekuwa na migogoro mingi ya familia, maana kila upande ungekuwa unakumbuka majukumu yake. Sababu kubwa ya Usawa wa kijinsia ni kutaka kumtoa mwanamke kutoka kwenye miliki/himaya ya mwanaume na kumfanya mtu huru. Sio jambo baya kumfanya mwanamke awe huru ila pia sio jambo zuri kumtoa kutoka kwenye kumtii mwanamme.
 
Bila kubadilisha sheria tulizo nazo hakutakuwa na hicho wanachoita haki sawa.mfano mtoto anatakiwa kupata matunzo na ada zote kutoka kwa baba je mama usawa wake huko wapi?
 
Back
Top Bottom