Je, hawa wanaweza kuoana?

loyda

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2014
Posts
436
Reaction score
128
Habari zenu wakuu,

Hapa nina wakati mgumu kidogo, nina rafiki yangu tumeshibana sana kaniomba ushauri.Ni hivi kuna jamaa mmoja kamuaproch baada ya huyo jamaa kufiwa na mkewe kama miezi miwili iliyopita.

Kabla mkewe hajafariki huyu rafiki yangu na jamaa walikuwa wakifahamiana kutokana na mdogo wa jamaa kuwa na mahusiano na shost wangu kipindi cha nyuma lakini walikuja kuachana.

Baada ya mdogo mtu kuachana ikabaki kama undugu coz huyo mdogo wa jamaa alimtambulisha huyu shost kwa kaka yake so walipoachana pia wakawa wanajaliana kama ndugu.

Hata siku ya msiba wa mkewe jamaa shost yangu alienda kwa ajili ya huyo x wake japo hawana tena mahusiano kimbembe kimekuja kaka mtu anataka kuweka shemejie ndani (siyo mdogo wake wa tumbo moja ni mtoto wa baba mdogo)

Hii kiutamaduni wetu imekaaje wapendwa
 
Mbona hiyo sio shida jamaa anao uwezo wa kuvuta jiko tuu haina bwai hiyo mambo
 
'Green Light' ila kwanza wacheki afya then waendelee.. Ujaluoni ni kama daily bread,kule wanaoa hata mtu na mdogo wake wa tumbo moja..
 
Hata angekuwa wa tumbo moja kama wana watoto aowe tu ili kuwe na uchungu wa kweli kwa watoto wa marehemu
 
Duh, mi sijaelewa kabisaa, bora nijiweke pembeni kuepuka msongamano.
 
mbona mwingine anaoa kabisa mdogo mtu wa tumbo moja!
najua kwama wa4 hivi waliolewa na mme wa dada mtu baada ya kufariki
 
Hii story watu wanaichangia tofauti au mimi sijaielewa vizuri.

Fafanua, shemeji yake kivipi?

Au unamaanisha aliyekuwa dem wa mdogo wake?

Au huyo dada ni mdogo wa marehemu?
 
Duh, mi sijaelewa kabisaa, bora nijiweke pembeni kuepuka msongamano.

Wewe umeelewa vizuri, sema wachangiaji ndo wanakuchanganya!

Alitaka kumaanisha mtu kuoa x wa mdogo wake, na sio shemeji kama wachangiaji baadhi walivyoelewa. Hapa kuna wanaodhani huyo ni mdogo wa marehem.
 
Ruksa tu hakuna shida ndo kwanza atawatunza vizuri watoto wa dada ake kuliko kuleta mtu ambae hana uhusiano na marehemu
 
Wewe umeelewa vizuri, sema wachangiaji ndo wanakuchanganya!

Alitaka kumaanisha mtu kuoa x wa mdogo wake, na sio shemeji kama wachangiaji baadhi walivyoelewa. Hapa kuna wanaodhani huyo ni mdogo wa marehem.

Nae ameandika kama kiswahili sio maza tangi bana
 
Mimi nakuwa wa pili ambaye sijaambulia kitu hapo.

Heading na content ni tofauti,

- Heading inasema mdogo wa marehem
- Content inasema aliyekuwa dem wa mdogo wake mfiwa

Madawa yamechanganywa changanywa hapa.
 
mi nikasomaaaaaaaaaaaaaaa nikaone sielewi, nimemwomba aweke picha:yo:
 
Duh, mi sijaelewa kabisaa, bora nijiweke pembeni kuepuka msongamano.

Kweli kabisa ameandika utadhani kakurupushwa, inabidi urudie kusoma hadi uelewe. Lakini kwa vile kichwa kinaeleweka we changia tu, kwa mtazamo wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…