Je hawa viongozi utawakumbuka kwa lipi? Liwe jema au baya!

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
Wana Jf,
Hawa viongozi utawakumbuka kwa lipi?
1. J.K. Nyerere;
-nitamkumbuka kwa kuachia umoja wa Watanzania
-kututunzia rasilimali zetu hasa madini,nk.
-kuona thamani ya Watanzania na kuishi maisha kama ya walio wengi.
-Aliwathamini sana wananchi wake.

2. A.H.Mwinyi;
-alitupa uwezo wa kujua yanayoendelea nchi zingine kwa kuruhusu vitu vingi nchini
-ni mtu wa watu asiye na makuu na mtu
-Hakuwa na uwezo wa kujua ni uhuru kiasi gani angetoa ktk sekta ya Uchumi.

3. B.W.MKAPA;
-Aliiwezea uchumi kwani pesa yetu ilikuwa na thamani, hivyo wananchi wengi walinufaika.
-Atleast alikuwa na uelewa nini maana ya uongozi .
-pia alikuwa na vision ya kutaka kupeleka nchi sehemu fulani.
-alijitahidi kuhimarisha miundo mbinu kama barabara na madaraja.
-ALIANZA UFISADI mara tu baada ya kifo cha Mwl. Nyerere.
-alikuwa mtu wa kwanza kufanya biashara binafsi IKULU, na kugeuza IKULU kuwa ofisi za biashara zake.
-Hakika alituibia sana hasa kipindi chake cha mwisho, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2005.

4. J.M. Kikwete;
-Ni kiongozi mwenye sura nzuri.
-Anajua kutia moyo watu jao hali ni ngumu kimaisha lkn tunaishi kwa matumaini ambayo anajua fika kwamba hayatapatikana ktk kipindi chake.
-kiongozi wa kwanza kukosa Trust ya watu wa Usalama wa Taifa, kwani mwaka 2010 maeneo yanakokaliwa na wakuu serikalini kama Oysterbay alipata kura chache kuliko Dr.Slaa.
-Ana Safari nyingi sana ndani na nje ya nchi hadi anakosa muda wa kutatua shida za wananchi.
-Makamu wake na Mama Kikwete nao wana safari nyingi sana na hii ni Matumizi mabaya ya pesa zetu.
-sijui hata anakopeleka nchi-labda anajua yeye.
-kila kitu kimeuzwa sasa -rasilimali zetu
-mgogoro kila mahali; CCM mgogoro, UVCCM mgogoro, wananch migogoro,n.k.
-Anapenda sana kulipiza kisasi; mfano yanayowakuta CHADEMA na viongozi wake sasa ni matokeo ya Dr. Slaa kukataa kutambua Urais wake mwaka jana (mwenye akili atalikua hilo).
-Anawatumia dola (hasa Polisi na Mahakama) kama vyombo vya kuwanyanyasia wananchi mbalimbali wanaodai haki zao.
-Ni kiongozi anayelenga kuwafurahisha rafiki zake, ndugu zake, jamaa zake na si kufanya vitu kwa maslahi ya wananchi hasa ktk nafasi za uongozi.
-Ameshindwa kujifunza ktk na uhalisia na hakika ndani ya muda mfupi, wananchi wengi hawana imani naye tena.

Wadau, nanyi ongezeni mazuri au mabaya mtakayowakumbukia hawa viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom