Je Hatuwezi Kujifunza kwa hawa???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Hatuwezi Kujifunza kwa hawa????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Prodigal Son, Jan 13, 2011.

 1. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  JE Hatuwezi Kujifunza kwa hawa?????

  Kwa Mtanzania yeyote ambaye anakipato halali, utakubaliana na mimi kwamba garama za maisha kila siku zinapanda ( Mfano Bei za Umeme, maji,pango, Mafuta mlio na magari,). Kila hali inapokuwa tete WATAWALA wanatoa sababu za kisiasa na wananchi wanaridhika na kukaa kimya. Ni mwezi uliopita serekali ya EVO MORALES- BOLIVIA aliazimia kuondoa FUEL SUBSIDIES kitu ambacho kingesababisha kupanda kwa bei ya mafuta, nav itu vingine,, Nchi nzima ililipuka kwa Maandamano. Tunisia nchi haitawaliki kuna maandamano kila siku tatizo VIJANA HAWANA AJIRA. Algeria Kuna maandamano pia KISA kupanda kwa garama za maisha na high rate of unemployement. Miaka michache hivi nilikuwa GABON bei tu ya mkate ilipanda nchi nzima ikalipuka kwa maandamano na fujo,,,,,,sasa sisi watanzania inamaana haya hayajatuadhiri??????Mfano;
  1. Bei ya Umeme imepanda;;;;;;;;;;;Wananchi,,,NGO,,,Wanaharakati, Wasomi,KIMYA
  2. Bei ya Gesi imepanda;;;;;Kila mtu kimya
  3. Bei ya Petroli,Diesel, kerosene;;;;Kila kukicha inapanda sababu zinazotolwea ni kisiasa zaidi,, mbona kuna ka ahueni ya bei za Mafuta Kenya, Uganda, Rwanda,, Miaka mitano imepita KIKWETE na serekali yake Mlituahidi Mgetoa Mtaji kwa TPDC ili iwe inaagiza mafuta na kutoa ushindani kwa makampuni binafsi mpaka leo,, ni siasa tu,,,,,wamewaachia Wahindi na baadhi ya Waarabu na vikampuni uchwara vyao wanagiza mafuta kwa bei rahisi wanuza kwa bei gali, wanachakachua mafuta magari ya watu yanaharibika WATAWALA MPO KIMYA kila siku mnatoa sababu za kisiasa;;;; KENYA kuna kampuni ya serekali inatoa ushindani kwa makampuni binafsi na mafuta hayapandi kila kukicha,,Mbona msijifunze huko?
  4. Bei ya MAJI;; imepanda saana, walala hoi tulio wengi hatupai maji safi na salama;; Nakumbuka mika mitano WASIRA alipo kwa waziri wa maji mlitoa ahadi mgejenga bwawa kubwa la maji Morogoro lingesaidia upatikanaji wa maji kwa jiji la DSM kwa mwaka mzima cha kushangaza mpaka leo hakuna kiliihofanyika;; wananchi tuliowengi tushasahu na tupo kimya
  5. GESI YA SONGOSONGO;; Tulishawishika tukabadili magari yetu kwa garama tena kubwa tu yawe yanatumia hiyo gesi, kwakuwa gesi inapatikana hapa nilifikiri bei ingekwa rahisi cha kushangaza bei sasa inakimbizana nay a Petrol na diesel
  Kumbuka SEREKALI iliyopo madarakani inatakiwa kuwajibika kwa watu wake. Hii ya kwetu hata kwa kutumia akili na uelewa wa kawaida haiwajibiki kwa wananchi wanaofaidika na kodi zetu kubwa tunazokatwa ni wanasiasa, familia zao na watu wao wa karibu.
  NINI KIFANYIKE
  Popular Uprising;;;;Hii imeshasaidia Nchi nyingi kuwaondoa watawala ambao walijisahau kwakujijali wao wenyewe na kuwasahau wananchi;;;;Mfano mzuri ni French REVOLUTION,'Bulldozer Revolution – Mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Slobodan Milosevic, Thailand – RED protests.
  Natoa wito kwa MNAOJIITA wanaharakati, wasomi, wanasiasa vijana mchukue hatua.NI vema tukaelewa kwamba HAWA watawala hatukuwalazimishia VYEO waliomba wenyewe ni wajibu wao kuwajibika,,,,
  SIONI sababu garama za maisha kupanda kila siku, Grand corruptions, Ukatili wa polisi na vyombo vingine vya dola,Nchi kukosa mwelekeo,, Haya yote yanawezekana kama watawala watakuwa makini. Mbona KENYA, Rwanda; Quarter, UAE, Jordan IMEWEZEKANA? Nchi kama QUARTER wanategemea mafuta na gesi tu, wamezitumia kuendeleza sekta nyingine na kujenga miundmbinu,,,,KIKWETE umeshindwa nini kutumia GESI, Dhahabu, TANZANITE, MISITU, Ardhi yenye RUTUBA kuiendeleza nchi??????????
   
Loading...