Je, hali inayoendelea kuhusu derby ya Kariakoo ni mpango mkakati wa kisiasa?

Je, hali inayoendelea kuhusu derby ya Kariakoo ni mpango mkakati wa kisiasa?

The introvert

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2023
Posts
1,118
Reaction score
2,228
HABARINI ZA ASUBUHI WANAJAMVI.

Naomba tushirikishane mambo machache kuhusu hali iliyopo kwa sasa kuhusiana na suala la derby ya kariakoo.

Je hali hii endelevu ya sintofahamu iliyopo baina ya TFF, TPLB, SIMBA SC pamoja na YOUNG AFRICANS SC ni mpango maalumu wenye mlengo wa kisiasa kwa ajili ya kuneutralize mapambano ya wananchi dhidi ya serikali yao?

Ndani ya hizi siku mbili ni kama agenda zote za kisiasa zimezimwa na hili swala.

Toa maoni yako wewe kama mdau!
✍🏿The introvert
 
Tunawekwa busy kuwapisha wapumue kidogo... Kiki zote zikiisha tunarudi square one
e7350b46-a77a-4779-ae44-99f3dd9ead44_0_watermark.jpeg
 
HABARINI ZA ASUBUHI WANAJAMVI.

Naomba tushirikishane mambo machache kuhusu hali iliyopo kwa sasa kuhusiana na suala la derby ya kariakoo.

Je hali hii endelevu ya sintofahamu iliyopo baina ya TFF, TPLB, SIMBA SC pamoja na YOUNG AFRICANS SC ni mpango maalumu wenye mlengo wa kisiasa kwa ajili ya kuneutralize mapambano ya wananchi dhidi ya serikali yao?

Ndani ya hizi siku mbili ni kama agenda zote za kisiasa zimezimwa na hili swala.

Toa maoni yako wewe kama mdau!
✍🏿The introvert
Wanacho pigania Yanga kwa Tz hakina tofauti na wanachopigania Chadema
1.Reforms kwenye mfumo wa uendeshaji ligi na club za mpira Tz
Mfano: mshindani na mshiriki wa ligi kuu kuwa na uwezo wa kudhamini vilabu vingine vingi vinavyokutana nae Uwanjani
2.Bodi ya ligi kuwa na watu wenye mrengo mmoja na kufanya maamuzi yasiozingatia haki na usawa .
Chadema wanalilia hayo hayo
Chama kuwa vyama vingine shikizi kupingana na chama kinachopinga Chama kilichoko madarakani
Tume yenye watu waliovua nguo za rangi fulani na kuvaa uhusika kulingana na uhitaji wa wakati huo,
Sasa kinachotokea ni Raia wa kawaida kupata sonona kwa sababu
Umezuia Chadema wasishiriki Uchaguzi
Ukazuia Soka la Bongo lisiwape Furaha
Wakati wanataka kukimbilia kanisani kupata neno la faraja, Ukafungia kanisa
Wakiwa wanataka hata kwenda kuangalia Dunia inasemaje huko X ukafunga x sasa unataka huyu mtu afe kabla ya muda wake?
 
Ujinga wa Tz wengi upo kwenye Simba na yanga, Pana kijiwe kimoja pale karume watu wapo nyomi 24/7 Kila ukipita mada inayojadiliwa ni Simba na yanga.
 
HABARINI ZA ASUBUHI WANAJAMVI.

Naomba tushirikishane mambo machache kuhusu hali iliyopo kwa sasa kuhusiana na suala la derby ya kariakoo.

Je hali hii endelevu ya sintofahamu iliyopo baina ya TFF, TPLB, SIMBA SC pamoja na YOUNG AFRICANS SC ni mpango maalumu wenye mlengo wa kisiasa kwa ajili ya kuneutralize mapambano ya wananchi dhidi ya serikali yao?

Ndani ya hizi siku mbili ni kama agenda zote za kisiasa zimezimwa na hili swala.

Toa maoni yako wewe kama mdau!
✍🏿The introvert
Ndiyo.No reform no election
 
Kwenye dunia ya sasa hata ufanye siasa za namna gani kuhadaa wananchi na kuhamisha ajenda na mijadala mahsusi itajulikana tu kuwa unafanya propaganda. Watu wana akili kuliko AI ni ngumu kuwahadaa waache kujadili mambo muhimu ya nchi yao watabaini tu kuwa kuna abrakadabra inafanyika kimkakati
 
Kwingine ni Lushoto Mjini kuna mijamaa pale stand hawapigi hata mswaki ni kelele tuu
hawa wapo karibu vijiwe vyote vya kuuzia magazeti wamejazana, mada kuu ni ubishi wa yanga na simba. Siasa za nchi hawajadili wanaogopa kama ukoma kuzungumzia yanayojiri
 
Sio Kwa dunia ya Sasa watafute mbinu nyingine hizo ni za kizamani No reform No election
 
Back
Top Bottom