Je, Faru Kileo ni muhimu kuliko Lissu, Ben Saanane na Azory?

Noel Shao

Member
Jan 19, 2017
89
185
“Kuna faru aliyejulikana kwa jina la Kileo aliuawa na majangili. Baada ya kuletewa taarifa za kifo chake tuliagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili tujue alivyouawa, tuwajue waliomuua na hatimaye tutathmini hali ya usalama wa faru wetu waliopo eneo hilo ambalo lipo mpakani na nchi jirani ya Kenya.”

“Mradi huu wa faru upo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na faru ameuawa jirani na vigingi vya mpaka wa kimataifa. Tumeunda kamati kuchunguza mauaji haya ya Faru Kileo na tutatoa taarifa rasmi uchunguzi utakapokamilika, japokuwa mradi huu unaendeshwa vizuri na kwa mafanikio makubwa lakini ni lazima tujiridhishe kama tuko salama kiasi gani.”
Waziri wa Maliasili na utalii, Hamis Kigwangalaa!

[HASHTAG]#MyTakes[/HASHTAG]!
Raslimali za nchi ni muhimu mno, kupambana na ujangili ni jambo bora pia.
Ila utu wa binadamu una thamani ya asili, huwezi substitute na mnyama au mali au chochote.

Pamoja na juhudi hizo, serikali kama ina double standard katika kutetea utanzania na material things. Mambo yote yana umuhimu ila kipau mbele ni uhai wa MTANZANIA na siyo Mali au wanyama.

Ben Saanane alipo potea tuliomba iundwe tume kuchunguza tukio la kupotea kwake, ila serikali ikapuuza na cha ajabu ikaunda tume ya kuchunguza kuuawa kwa "Faru John" Ben Saanane akaonekane si kipau mbele bali Mali za nchi zina thamani kuliko damu ya mmoja wetu.

Tume za haki za binadamu zikapiga kelele, wana harakati wakapaza sauti, Kizazi Cha Kuhoji (UTG) wakatoa matamko, kuundwe tume ya kuchunguza matukio ya kutekwa, kupigwa, kuteswa, na kuuawa kwa watu. Ila hakuna tume ya bunge au serikalini iliyo ridhia uundwaji wa tume.

Leo Faru Kileo ameundiwa tume, ambayo inaweza kutoa majibu ya haraka kuliko uchunguzi wa kifo cha Acquline, nk.

Tundu LISSU alipigwa risasi, bunge mpaka Leo hawaja ridhia kutoa haki za matibabu kwa Mh.Lissu, ila Faru Fausta na Faru Ndugai walipo ugua walitibiwa . Hapa inatoa picha gani? Thamani ya asili ya damu ya mwanadamu hasa MTANZANIA haina maana, jambo ambalo si sawa!

Mwandishi Azory Gwanda amepotea, baadhi yetu tuna ona poa tu. Bunge linaona poa tu,serikali nayo inaendelea na uchunguzi. Siyo afya, siyo maana ya uzalendo, siyo maana ya utaifa, na siyo maana ya utanzania.

Ila Matukio ya kutisha yanapo tokea nchini hasa ya kuvamiwa, kutekwa, kupigwa risasi, kunyanyaswa na kuuawa yanafaa yaibue taharuki kwa kila MTANZANIA, nchi isitulie.

Siyo tunaona wenzetu wanateseka tunaendelea na our daily routine, we don't care about him/her, we just rise up our vocal that's not our case, its belong to them, We should not take it as business as usual.
I genuinely assured you, we are supposed to react now or perish .

Its not time to keep quite, i call on our compatriots to join the efforts against those actions, if we dont react now, next generation will not be able to forgive us.

Nini maoni yako?

Ndimi, Noel Shao .
[HASHTAG]#MjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]
 
Wanaogopa wakikaa kimya hata faru john na faru ndugai watauawa, wanadhani faru hao wawili hawawezi kufa
 
Back
Top Bottom