Je elimu bure imeshusha elimu yetu?????

Je elimu bure imeshusha elimu yetu?????

gm man

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2017
Posts
1,177
Reaction score
1,456
Wakuu
Ni miaka kadhaaa sasa tangu nilipo hitimu kidato cha nne katika shule Fulani ya kata hapa kwetu

Nakumbuka shule yetu ya kata tulifaulu watu wengi kuliko miaka yote ya nyuma....
Division one zilikuwa 15 haikuwahi kutokea..

Tokea shule ile ilipoanzishwa ilikuwa na ongezeko la wanafunzi kufaulu kila Mwaka

Baada ya mimi kumaliza kidato cha 6 nimejaribu kuangalia graph ya ufaulu kwa shule yetu na kuona ikishuka Sana.... Hivi sasa vijana wa shule yetu hawafaulu tena kwa kishindo ..idadi ya division 1,2 na 3 inazidi kupungua huku division 0 zikiongezeka haswa Mwaka 2017 na 2018

Ndipo hapa ninapo jiuliza "je Sera ya elimu bure inarudisha nyuma elimu yetu??? "

Nakumbuka wakati mimi nasoma tulikuwa tunalipa michango ya shule ambayo kwa sasa haipo tena..

Siku ya school baraza mkuu wa shule alituelezea matumizi ya fedha zetu huku nikimsikia akisema kuwa baadhi ya fedha tumewalipa waalimu.. Hii ilimaanisha kuwa shule ilikuwa ikiajiri baadhi ya walimu kwa fedha zetu sisi ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu... Leo hii michango ile haipo basi shule haiwezi kuajiri walimu ili kuweza kupambana na uhaba wa walimu (nakumbuka walimu waliokuwa wameajiriwa na shule walikuwa wa mathematics, physics, chemistry na biology.. Wengi mnafahamu uhaba wa walimu wa science katika taifa letu)

Pamoja na michango ile pia tulikuwa na tuition ambayo kwa siku tulichangia shilingi 200...na tulisoma masomo mawili kila siku kuanzia saa tisa alasiri hadi saa kumi na moja...

Tuition ile ilisaidia sana walimu kuweza kimaliza topic kwa wakati.. Pia ilisaidia baadhi ya wanafunzi kukosa muda wa kuzunguka na mtaa na kuwa keep busy na kusoma..
Kwa upande wangu ilinisaidia Sana kuweza kufaulu kwakuwa niliweza kumaliza topic kwa wakati na kufanya revision ya uhakika..

Hivi sasa tuition za kuchangia shuleni haziruhusiwi... Tuition ni bure
Maswali ya kujiuliza
Je nimwalimu gani yupo tayari kupoteza muda wake bila malipo????

Kwa mshara gani mwalimu anaolipwa mpaka aweze kufundisha tuition bure????

Ukipata majibu ya maswali hayo unaweza kugundua kuwa elimu bure katika shule niliyo soma imepunguza baadhi ya vitu
Imepunguza tuition shuleni Pia imepunguza waalimu wa kuajiriwa na shule ..
Je serikali imeajiri walimu wa kutosha?????

Hitimisho
Kwa upande wangu naamini waliotuletea elimu bure hawakujipanga kutupatia elimu bure... Japo ni haki yetu kupata elimu bure

Serikali ilitakiwa kuajiri waalimu wa kutosha na kuongeza walimu wa masomo ya science

Serikali inatakiwa kuboresha mishahara ya waalimu na kuwapa marupurupu ya kutosha..
Serikali inatakiwa kuongeza vitendea kazi mashuleni..

Katika shule yetu ufaulu wa masomo ya science umpeungua maradufu

Shule hizi za kata ni Msaada mkubwa kwetu sisi masikini lakini serikali ni kama imezisahau

Wako katika elimu

gm man
 
Back
Top Bottom