Je, EAC inaweza kumudu bila Tanzania?

Je, EAC inaweza kumudu bila Tanzania?

Maswala

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Posts
560
Reaction score
225
Wana JF hapa nimeambatanisha picha hapa chini, niliyoitoa katika gazeti la kila juma ya The East African la Aug 31-Sep 6, 2013.

Kutokana na takwimu katika gazeti hili:

1. Tanzania ina ardhi kubwa kuliko nchi zote kwa pamoja.

2. Kenya haina aridhi hata ya akiba, kiasi kwamba tayari imetumia sehemu ya misitu yake ya asili.

3. Rwanda na km za mraba zisizofikia 3,500 kati ya 26,000

4. Burundi ina akiba ya 16,000 km za mraba 16,000 kati ya 27,000.

5. Uganda ndiyo yenye akiba nzuri ya ardhi inayofikia km za mraba 78,000.

6. Burundi ina akiba kubwa ya ardhi kuliko Kenya na Rwanda.

7. Akiba ya Tanzania ni zaidi ya km za mraba 450,000! Ukijumlisha akiba ya aridhi za nchi hizo nne, utagundua kuwa haifikii hata theluthi 1 ya akiba ya ardhi ya Tanzania.

Kwa maana hiyo ni wazi kuwa kupishana kunakoendela kunachochewa na wivu, uchu wa ardhi ya Watanzania.

Kibiashara, chati inaonyesha kuwa EAC ni tegemeo la pili, ambapo Kenya ndo mnufaika mkubwa zaidi ya wenzake.

Pia Tanzania inaonyesha kuwa na maji mengi kuliko zote za EAC.

Ukiongeza mali asili za nchi hii kama vile madini, gesi, mafuta, bahari, maziwa, mipaka 8, maeneo ya kitalii n.k. utagundua kuwa Tanzania si mbia wa kutengwa kwa watawala wenye busara. Ndiyo maana mataifa makubwa hayakomi kuizuru nchi hii.

Pia tanzania ni soko muhimu kwani ina idadi kubwa ya watu kuliko nchi zote za EAC. Kenya itaathirika zaidi endapo jumuiya hii itakufa.

Sasa ni wakati kwa viongozi wetu kuwa na utashi kujenga na kuimarisha mahusiano na nchi zingine kama DRC ambayo inaweza kuleta faida pande zote mbili kwa uwiano unaoshabiiana.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
mleta mada: sifa ulizozitoa hapo ni za kweli. Lakini EAC inaweza kuwepo na kufanikiwa KWA HARAKA ZAIDI kama Tanzania haitakuwemo. Sababu mmoja kubwa ni kwamba siasa zitapungua sana ndani ya jumuiya, watabaki wenye utamaduni wa utendaji.
 
Japan na Uk zina ukubwa gani? Ardhi nani ana shida nayo? Kila kitu ni strategic

Strategy? Yes! Hata ukoloni na utumwa ni miongoni mwa "strategies" zilizolinyonya bara hili. Ndio maana Uingereza, pamoja na udogo wake ni imara!

Kagame ametenda nini kwa Rwanda-kuwachinja na kuwakimbiza nchi za nje wapinzani wenzake wa kisiasa?

Museveni kaifanyia nini Uganda tangu aingie madarakani.....Nenda ukafanye research kampala

Uhuru- ana utendaji gani unaoujua zaidi ya historia ya utajiri wa kupora ardhi uliofanywa na familia yake miaka ya nyuma?

acha kukurupuka.
 
Strategy? Yes! Hata ukoloni na utumwa ni miongoni mwa "strategies" zilizolinyonya bara hili. Ndio maana Uingereza, pamoja na udogo wake ni imara!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Uwezo wa Tanzania kumudu bila EAC nimkubwa tu, tukumbuke miaka ambayo EAC ilivunjwa tanzania nchi hizi zilikuwaje? kwa suala la kuwa na ardhi ya akiba yaweza kuwa faida au yaweza kuwa chanzo cha migogoro kwa nchi wananchama na ndio maana wanatama movement ziongezeke kwa kasi na ukumbuke tanzania ndio anaye suasua katika kukubali baadhi ya sheria katika jumuiya hii... lakini kwa sababu ambazo naona ni zamsingi

Nilazima Tujue

chanzo cha matatizo ya EAC yameanzishwa na Kenya mara baada ya Obama kuja TZ jamaa walikasirika kuanzia Uongozi hadi Raia wake..... Kenya kaanza kuwatumia baadhi ya viongozi kama Museveni na Kagame kueneza chuki yake na baada ya kauli ya rais ndio kabisaa ikachochea lakini pia tujue kwamba Kagame na Museveni lao Moja kule DRC ambapo tanzania inamajeshi yake...... kwaiyo hapa ni Kenya vs Tanzania = Obama trip, Kagame+Museveni vs Tanzania = DRC .

Hawa nikuwa kalia kimya bila msamaha wala kujipendekeza kwani Rais Kenyatta ameanza kusaini mikataba kinyume na sera na taratibu ya EAC mfano ni huo mradi wa Bandari, ule uko chini ya EAC nilazima TZ wangeusishwa kisheria kwani hapa tukifuatilia bado mgogoro utazidi japo niukweli ambao hata Kenyatta anajua hilo...... kuna mambo mengi ambayo nchi hizi 3 zimefanya kinyume na taratibu na mkataba wa EAC AMBAO NIKOSA KUBWA NIKAMA WAMESHAUVUNJA TU BADO KIMAANDISHI NA KAULI ZA MOJA KWA MOJA

Mkumbuke kuwa hata EAC ya mwanzo Jomo Kenyatta ndiye chanzo cha kuvunjika kwake leo mwanaye kaja analeta yale yale. kingine ni ukaribu wa TZ na USA, kwani kule US jamaa atambuliki kama rais coz ni mtuhumiwa kule ICC hawa watarudi tuu na huu dnio muda wa wana Diplomasia wa TZ kusimama na kuangalia mstakabali wa taifa if hawa jamaa wakitunyima ushirikiano Plan B inatakiwa ili kuweka mambo sawa adhari zaweza kuwepo na faida zaweza kuwepo kazi kwetu kuweka focus.
 
Japan na Uk zina ukubwa gani? Ardhi nani ana shida nayo? Kila kitu ni strategic

Mbona unazungumzia ardhi bila kutaja soko, maji, nk? Waache Wakenya na Waganda waburuzwe na Paul Kagame. Watakuja kumshtukia when it is too late! Kuhusu ardhi, asikudanganye mtu, ufinyu wa ardhi huzaa conflicts zisizoisha. Wakenya mate yanawadondoka wakiitamani ardhi yetu. Tusiwachekee hawa watu, waachwe waendelee na mipango yao ya kuijumuisha hata Al Shabaab kwenye EAC!
 
Kagame ametenda nini kwa Rwanda-kuwachinja na kuwakimbiza nchi za nje wapinzani wenzake wa kisiasa?

Museveni kaifanyia nini Uganda tangu aingie madarakani.....Nenda ukafanye research kampala

Uhuru- ana utendaji gani unaoujua zaidi ya historia ya utajiri wa kupora ardhi uliofanywa na familia yake miaka ya nyuma?

acha kukurupuka.

bahati mbaya umezungumzia VIONGOZI, umesahau WATU. next time usikurupuke.
 
bahati mbaya umezungumzia VIONGOZI, umesahau WATU. next time usikurupuke.

watu kivipi?

hakuna nchi zenye watu waliogawanyika kiitikadi kama hizo...

Kenya kuna - anti uhuru wengi sana
Uganda ndiyo usipima wanasema wazi kuwa wanatawaliwa na mtusi...na wakichachamaa M7 anatishia kuvunja bunge nchi itawaliwe kijeshi tena
Rwanza ndiyo usiombe-watu wametiishwa kwa nguvu na kuogopa kufanyiziwa na vibaraka wa kagame.

kama ni watu soko......kenya inaihitaji tz kwa soko la bidhaa za viwanda vyake....soko la kenya ni dogo ndiyo maana hapa tz tu kuna equity bank, kcb, cb, boa zote ni bank kutoka kenya achilia mbali bidhaa za viwanda ukianzia omo, maziwa na zingine nyingi...
 
Ukibahatika kufanya kazi/project/biashara na watu wa nchi hizo utagundua tofauti yao na waTZ (kwa wastani of course). Kwa kusoma na kusikia juu juu unaweza ukawa na mtazamo tofauti.
 
Ukibahatika kufanya kazi/project/biashara na watu wa nchi hizo utagundua tofauti yao na waTZ (kwa wastani of course). Kwa kusoma na kusikia juu juu unaweza ukawa na mtazamo tofauti.

Kweli kabisa. Hawa wanaosema kuwa wengine hawataweza bila ya wao, waangalie wako wapi kimaendeleo hivi sasa? Sijui kwa nini watu hawawi 'realistic' badala ya kuamini ngonjera tu za ardhi, maliasili etc. Well, ardhi, maliasili nk vitafaa tu ikiwa kuna viongozi. Tanzania haina, na haikuwa na viongozi waliokamilika (walikuwepo nusu nusu ie. umahiri wa siasa bila uchumi tu). Bila ya viongozi vitu hivyo havina maana: Taiwan, Singapore, Japan zina ardhi au maliasili ganii? Uchumi wa Mauritius ni mzuri kuliko wa Nigeria.
 
Tanzania inazo nguzo za uchumi. Hata sisi ajenda yetu kuu ni uboreshaji wa miundo mbinu ya kiuchumi. Tanzania imekuwa na viongozi waliopigania maslai nchi nyingi Africa. Na sasa ndio wakati wa kujiweka sawa kiuchumi. Watanzania sasa wanalewa, wanahitaji mageuzi ya kimfumo. Hili ni jukumu la waTZ wenyewe.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kweli kabisa. Hawa wanaosema kuwa wengine hawataweza bila ya wao, waangalie wako wapi kimaendeleo hivi sasa? Sijui kwa nini watu hawawi 'realistic' badala ya kuamini ngonjera tu za ardhi, maliasili etc. Well, ardhi, maliasili nk vitafaa tu ikiwa kuna viongozi. Tanzania haina, na haikuwa na viongozi waliokamilika (walikuwepo nusu nusu ie. umahiri wa siasa bila uchumi tu). Bila ya viongozi vitu hivyo havina maana: Taiwan, Singapore, Japan zina ardhi au maliasili ganii? Uchumi wa Mauritius ni mzuri kuliko wa Nigeria.

ni kweli kabisa mkuu, lakini usiangalie uchumi wa nairobi au utajiri wa mtu mmoja ukadhani ni wa wakenya wote, ingia Uganda uone, nenda Rwanda vijijini uone wahutu walivyogeuzwa watumwa na wachunga ng'ombe wa watutsi.

Afya ya familia haipimwi kwa kuangalia kitambi cha baba!
 
😛layball:
 
Japan na Uk zina ukubwa gani? Ardhi nani ana shida nayo? Kila kitu ni strategic
Ndugu hawa jirani zetu wanatuhitaji sana kuliko sisi tunavyo wahitaji. Pia tumshukuru sana rais wetu Kikwete kwa kutuokoa kuchelewa kuingia kichwa kichwa kwenye shirikisho la kisiasa zile siasa zao za kibabe tusingezimudu ndugu zangu zangu hata timu ya Samweli Sitta inayotuwakilisha katika shirikisho hilo japo watz huwa tunatazama zaidi madhaifu ya viongozi wetu mfano timu ta Sitta ilishawahi kukataa pendekezo la wajumbe wa Kenya la kutaka kuingiza kipengele cha masuala ya ulinzi eti taifa moja la Afrika mashariki likishambuliwa kijeshi nchi zote ziingie kijeshi na hili lilikuja baada ya Kenya kuwa imezidiwa na alshabab hakuna asiyejua jinsi Kenya ilivyozidiwa nguvu na al shababu hadi akaomba kuunganisha majeshi yake na majeshi ya umoja wa Africa AMISOM afu pia Uganda inawaasi wengi pia kwa mtindo wa siasa zao wanayo nafasi kubwa ya kutengeneza maadui yote haya ndio yanachangangia haya tunayoyaona sasa tuamke watanzania MUNGU anatupenda jamaa wamejionyesha mapema kabla hatujafika mbalimbali ya hii safari hata kama tukiendelea nayo tatasonga kwa tahadhari kiliko kwenda kichwa kichwa the hero is the one who stand alone MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Tusidanganyane Eac itasambaratika haraka bila Tz, na ikivumilia kidogo itaukuwa ni ya kulazimisha kishifitna tu, ni sawa na Tanzania kuungana kiuchumi na Gabon huku MiKongo ikitugawa. Kenya itaenda chini na kwa maumivu itawageukia Rwanda/Uganda hapo shida itawafanya wajipendekeze mmoja baada ya mwingine. Uchumi wa Tanzania utaimarika daima
 
Kagame ametenda nini kwa Rwanda-kuwachinja na kuwakimbiza nchi za nje wapinzani wenzake wa kisiasa?

Museveni kaifanyia nini Uganda tangu aingie madarakani.....Nenda ukafanye research kampala

Uhuru- ana utendaji gani unaoujua zaidi ya historia ya utajiri wa kupora ardhi uliofanywa na familia yake miaka ya nyuma?

acha kukurupuka.
hater!
 
Tuwaangalie vizuri hawa jirani zetu si watu wema hata kidogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom