Sijasema kwamba ubora wa maandishi yangu unatakiwa kuwa sahihi wakati wote, hili nalikubali. Hapa naongelea kitu tofauti.
Naongelea standards na applications zake. Naongelea "Noblesse Oblige". Naongelea "To whom much is given, much is required". Hizi ni basic principles. Huwezi kumpa mtoto wa darasa la pili mtihani wa Chuo Kikuu kuandika research paper, utaonekana unachekesha.
Mkuu, ni vigumu kunishawishi kuwa hapa JF panafanana kwa namna yoyote na chumba cha mtihani. Ungeweza kufananisha majadiliano ya kawaida kati ya mwanafunzi wa darasa la pili na mtu wa chuo kikuu. Katika maongezi ya kawaida, hakuna tofauti kubwa kati ya alie chuo kikuu na alie katika shule za chini.Mimi kwa kazi ninayofanya na dhamana yake kwa maisha ya kila siku kwa wananchi wa Tanzania ni kama mtoto wa darasa la pili. Dr. Slaa kazi anayofanya na hususan anayoiomba ya urais, dhamana yake kwa maendeleo ya taifa ni kama mtihani wa Chuo Kikuu kuandika research paper. Kutupa mimi mtoto wa darasa la pili na Dr. Slaa mtu anayeandika research paper ya chuo kikuu standards zile zile na mtihani ule ule itakuwa ni utovu wa maarifa.
Mimi si Dr, Slaa ni Dr. Mimi siko katika uongozi wa kisiasa wa Tanzania ngazi ya taifa, Slaa yumo, mimi sijaomba dhamana ya kupigiwa kura na wananchi hata ujumbe wa nyumba kumi, Slaa kashaomba na sasa anaomba kura za mamilioni ya Watanzania nchini kote.
Utawezaje kutuweka katika fungu moja?
Sikusema kama napingana na ligi (trust me... napenda sana ligi za JF). Tatizo ni kuwa, sidhani kama Dr Slaa ana muda wa kuendesha ligi na yeyote hapa JF kwa muda huu. Ligi zinahitaji uwepo JF masaa 24, otherwise kina Kiranga na wenzake watakuita muongo.
Unlike you, mimi sitetei ligi, natetea majadiliano yenye mantiki.
Sitaki Dr. Slaa aje kuendesha ligi, nataka aje kuendesha majadiliano yenye mantiki.
So far Dr. Slaa ananipa haki ya kumuita muongo, kwa kuahidi kwamba maswali yatajibiwa halafu kukimbia bila kujibu maswali wala kujiudhuru
Waswahili walisema "Ada ya mja kunena, muungwana ni matendo".
Kiranga said:Kama unaita kuulizana kuendeleza ligi, then point nzima ya JF ni kuendeleza ligi. Kama huna nia ya kuendeleza ligi huhitaji kuwa JF.
Kiranga sitaki kukuaibisha rafiki yangu ila katika hili umeanza kujichanganya na kupotoka.
Hiki ndicho ulisema somewhere hapo juu
Come on ... mbona unaniangusha mazee
Ndio madhara ya kuwa all over the map hadi unasahau hata uliyoyasema (andika). Sasa subiri spin....
Unayosema ni sahihi kabisa. Ila ni sahihi kwenye nyanja tofauti na hapa tulipo. Hapa JF hakuna haja ya kuwa too keen na maandishi tunayoyatoa. Sababu ni kuwa hapa tunafanya discussion tu.
Mkuu, ni vigumu kunishawishi kuwa hapa JF panafanana kwa namna yoyote na chumba cha mtihani. Ungeweza kufananisha majadiliano ya kawaida kati ya mwanafunzi wa darasa la pili na mtu wa chuo kikuu. Katika maongezi ya kawaida, hakuna tofauti kubwa kati ya alie chuo kikuu na alie katika shule za chini.
Japokuwa hata ufananisho wako hapo juu si sahihi. Siamini kuwa huwezi kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais. Level hiyo naamini umeifikia. Tofauti yako nae ni maamuzi, uthubutu na nia ya kuomba kuchaguliwa tu. Inawezekana usiwe na exposure ya matatizo ya msingi ya Taifa kama alivyo yeye. Hiyo inaweza kuwatofautisha zaidi..
Vyovyote iwavyo, mapungufu hayo si ya msingi sana kwa taasisi ya Rais, maana ana watu wa kutosha kuhakikisha kuwa nyaraka zake zote ziko sahihi.
Kiranga sitaki kukuaibisha rafiki yangu ila katika hili umeanza kujichanganya na kupotoka.
Hiki ndicho ulisema somewhere hapo juu
Come on ... mbona unaniangusha mazee
Kama unaita kuulizana kuendeleza ligi, then point nzima ya JF ni kuendeleza ligi. Kama huna nia ya kuendeleza ligi huhitaji kuwa JF.
...Nafurahi umeona hili, lakini yeye na jeshi lake lote hawataweza kurekebisha chochote kwamba kuna makosa, je amekubali kwamba wana mapungufu haya na watayafanyia kazi /
Huwezi kunipata kirahisi hivi, this is a very lawyerly qualification.
Sikusema kwamba napenda ligi. Nimesema.
Kama unaita nyekundu ni kijani, then Simba Sports Club wanavaa jezi za kijani. It is a logical twist ambayo wengi wanaosoma vitu juu juu hapa JF hawawezi kuiona.
Ndiyo maana wengine wanaona contradiction sehemu ambapo haipo, wengine wanataka kuniaibisha sehemu ambayo hamna cha aibu, na wengine wanaona nipo all over the map wakati mimi nipo somewhere on a ship near Port Harcourt Nigeria.
Yele yele yele yele ... "same difference" ... kama unakumbuka ile movie ya Gene Hackman na Keanu wa matrix (replacements?)
Yele yele yele yele ... "same difference" ... kama unakumbuka ile movie ya Gene Hackman na Keanu wa matrix (replacements?)
JF tunawasiliana kwa maandishi. Kama unasema hatuna haja ya kuwa too keen on maandishi, basically unasema hatuna haja ya kuwa too keen on anything. How can we be too keen on anything if we cannot be too keen on the way we communicate/
Sijasema JF ni chumba cha mtihani, nimesema standards za kum judge Slaa kwa level yake, popote atakapokuwa, zikilinganishwa na standards za kuni judge mimi, ni tofauti kama mtihani wa darasa la pili na research paper ya Chuo Kikuu. Big difference.
Unajuaje kwamba naweza kuomba urais? Vipi kama nina uwezo na ujasiri ninao lakini katiba hainiruhusu kwa sababu inanilazimisha kuingia katika chama cha siasa na mimi siamini katika kushiriki katika vyama hivi ? Usiweke assumptions tu.
Unaweza kumwambia mtu "japo hujasema kwamba unataka kununua hili gari langu, lakini una uwezo huo, hivyo nipe hela zako, ni haki yangu nikuuzie gari hili kwa sababu una uwezo wa kununua gari hili" ? Si utakuwa kichekesho ?
Quote ya hapo juu naikubali kabisa. Na wala sijakulaumu kwa kufanya scrutiny kwa mgombea yeyote. Ninachohofia ni kutumia muda mwigi kujadili makosa ambayo hayana mshiko. Kama ungejadili na ku-analyse kilichoandikwa na mtoa hoja wa kwanza kwenye thread hii, ambae ametoa shutuma za udhaifu mkubwa wa mgombea, ningeona kuna mantiki kubwa katika mapungufu yaliyoonekana. Lakini kudhani kuwa matumizi ya paragraphs, punctuations n.k za ujumbe ndio mapungufu makubwa, inanipa shida kukubali.Hata kama ningekuwa na chama cha kisiasa na kuondoa issue ya katiba kutonipa nafasi kwa sababu ya kutokuwa na chama, the fact kwamba nina haki/ uwezo wa kugombea urais hainipi presidential level scrutiny automatically kama sija declare nia kwamba nataka kuwa rais. Wangapi wanaweza kuwa rais wa Tanzania lakini hatusikii kuandikwa magazetini wala kuwa scrutinized? Hii ni kwa sababu hawajasema kwamba wanataka kuwa rais, Slaa kasema, kwa hiyo scrutiny level kwake na kwangu ni tofauti.
Sina uhakika kama wana muda wa kukubali au kukataa makosa madogo kama hayo. Siamini kuwa kuna busara yoyote katika kufanya hivyo.Nafurahi umeona hili, lakini yeye na jeshi lake lote hawataweza kurekebisha chochote kwamba kuna makosa, je amekubali kwamba wana mapungufu haya na watayafanyia kazi /
slaa hawezi kuwa raisi hana vigezo
Mwandish Bollen Ngetti aliandika"mtu huwezi kuamka tu usingizini na na kutaka kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hasa kwa nchi changa kama hizi za dunia ya tatu ( na Tanzania ikiwemo) bali yapo mazingira yanayomuandaa mtu ndani na nje ya nchi kuwa mkuu wa nchi.