GE2025 Je Dorothy Temu anawania Ukuu wa Mkoa kama wagombea Urais wanawake waliomtangulia?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
11,798
Reaction score
18,037
Anna Mghwira aliwahi kugombea Urais wa JMT kupitia ACT Wazalendo mwaka 2015 na kushindwa. Baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa katika serikali ya CCM. Mwaka 2020 Queen Sendiga aligombea Urais kupitia ADC na kushindwa. Naye baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa katika serikali ya CCM.

Je lengo la Dorothy Temu kugombea Urais kupitia ACT Wazalendo ni kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa baada ya Uchaguzi Mkuu? Kwa vyo vyote vile Dorothy Temu hawezi kushinda Urais, hilo analijua na Chama chake cha ACT Wazalendo kinajua.
 
Sendiga na Mhgwira wako kazini ....huyu Temu sina hakika.....
 
Una Jicho la Tai!
 
Anna Mghwira alikwisha fariki, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Alinyanyaswa sana na Sabaya!
Najua ....apumzike kwa Amani...Sabaya anamnyanyasa RC aliemuapisha khaa.....
 
Wanakuwa wamepewa maelekezo maalum na hao na CCM .
 
Dorothy Temu amewaahidi wafuasi wake kwamba watalinda kura siku ya uchaguzi.Ngoja tuone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…