Je, Dkt. Shein bado ni mjumbe halali wa Baraza la Mawaziri?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
Mpaka sasa kwa taarifa za vyombo mbalimbali vya habari tumeona kumefanyika vikao viwili vya baraza la mawaziri vilivyoongozwa na Rais Dkt. Magufuli.

Lakini vikao vyote hivyo mahali anapopaswa kukaa Rais wa Zanzibar ambaye kutokana na wadhifa wake ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa muungano imekuwa wazi.

Rais wa Zanzibar huapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Muungano. Kipindi kilichopita alikuwa akiapishwa na Rais wa muungano mpaka pale wa-Znz walipolalamika wakidai Rais wao anadhalilishwa.

Sasa naomba kuuliza wataalamu wa sheria na katiba kama Dkt. Shein bado ni mjumbe halali wa Baraza la Mawaziri wa Muungano.

cc EMT, Kiranga, Pasco, Nguruvi3, Kimbunga, Tetty, MsemajiUkweli
 
Kama yeye anasema bado ni Rais halali wa Zanzibar, basi anasifa kuwa sehemu ya Baraza la Mawaziri.
 
Shein ni Rais halali wa Zanzibar na anaendelea kushika wadhifa huo, na by extension nyadhifa zote zinazotokana na wadhifa huo, mpaka Rais mwingine aapishwe, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na kanuni ya kimsingi ya kukataa power vacuum.
 
Kuna watu ni wabunge na mawaziri japo hawajala kiapo na wanapiga kazi kamakawa...swala ni nani ameshinda uchaguzi? Huyo ndiye mwenye uhalali Kama uchaguz umeharibika iundwe serikali ya mpito mpaka mgogoro utanzuliwe,mtu kuendelea kuongoza wakati muda wa mkataba wako na wananchi umeisha ni kuwakosea wananchi na ni dhambi duniani na mbinguni.
 
Katika mada yako inabidi kutofautisha kati ya kutohudhuria na kuzuiwa (au kukosa sifa ya) kuhudhuria.
 
Yeye ni Amir Jeshi mkuu kwa zenji anashindwaje kijiapisha? na yeye ndio mpangaji wa tarehe ya Uchaguzi kwanini asipange uchaguzi ufanyika after five years.
 
Back
Top Bottom