Je CCM wanafuata Sheria zote za Nchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je CCM wanafuata Sheria zote za Nchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fitinamwiko, Aug 28, 2012.

 1. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Nashindwa kuelewa, kila siku Police wanavunja,kuzuia au kukataa kutoa vibali kwa vyama vya siasa. Wakati mwingine utakuta wasemaji wakuu wa hiyo mikutano ni wenyeviti wa Taifa wa vyama husika, lakini Police bado watawanyima vibali au kubadirisha ratiba. Tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, sijawahi kusikia Police, wamewanyima CCM kibali, mkutano utakaohutubiwa na Mwenyekiti wake wa Taifa.
  Ukiangalia masuala ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa CCM Taifa, anahitaji ulinzi mkubwa,Lakini sijasikia Police wakithubutu kuzuia mikutano yake kwa sababu wanazowapa wapinzani.
  Msafara wa wenyekiti wa CCM Taifa ni kero kubwa kwa wananchi, barabara hufungwa, magari huzuiliwa kwa takribani ya masaa zaidi ya mawili, lakini sijasikia Police, wakionyesha concern kama wanavyotoa kupinga maandamano ya wapinzani. Msafara peke yake wa Mwenyekiti wa CCM Taifa ni msululu enough kuitwa maandamano, IGP Mwema sijamsikia akiupiga marufuku.
  Swali najiuliza,
  1)Hawa wenzetu wa CCM, wanazifuata sheria zote, hivyo Police hawana sababu ya kuwaingilia mikutano/maandamano yao?
  2)Na kama Jibu Ndio wanafuata sheria, Swali lingine ni Mbona rushwa Ime/nashamiri katika chaguzi zote za CCM, au Rushwa si uvunjaji wa sheria? Sheria ni sheria, ukivunja moja basi ni rahisi kuvunja nyinginezo
  3)Nani anayetafsiri sheria Police au Mahakama? Mbona sijawahi kusikia Viongozi wa Upinzani wakihukumiwa Faini/Vifungo kwa kuvunja hizo sheria zinazo simamiwa na POLICE?

  Wakati umefika kwa Serikali ya CCM, kuamua TANZANIA INAFUATA MFUMO WA CHAMA CHA MAPINDUZI ONLY, badala ya hili changa la macho, huku tukizidi kuona police wakiua ndugu zetu.
   
 2. t

  tenende JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wajibu wetu ni kuwalazimisha polisi wafanye kile tunachotaka, maadamu tumezingatia sheria. Wakubwa wengi wa Polisi ni wana -CCM, fuatilia lugha na matendo ya akina TIBAIGANA na Omar Mahita na hata wengi waliopo!...
   
Loading...