GE2025 Je, CCM imeheshimu maoni ya wajumbe kwenye kura za maoni uchaguzi wa wabunge wa CCM? Au ni kuwasumbua tu wajumbe?

GE2025 Je, CCM imeheshimu maoni ya wajumbe kwenye kura za maoni uchaguzi wa wabunge wa CCM? Au ni kuwasumbua tu wajumbe?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,672
Reaction score
4,560
TUJIULIZE JE,Kuna haja ya wajumbe wa CCM kupiga kura ya MAONI ilhali wakijua ni NEC ndiyo inachagua Wabunge?.Je kufanya hivi siyo kuliuza haki za wajumbe waliopiga kura?.Baada ya Kamati kuu ya CCM yaani NEC kutangaza majina ya wagombea ubunge wa CCM ,Vilio vimesikika maeneo mbalimbali ya nchi.Baadhi ya wabunge walioshinda kura za MAONI hawajapewa nafasi badala yake wamepewa walioshindwa!Tuchukue mifano Wabunge waliotoka CHADEMA Ester Matiko,na Esta Bulaya wote walioshindwa kwenye kura za MAONI lakini wamerudishwa kugombea kwenye majimbo yao.

Tuangalie Jimbo la KIGOMA mjini,Baba levo amepewa nafasi ilhali alishindwa kura za MAONI.Kule Tanga ndiyo kufuru UMMY Aliyepata kura ,zaidi ya 5000 amekatwa na nafasi yake kapewa Mbaraka Aliyepata kura 80,CCM inatuma ujumbe gani Kwa wajumbe waliopiga kura za MAONI?

Nafikiri kama NEC ikiona hakuna haja ya kupiga kura walete jina Moja Kila Jimbo Ili wajumbe wapige kura za Ndiyo na HAPANA kama walivyofanya Kule Chalinze na Bukombe.

Kama wajumbe wa CCM wametendewa hivi itakuwaje Kwa kura za wananchi wasioichagua CCM?
 
Back
Top Bottom