Je BET Awards wapo sahihi?

Je BET Awards wapo sahihi?

makavilondo

New Member
Joined
Jun 26, 2015
Posts
2
Reaction score
2
11403409_1001312156568885_7615013724802949433_n.jpg

BET Awards waliamua kuweka vipengele viwili vya Best International Act kwa Afrika na UK ili kutambua ukubwa wa viwanda ya muziki katika maeneo hayo. Hata hivyo vipengele hivi hutolewa saa chache kabla ya show yenyewe ya utoaji tuzo hizo ambazo huhusisha vipengele vyote vinavyoshindaniwa.

Kumekuwepo na mitazamo tofauti kuhusiana na uamuzi wa BET Awards kuwatangaza washindi wa vipengele vya Afrika na UK mapema kabla ya washindi wengine wengine wa Marekani.

Fuse ODG aliyekuwa ametajwa kuwania tuzo hizo, amedai hakwenda kwasababu anahisi BET hawaheshimu ukubwa wa muziki wa UK na Afrika. Wengine wanasema hata hivyo inatosha tu na ni heshima pia. Nini mtazamamo wako?
 
Yaan hata msanii mmoja wa Africa kupewa chance ya kuperform live hawapewi;: Last year ilkua the same ambapo kipengele cha International Act Africa kilitolewa mapema sana,;: hata msanii Diamond sijui kama alfika that time coz hakujua
 
Back
Top Bottom