Habari wandugu. Naomba kujua kama askari wa usalama barabarani wako juu ya sheria?
Leo asubuhi nikiwa natoka nyumbani kwangu, umbali kama wa kilomita moja tu kutoka kwangu nilisimamishwa na askari wa trafiki namba F 8548 (pichani) akiwa na mwenzake mwenye tochi, kosa ni overspeed. Sikuwahi kuona trafiki eneo hilo kwa takriban miaka nane sasa ambayo nimeishi maeneo hayo.
Nilimwambia askari huyo kwamba hapakuwa na kibao cha speed limit maeneo hayo na kibao cha speed kipo mita 500 mbele ya aliponikamatia.
Askari huyo hakuweza kunielewa na akanipa cheti. Cha ajabu ni kwamba alisimamisha gari nyingine aina ya Toyota Raum, yeye pia alikuwa ameoverspeed. Baada ya kuona kwamba dereva wa Raum ni askari mwenzie akamruhusu kuondoka bila kumcharge.
Kwa nini asingempa cheti kama alivyonifanyia mimi? Sasa najiuliza kwamba hawa askari wapo juu ya sheria.
Na eneo alilonikamata hakuna alama yoyote ya speed. Alama ipo mita 500 mbele.
Wewe askari wa trafiki namba F 8548 (pichani) Mungu anakuona. Tuwe makini wandugu tunaoendesha vyombo vya moto. Ni mwendo wa kuviziana na kubambikiana. Wameshika mpini wa jambia makali wameelekeza kwa raia.
Hatuna pa kupumulia. Naamini kwamba askari huyu angefuata ushauri wa Mheshimiwa Makamu wa Rais kwamba kazi ya askari wa usalama barabarani inahitaji busara na sio kukomoana.
Ni kuelekezana pia. Lakini trafic polisi wetu baadhi yao hekima hii imewapitia kushoto. Wana kazi ya kukomoa kama vile wana visasi na madereva. Mungu awasaidie kujitambua.