Mzee mtambuzi ,huwa nashikwa nashauku fulani hivi nikiona post zako leo nimejikuta nasema oh !afadhali! Tena kwa sauti maana hunipa utulivu kwa kiasi flani na concentration sana,asante sana.ninasikitika kusema kwamba binadamu wengi kwa sasa wamepoteza ile childish heart mtambuzi,hasa sisi wanawake tu wanyama na tena watu wengine hudiriki kutuita mashetani ni sawa kabisa penye ukweli lazima niseme mtanisamehe ,kuna watu wan roho mbaya sana mfano:iliripotiwa yule mwanamke aliyemnywesha wifi yake maji aliyosagia vipande vya chupa vilivyomsababishia kukosa hajakubwa alafu akamwagia maji moto sekemu za siri huu ninini kam sio ushetani jamani,unamkuta mama anamtesa mtoto wa kambo anamfanyisha kazi,wakwake wanakaa sebuleni chakula nacho anakuwa wamwisho inshort mtambuzi watoto wanateseka kuliko watu wazima hapa tanzania sio mjini hata vijijini ,hasa mama wa kambo.ninafurahi binafsi kusema hivi sikupewa roho ya unyanyasaji kabisa,namshukuru mungu childish heart haijatoweka n ninaishi kwa misingi hii mikuu miwili niliyoipata kutokana na experience yangu ya miaka inayozidi 25 kwamba hapa duniani ninapita tuu siishi milele,na ninaamini ngome yangu ikianguka nyingine itasismama ambayo nitakuwa sina maamuzi nayo,kwa hiyo ninaishi relax sana ,ninaishi nandugu wengi katika familia na pi mtoto wa kambo ninaye siwezi mnyanyasa kabisa na mungu anisaidie.
Pia wanawake wengi hawaitambui siri ya urembo ukitaka mwanaume azidi kukupenda sana mpende mtoto wake kama wako hata vikipita visweta mnunulie wake yule wako mwache utaona jambololote jema kama huwezi kuwafanyia watoto wote mtangulize wakambo kwanza utaona fuata huu ushauri wangu,.
Nina mfano huu:kuishi na watu vizuri nilijifunza kutoka kwa mama yangu japo sio kwa kiasi kikubwa marehemu mama yangu alikuwa ni mke wandoa wa baba yangu ila baba yangu alikuwa na mke mmja wakisomali na alizaanaye mtoto mmjamwaka 74, mama yetu alimpenda sana kaka yule na tuliishi wote ,mama yakle alikuja kukaa kwa bibi .mamayetu wakati anafariki alimwita huyu kaka yetu akatukabidhi kwake ,baada ya muda baba akahama home yule kaka yetu alitutunza sana ada ya shule matumizi ukiishiwa unamwambiaetc,alitubeba mpaka tukamaliza form six wote tukaenda chuo kikuu nasasa hivi wote tumemzidi elimu maana alishindwa kuenda mbele akitusaidia tunyanyuke sisi.mpaka leo sijawaza nitampa nini ktk maisha yangu mama aliona mbali sana ,nahisi tungeishia mtaani wote ,asanteni