GE2025 Je, Ahadi za Uongo Wakati wa Kampeni za uchaguzi Zina Adhabu Kisheria?

GE2025 Je, Ahadi za Uongo Wakati wa Kampeni za uchaguzi Zina Adhabu Kisheria?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Wagombea wengi huahidi mambo makubwa wakati wa kampeni kama vile kujenga barabara, ajira kwa vijana, au elimu bure hata kama hawana uwezo wa kutimiza, Uutakuta mbunge anahaadi ujenzi wa barabara ya lami lakini kumbuka mbunge hawezi kujenga kwa hela zake mpaka akaombe hela bungeni na bunge liidhinishe huu sio uongo?

Lakini je, kutoa ahadi za uongo ni kosa kisheria? Kwa sasa, sheria nyingi hazitoi adhabu ya moja kwa moja kwa ahadi za kisiasa zisizotekelezeka, ila hatua zinaweza kuchukuliwa ikiwa kuna ushahidi wa udanganyifu wa makusudi kwa nia ya kupotosha umma kwanini wasichukuliwe hatua za haraka kwa uwongo wao mkubwa tena mbele ya umati wa watu? kama huwa wanachukuliwa hatua za kisheria ni zipi?

Ni wakati wa kuelimika: Hoja mbele ya ushabiki! Kagua ahadi, uliza maswali, piga kura kwa uelewa.
1753088852998.png
 
Nadhani watu wengi ni ngumu kuweza kuzijuia hizo sheria za kuwajibisha ila kwa kuwa matamshi ni ya muhusika awe ni Mbunge au Diwani na anaongozwa na chama fulani itakuwa chama ndicho chenye makosa kikatiba au kimiongozo kutokana na Ilani ya chama na pia ilan hizo zinaonesha wazi vipaumbele vyake katika muda fulani wa uongozi na kila kiongozi inabidi afwate ilani inasemaje kama mtoa ahadi atatoa ahadi nje ya miongozo hiyo basi tuakikishe huyo mtu ni tajiri kweli kweli pesa anazo yeye mwenyewe kwanza siyo kusubiria misaada kwa watu wengine ilishindikana
hvyo basi atoe ahadi kulingana na ilani yake inavyosema katika sehemu yake husika anayogombea tusiendeshwe kwa mihemko ya tamaa bila kuona mbele.
 
Back
Top Bottom