JB ametaja wachezaji wake watakaoimaliza Yanga kesho

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
8563bf8d3250f94e6bd172d339ca3a20.jpg

MSANII maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven ‘JB ‘ ambae ni shabiki wa kutupwa wa timu ya Simba ametamba kuwa kikosi chake hakiwezi kumuangusha kutokana na kuwa na washambuliaji wenye uchu ya kufunga.


Jacob Steven ‘JB’ ambaye amesema Simba kwasasa ipo vizuri sana katika safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Ibrahim Ajibu, Laudit Mavugo, pamoja na Juma liuzio hivyo basi Yanga lazima atasuburi kwa hawa watu watatu.


“Mimi naona hiyo mechi tunamfunga Yanga mabao mawili kwa bila huku wafungaji wakiwa ni vijana wanaojituma ili kurudisha heshima ya klabu yetu Simba ambao ni Ajibu na Mavugo,” alisema JB.


Aidha muingizaji huyo amewambia wapenzi wa Simba kuwa mwaka huu kombe la Ligi kuu Tanzania bara linaenda mitaa ya Msimbazi hivyo tuwasapoti vijana wetu katika mazuri ambayo wanayafanya na pia umoja wetu ndiyo ushindi wetu.
 
Back
Top Bottom