Jaribu kufikiria mazungumzo haya ya mke na mume

YNNAH

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
1,702
969
Mke: hivi mume wangu mi nikifa utaoa tena?
Mume: kwanini nisioe.? Nitaoa tu.
Mke: huyo mwanamke ataishi humu ndani?
Mume: ataishi humu na atakuwa anawatunza watoto wetu.
Mke: atalala kwenye kitanda hiki?
Mume: atalala hapa na mimi na tutakuwa tunaenjoy zaidi ya tunavyoenjoy sasa na wewe.
Mke: mi nikifa nitaacha nguo,je atavaa nguo zangu?
Mume: sina uhakika sana sababu yeye ni mnene sana kuliko hata wewe,nadhani atachagua zinazomtosha tu.
Je,unadhani nini kitafua ta baada ya jibu hilo?
 
baada ya hapo ni ngumi tuuuu kwa kwenda mbele kwani mke atakuwa ameshagundua kuwa mme tayari anae mwanamke tena mnene kuliko huyo mke wake kwa hiyo akifa tu anahamia
 
Kwa habari za kusikitisha bi mkubwa kafa na bi mdogo yupo ndani ya nyumba. RIP bi mkubwa
 
huyo jamaa nimemkubali, anajua kuua kwa maneno matamu. nashauri wengine waliowachoka wenzi wao watumie staili hiyo, na siyo wanaume tu, hata wanawake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom